Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume: Chanzo cha tatizo na ushauri wa jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume: Chanzo cha tatizo na ushauri wa jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo

Njia za kulimaliza tatizo la upungufu wa nguvu za kiume
Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunakuwa katika uwanja mpana zaidi wa tafakari za kibaiolojia na kisaikolojia walizonazo wanaume.

Lakini kwa kufupisha mlolongo wa mambo sehemu kuu tatu zinaweza kabisa kukidhi mchanganuo mzima wa jinsi tatizo hili linavyowasumbua wanaume wengi duniani.

Sehemu kubwa ya malalamiko ya wanaume katika sakata hili yanagusa zaidi maeneo matatu ambayo ni KUKOSA MSISIMKO, KUSHINDWA KURUDIA TENDO NA KUKOSA KABISA NGUVU, huku kufika kileleni mapema kukihusishwa pia kama pacha wa janga hili ambalo linawasumbua zaidi wanaume, ingawa na wanawake wanakabiliwa na sehemu ndogo ya tatizo hili.

Hata hivyo uchunguzi wa hivi karibuni uliowahusisha wanaume wanaofika kliniki au kupata tiba za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume umeonesha kuwa, si wanaume wengi wenye sababu za kibaiolojia zinazowafanya wakose nguvu za kiume, wengi wao huwa na matatizo ya kisaikolojia zaidi ambayo wahusika wanaweza kujiponya nayo bila hata kutumia vidonge wala dawa za miti shamba.

Ingawa Matabibu wanataja magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya zinaa, unene wa kupita kiasi, umri mkubwa kuwa ndiyo chanzo cha wanaume kupungukiwa na nguvu za kiume, lakini imebainika kuwa idadi kubwa ya wanaume wanaofika hospitalini kutafuta nguvu za kiume hawana magonjwa hayo.

Huu ni ushahidi kuwa wanaokabiliwa na janga hili wamebeba tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kimawazo zaidi kuliko hali halisi.

Ukweli wa mambo ulioibuliwa na wanasaikolojia umebaini kuwa, wale wote wanaolalamikia/lalamikiwa kuwa hawana nguvu iwe ya kufika kileleni mapema, kutokuwa na msisimko na kushindwa kurudia tendo wamekosa maarifa tu ya kufahamu na hawaijui miili yao na kwamba wanaishi kwa kusikia zaidi ya kujitambua.

Katika hali ya kawaida kila mwanadamu ameumbwa kwa namna yake na inapotokea kushabihiana basi ni bahati, lakini mara nyingi usawa hupatikana kwa mmoja kujifunza au kusaidiwa kufikia kiwango cha mtu anayemuhitaji kuwa nae katika maisha hasa ya kimapenzi.

Jambo hili wataalamu wanasema kuwa miili iko tayari kutii mafunzo na kubadilisha tabia zake kulingana na utashi wa mhusika.


Tatizo kubwa lililopo kwa wapenzi wengi wanaolalamikia upungufu wa nguvu ni kwamba maisha yao wanayachezea kwenye viwanja vya wenzao wanaokutana nao katika vijiwe na sehemu za kazi.

Usikivu wa mazungumzo toka kwa wanaume wengine wenye uwezo wa kwenda mara nne hadi saba katika tendo au wanatumia dakika arobaini kufika kileleni umewafanya wanaume wengi kujihisi tu kuwa wao wana kasoro eti kwa kuwa huishia mara mbili au moja katika kufanya tendo.

Dhana ya kujiona ni mwenye kasoro inapojengeka akilini mwa mwanaume, huchipua hofu na hatimaye kumfanya ashindwe kabisa kusisimka anapofikiria au kukutana na mwanamke.

Matokeo ya hangaiko la akili hushusha uwezo wa mwili na kumuongoza mtu kwenye kuwaza ugonjwa kisha kukimbilia hospitali au kwa waganga kutafuta tiba ya ugongwa ambao kimsingi hana.

Lakini ukweli uko wazi kwamba kukimbilia kutafuta uwezo wa kufanya mapenzi mara sita au saba hakumfanyi mwanaume awe mlinganifu mwenye kusifiwa na wanawake wengi, kwani si wanawake wote wana uwezo wa kufanya mapenzi kwa raundi hizo na si wote wanapenda kutumia takika 30 kucheza mpira wa kikubwa, wengine hukinai mapema na huona kero kuwa na wanaume ving’ang’anizi wenye sifa za kuganda wanapopewa.

Kwa kufahamu haya utagundua kuwa,kukimbilia kutafuta tiba ya kumudu kwenda mara saba ni jitihada mfu kabisa zisizohitajika katika maisha ya mwanaume hasa ukizingatia kwamba wenye uwezo wa kufanya mapenzi mara nyingi hawakuzaliwa hivyo, bali walijizoeza kupitia mazingira ya malezi na makuzi yao.

Maana hawezi kuwa mzoefu wa raundi kama alipokuwa mvulana alilelewa katika mafundisho ya kukatazwa ngono na kulindwa hadi akakakua.

Kadhalika hawi hodari wa kimapenzi kama ni msichana aliyefundishwa kujitunza, yote yatakayofuata kwa mvulana au msichana humea baada ya kupandwa na tabia chipukizi za ukubwani.

Kwa msingi huo mwanaume ana jukumu la kuutengeneza mwili wake uwe katika staili aitakayo.

Ndiyo maana kuna wengine hawamudu kulala bila kufanya ngono, hii ikiwa na maana kuwa wamejizoeza tu, si kwamba wameumbwa na nguvu hizo.
 
Unawahi kufika kileleni? Unachelewa kupata nguvu za kurudia tendo? Dawa ni hii!

Uwanja wetu wa leo, utakuwa na kazi moja tu, kujadili tatizo la kuwahi kufika kileleni, kuchelewa kupata nguvu za kurudia tendo, chanzo na tiba yake. Dhumuni la kuandika mada hii limetokana na maoni ya wasomaji wengi.

Wasomaji hao ambao wengi ni wanaume, waliniomba niwaandikie hivyo ili kunusuru uhusiano wao. Wengine wapo kwenye ndoa, kwahiyo waliniambia kuwa ushauri wangu unaweza kuwa tiba timilifu kwao.

Hivyo basi, kutokana na kutambua umuhimu wao, ndiyo maana sijasita kuandika haya unayoyasoma.

Tatizo la kuwahi kufika kileleni, mara nyingi huendana na mambo mengine ambayo huchagiza wenzi wengi kusalitiana ama kutengana kabisa.

Wanawake wengi wanagombana na watu wao kwa sababu kama hizi, hawavutiwi kuwaona waume wao wakiwahi kufika kileleni, hivyo kushindwa kuwapa dozi inayotosheleza.

Wanasikitishwa na hali ya wenzi wao ya kukosa nguvu za kutosha wakati wa kufanya tendo la ndoa ama ugoigoi wa kuchelewa kurudiwa na nguvu za kufanya kweli.

Aidha, wanakosa amani wanapobaini kwamba wapenzi wao hawana msisimko wakati wa kufanya yale mambo yetu. Hata hivyo, tunapogeuka kisaikolojia hili si tatizo kubwa, bali linahitaji kutuliza akili.

Ninaposema kutuliza akili, nakuwa namaanisha kuwa wengi hawana magonjwa yanayohitaji dawa, isipokuwa wanasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia tu.

Vijana na baadhi ya watu wazima wengine wanaenda kwa waganga na wakati mwingine wakijikuta wanajiingiza katika matumizi ya mitishamba bila kuelewa kwamba ugonjwa wao haupo kwenye kasoro za kimaumbile, bali upo akilini.

Hapa nataka tukubaliane kwamba jambo kubwa linalowasumbua wanaume wengi wanaodai kuwa hawana nguvu ni ukosefu wa elimu ya mabadiliko ya kibinadamu na ufahamu duni wa mbinu za kuwawezesha kucheza michezo ya kimapenzi kwa ufanisi.

Mpenzi ni sanaa pana, ina mafunzo mengi na ili uimudu, unatakiwa ujifunze kila siku mabadiliko yaliyopo. Sambamba na hilo, kujua mapito, mazingira, mabadiliko ya mwili na kuyakubali ni mambo ya msingi.

Pamoja na matatizo haya kuwakera wanawake kama nilivyotangulia kusema, huwafanya wanaume kukosa amani. Mara nyingi wanaopata dosari hizi, hujihisi wana nuksi.

Hata hivyo, mshangao unaokuja hapa ni kwamba wanaume hupenda kutafuta mbinu za kutatua tatizo lao bila kuwashirikisha wenzi wao, kana kwamba wao haliwahusu.

Saikolojia inatambua kuwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ni zao la udhaifu wa mke na mume na sio la mwanaume peke yake kama watu wengi wanavyodhani.

Kwa mfano, mwanaume atapata wapi msisimko wa kimahaba kama mwanamke hatakuwa mtundu wa kubuni mbinu za kuufanya mwili uliopoa usisimke?
Atavutiwa nini mwanaume kurudia awamu ya pili, ikiwa kwenye mzunguko wa kwanza alikutana na harufu isiyofaa? Nakshi nakshi humuongezea mwanaume hamu ya kutaka tena na tena. Huo ndiyo ukweli!
Napenda niweke ukweli kweupe, mara nyingi tatizo la msisimko wa kurudia tendo, husababishwa na mwanamke mwenyewe. Kwa maana hiyo, ili litatuliwe ni lazima ziwepo juhudi za pande mbili.

Tuweke kituo kwa leo, nakuomba tukutane wakati ujao ili tuendelee na mada hii. Bila shaka, tutakapokutana ishu ijayo, utaweza kungamua mengi kuhusu somo hili. Mimi na wewe tupo together as one.
 
KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Wanaume wengi hapa duniani huamini kuwa, mwanaume hasa ni yule anayeweza kufanya tendo hilo kwa muda mrefu na mara nyingi ndio maana vijana wengi utawasikia wakijisifu kuwa, mpenzi wake hakulala usiku mzima kutokana na dozi ya maana aliyompa na ukimuuliza mtu wa namna hii atakwambia kuwa alikwenda mizunguko sita usiku mzima.
Hata hivyo, ukweli ni kuwa, watu wengi hufikia hatua ya kusema uongo ili waonekana kuwa ni wanaume hasa mbele ya wenzao huku wangine wakigubikwa na nadharia kuwa ukubwa wa uume unaashiria jinsi gani walivyo wanaume kitu ambacho si kweli.

Ni mtazamo huu ndio unaowafanya wanaume wakitaniwa au kuambiwa kuwa wako kama wanawake wanaweza waue mtu. Tunaamini kuwa uanamke ni udhaifu na uanaume ni ushujaa fulani hivi.
Wakati hali ikiwa hivyo, hivi sasa wanaume wengi wamekuwa wakihangaika na jambo moja kubwa, kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume ili kujiongezea heshima faragha!
Ukitaka kuthibitisha hili jaribu kuangalia karibu katika kila gazeti utakalo soma, ni nadra sana kukosa tangazo dogo la biashara lililotolewa na mganga wa kienyeji anayejigamba kuwa anazo dawa za kuongeza nguvu za kiume, na matangazo hayo hayaishii magazetini tu, bali hata redioni pia yapo.
Mbaya zaidi dawa zinazoongelewa hupewa majina mengi ya kusisimua kama kombora, simba na nyati siushasikia mziki wa nyati akikasirika sasa jenga picha nuvu ya hiyo dawa, hata hivyo, dawa nyingi ni uzushi tu na hupewa majina hayo ili kuwavuta wateja na kuwashawishi kuzijaribu, enewei ndivyo biashara zilivyo.

Wingi huu wa matangazo umeanza kuonekana katika miaka ya hivi karibuni, na kadiri siku zinavyozidi ndivyo idadi ya waganga wanaojigamba kuwa na dawa hizo inavyozidi kushamiri, kuna waganga wenye dawa za Kiswahili, Kiarabu na za Kichina ndio usiseme!
Binafsi utitili wa matangazo haya umenifanya niamini kuwa, kuna tatizo kubwa la wanaume kupungukiwa nguvu hizo, na ingawa hakuna utafiti wa kitaalamu uliofanywa rasmi, lakini inaonyesha kuwa tatizo hilo kwa sasa ni kubwa sana na si Tanzania tu, bali ni dunia nzima.

Kutokana na hali hiyo ndipo waganga wa kienyeji pamoja na makampuni mengi makubwa duniani hujaribu kuelekeza nguvu zao katika kufanya utafiti wa kutengeneza dawa za kusaidia watu wenye tatizo hilo, na bahati nzuri kwa makampuni na waganga hao ni kwamba inaonekana kama biashara inawaendea vizuri.
Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi moja ya biashara ya dawa za aina hiyo nchini Uingereza, imebainika kuwa asilimia 46 ya wanaume nchini humo hutumia dawa hizo, hata hivyo wengi wao huzitumia bila ya kupata ushauri wa daktari na maduka mengi ya dawa yametozwa faini kwa kuwauzia dawa hizo bila ya kuwa na vyeti vya daktari.
Kupungua kwa nguvu miongoni mwa wanaume wengi kumesababisha wengi wao waishi katika maisha na hali ya usononekaji na wengine wamekumbwa na umauti kutokana na hali hiyo ya kuishi na sononi kwa muda mrefu.

Kuna mambo mengi yanayosababisha wanaume wengi wajikute wakipungukiwa nguvu za kiume, wataalamu wa masuala ya saikolojia wanaamini kuwa mara nyingi suala hilo, hasa kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 45, husababishwa na msongo wa akili kuliko ufanyaji kazi wa misuli ya mwili.

Watu wengi wanaofikiri kuwa wamepungukiwa na nguvu hizo huwa hawako hivyo, inasema sehemu moja ya utafiti uliofanywa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Havard, nchini Marekani na kufafanua kuwa:

Tatizo la watu hao huwa ni kushiriki tendo hilo kwa wakati usio muafaka kwao, wanashiriki wakati bado hawajajitayarisha kiakili au wanapokuwa wamejitayarisha, basi njiani hukutana na wenzi ambao hawaafiki mwelekeo wa safari yao.

Wataalamu wa masuala ya vyakula nao wanaeleza kuwa tatizo hilo huwapata wanaume wengi kwa sababu ya utumiaji wa vyakula vyenye kuongeza kiwango kikubwa cha mafuta mwilini ambao hawashiriki katika mazoezi ya viungo ambayo huifanya misuli ya damu mwilini kutokufanya kazi vizuri na hivyo kusababisha matatizo mengi ya mwili kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

Kumbukumbu yangu inaonesha kuwa, Mheshimiwa Mbunge wa Viti maalumu kuputua tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Janet Bina Kahama, 10 Aprili 2007 katika kikao cha saba cha bunge aliulizwa swali ambalo lilikuwa namba 8 lenye kipengele a, b, na c ambapo kwenye kipengele b aliuliza: Je, serikali inafahamu ni sababu gani zinasababisha kupungua kwa nguvu za kiume kunakotangazwa sana na waganga wa jadi?

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Homeli Mwakyusa alijibu kuwa, Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi, baadhi yao ni lishe duni hasa mboga za majani, kutokula aina mbalimbali za jamii ya karanga (nuts), matumizi yasiyofaa ya ulevi kama pombe, sigara na dawa za kulevya, dawa zinazotibu baadhi ya magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya akili na vilevile kutopumzika kunakosababishwa na shughuli nyingi za kijamii hivyo kusababisha uchovu.

Lakini ni kweli dawa hizi za asili zinauwezo wa kutatua tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Pro. Mwakyusa anathibitisha kwa kusema kuwa, dawa nyingi za tiba asili ni virutubisho ambavyo muhitaji angeweza kuvipata endapo angekula vyakula vyenye virutubisho hivyo.

Pamoja na kuwa dawa hizo hazijafanyiwa utafiti wa sayansi ya leo na kutokana na unyeti wa usiri wa watumiaji wa dawa hizo zingekuwa na madhara zisingetumiwa na wananchi hata huko zinakotoka yaani maeneo yake ya asili.

Na kusisitiza kuwa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii haijapokea taarifa ya tukio kutoka kwa walalamikaji wanaotumia dawa hizo za kuongeza nguvu za kiume.

Hata hivyo, hali ni tofauti kidogo katika nchi zilizoendelea kama Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya, matumizi ya dawa hizi hutolewa kwa watu baada ya kuandikiwa cheti na daktari, na watu wenye matatizo ya msukumo wa ndamu (BP), mara nyingi wamekuwa wakishauriwa kutotumia dawa hizo kwa sababu ni hatari kwa maisha yao.

Hii ni kwa sababu dawa nyingi, kama Viagra, Ciallis, Levitra, Yohimbine na nyingine mbali ya kuwa na nafasi ya kusababisha magonjwa ya moyo, kwa watu wasiokuwa nayo, pia yana madhara mengine kama vile kusababisha upofu na kuleta hali ya mwili kuwa na kitetemeshi.

Madhara mengine ya dawa hizo ni pamoja na kumsababishia mtumiaji hali ya kuumwa na kichwa mara kwa mara, macho kuwa mekundu, kuziba kwa hewa puani na maumivu ya tumbo pamoja na kuharisha.

Haya ni aina ya madhara yanayotokana na dawa za kizungu, ambazo kabla ya kuingia madukani kufanyiwa utafiti wa kina kuangalia madhara yake kwa watumiaji, na ingawa hayo yote yanafanyika lakini bado athari zake kwa watumiaji zinaonekana.

Mwandishi na muandaaji mkongwe wa filamu nchini ambaye kwa sasa anaishi Marekani, Chemi Che-Mponda alishawahi kuandika makala isemayo ‘kukosa nguvu za kiume si mwisho wa dunia!' na katika makala hiyo kulikuwa na hadithi hii isome ili ujue kinachoweza kukutokea kwa kujifanya mjuaji na kuagiza dawa za kuoneza nguvu kwenye mtandao.

Chemi alianza hivi: "Jamani, jamani, jamani, kuna jirani yangu kafa hivi majuzi. Alikuwa ni baba wa makamu, mmarekani mweusi. Alikuwa mcheshi na ilikuwa kila tukionana lazima tusalimiane.
"Mara ananinunulia kahawa halafu tunakaa namsimulia kuhusu Afrika. Yule baba, alionekana mzima na mwenye afya fiti kabisa. Nilibakia kushangaa kusikia kafa na si kwa ajali. Mke wake alifariki mwaka juzi, lakini miezi ya karibuni alikuwa anaonekana mwenye furaha kwa vile alipata mpenzi, dada mwenye miaka 25 hivi.

"Story niliyosikia ni hivi: Kumbe jamaa alikuwa na matatizo ya moyo. Alifia kitandani akiwa kwenye shughuli ya kufanya tendo la ndoa na mpenzi wake. Tena wanasema alifariki mara alipofikia kilele cha tendo."Navyosikia ilikuwa ni ‘massive heart attack'. Kama ni massive bila shaka na utamu wa shughuli hakujua kuwa yuko hatarini. Mpenzi wake alipiga sana kelele, majirani walipigiga simu 911 (polisi) kwa vile walidhania wameingiliwa na majambazi.

"Kumbe jamaa alikuwa mtumizi wa Viagra, yaani vile vidonge vya kuongeza uume, na kumpa mwanaume uweza wa kufanya tendo la ndoa. Ndugu zake wanalamika kweli, maana hakuzipata kwa prescription (maelezo) ya daktari, alizaiagiza kwenye mtandao (internet).
Hiyo ni baadhi ya mifano hai inayoonesha wazi madhara unayoweza kupata kwa kuamua kutumia tu dawa bila maelekezo kutoka kwa daktari!

Binafsi nina hofu juu ya dawa ‘za kienyeji' zinazotengenezwa na waganga na kuuzwa kama karanga kila kona ya miji mbalimbali ya Tanzania bila ya kufanyiwa utafiti wa kina, ni wazi kama kanuni za kiafya zinavyosema, kuwa kila dawa ina madhara yake, lakini je, ni nani anapima madhara mabaya yatokanayo na dawa hizi za kienyeji zinazouzwa kama njugu?

Ukiacha madhara yatokanayo na dawa hizo, pia wanaume wengi hukumbwa na tatizo hili la kupungukiwa nguvu kwa sababu ya uvutaji wa sigara kwa wingi, utafiti mbalimbali wa kitabibu duniani unaonyesha kuwa matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku huwasababishia wanaume upungufu wa nguvu hizo.

Ni kweli ulio wazi kwamba tatizo la wanaume wengi kupungukiwa nguvu za kiume nchini kwetu na duniani kote linazidi kushika kasi na tiba mbadara zinahitajika ili kurudisha heshima na furaha miongoni mwa wanaume wengi duniani, lakini utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu haupaswi kufanyika kiholela kwa kuzingatia kuwa matatizo yake kiafya ni makubwa kuliko faraja ya muda mfupi anayopata mtumiaji!

Siku moja nilikuwa nimekaa kwenye kijiwe cha kahawa Kariakoo jijini Dar es Salaam nikachokonoa wazee kwa kuchomekea mada hii, mambo mengi walinieleza lakini kubwa zaidi ni kuwa, vijana wa siku hizi wanakubwa zaidi na tatizo hili kutokana na kufakamia vyakula visivyo vya asili na kusahau kuwa, miogo, asali, karanga na pweza huweza kukusaidia ukawa na nguvu kama nyati. Vyakula vingi vinavyoingizwa nchini vikiwa vimesindikwa ambavyo vijana wengi hukimbilia na kujiona kuwa, babu kubwa wakivila hivyo na kumcheka mzalendo anayepata muogo wa kuchoma na chachandu huku akishushia na juisi ya mua pale Kariakoo bila kujua kuwa sehemu kubwa ya aina nyingi ya vyakula wanavyokula ni sumu yenye ladha nzuri inayonenepesha! Madhara yake ni mengi na miongoni mwake ni kuwasababishia watumiaji kukosa nguvu za kurudia tendo.

Hata hivyo, kuna wakati pia upendo unapopungua na mvuto unapungua baina ya wanandoa, mwanaume anaweza kujikuta kila akiwa faragha anashindwa kuendesha gari kwa muda mrefu na anaweza kudhani kuwa ana matatizo kumbe hali hiyo inamkumbwa kutokana na kutokuvutiwa na mwenzi wake.

Tatizo kama hili linaweza kutatuliwa kwa kumueleza wazi mkeo ama mpenzi wako jinsi gani anaweza kujipanga na kuonekana na mvuto wa hatari utakaokufanya uchanganyikiwe kila umuonapo na hata mkiingia kwenye mambo fulani basi kwa hakika utahamasika na kutoa dozi ya maana.

Uchovu wa kazi za ajira
Mkufunzi wangu wa saikolojia katika Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa ambaye ameshatanulia mbele za haki, Pro. Samuel Mshana (Mungu amlaze mahali pema peponi) aliwahi niambia kuwa wanawake wanataka security kutoka kwa mwanaume nami nikamtania Pro. Sasa mbona mimi na mwili mdogo nitampa ulinzi gani mwanamke akacheka kisha akaniambia ulinzi naouzungumzia ni wa jumla ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mambo yanakwenda sana ndani ya nyumba yani watoto wanakwenda shule na mambo ya mlo wa uhakika.

Hivyo ni wazi kuwa wanaume huhangaika kwa kiasi kikubwa kuhakikisha wanamudu majukumu yao ya kila siku na huko makazini kuna mauzauza mengi na usiombe ufanye kazi kwenye kampuni binafsi kila kukicha wewe upo roho juu sasa katika hali kama hiyo ukikutana na mwenzi wako kunako majambozi utahisi una upungufu wa nguvu za kiume kwani mara tu baada ya kumaliza mshindo wa kwanza hutoweza kurudia tena! Hali ni hivyo hivyo kwa watu wanaofanya kazi nzito zinazosababisha wajikute wanarudi majumbani wakiwa wamechoka.

Hivyo basi, endapo nawe ni miongoni mwa watu wanaokumbana na tatizo la kushindwa kurudia majambozi kwa sababu ya uchovu na msongo wa mawazo kutoka kazini hakikisha unapanga muda muafaka na mwenzi wako kupeana raha.

Mfano kama Jumamosi unafanya kazi nusu siku ukitoka usiende kulewa kama ni mtu wa kinywaji bali nenda kapumzike kisha kesho yake waweza kumtoa out mama na kwenda mazingira tofauti kupeana kitu roho inapenda hakika utajishangaa jinsi utakavyomudu majambozi.

Kuchacha
Nakumbuka vema miaka ya 1990 enzi hizo Redio Tanzania pekee ndio ilikuwa ikitupa burudani na moja kati ya nyimbo ambazo ilikuwa ikinikuna ni kuchacha usiombee' iliyoimbwa na Juwata Jazz na hichi ni kibwagizo chak Maradhi yote ugua lakini kuchacha usiombe ebwana usije ukawa katika hali mbaya kifedha na kila jambo unalolipanga linakwenda ndivyo sivyo hali inayokusababishia uchache kisha mwenzi wako akakuomba unyumba hapa kuna mawili ama kuchelewa sana kufika safari yenu ama kumaliza halaka kisha jamaa analala chapchap na hataki tena kuonesha ushirikioano hata mamaa akimbembeleza vipi!

Hivyo basi, si vema kukutana kimwili na mwenza wako kipindi ukiwa umechacha kwani wanaume wengi pindi wanapokuwa na msongo wa mawazo hukimbilia kuomba unyumba kwa wenzi wao wakiamini kuwa, wao ndio watawasaidia kuwapunguzia mawazo badala ya kutafuta njia mbadara ya kumaliza tatizo.

Kuishiwa hamu ya nyama na mapishi yale yale kila siku
Uzoefu wangu unanionesha kuwa wanaume wengi hujikuta wakikosa hamu ya kurudia tendo la ndoa mara bada ya kumnaliza mzunguko wa kwanza kutokana na wake zao kutowaonesha ubunifu yaani kila siku ni kifo cha mende tu hakuna jipya linaloongezwa hata nakshi za miguno ni ile ile hali inayosababisha wanaume wakose hamy ya kuendelea mara baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza.

Wanaume wengi hujikuta wanalazimika kutafuta kimada ili kupata radha mpya na huko mambo huwa mulua kwani hufanikiwa kwenda raundi hadi tatu na bado akawa na hamu kwa vile tu amekutana na vitu adimu hivyo basi, mwanaume anapaswa kumueleza wazi mkewe kuwa anahitaji wakutane faragha ambapo anataka vutu hadimu vya kabatini na si kumsaliti mwenza wako kwani uwezo wa kumfanya awe bora kunako majambozi unao wewe mnwenyewe mwanamme.

Mfano siku akikwambia anakwenda kwenye kitchen party mruhusu kisha akiwa huko mtumie meseji kuwa, "mpenzi najiandaa kumalizia sehemu ya pili ya soma ulilojifunza yaani la vitendo, hakika leo nitafaidi" asikdanganye mtu hapo hata kama bi. Harusi mtarajiwa hakufundishwa mambo fulani ya kumpagawisha mumewe atahakikisha hakuangushi atakuja na mambo mapya na hapo ndipo mwanaume hujikuta akiganda kifuani.

Nimalize kwa kusema kuwa, hakuna haja ya kukurupuka na kukimbilia kununua dawa za kuongeza nguvu ya kiume bila kutafakari kwa kina chanzo cha tatizo lako kwani yawezekana tatizo ulilonalo linaweza kutatulika kwa njia nyingine ambazo hazitakufanya uwe hatarini.
 
wape hao wazee wa kimoko chali lakini naona kila unapogusa mambo fulani wanakuwa wanakutoa ktk line mie naona upo poa ile mbaya nipe waeleze unajua wabongo ukigusa maini wanajifanaya wakali
wangu nipe kuhusu wale wanaopenda kula kiboga athari zake
 
Hivi ni kweli wanaoumwa ugonjwa wa ngiri hawawezi kurudia tendo kabisa.Na pia tendo la kwanza linaisha baada ya mda mfupi sana
 
Hivi ni kweli wanaoumwa ugonjwa wa ngiri hawawezi kurudia tendo kabisa.Na pia tendo la kwanza linaisha baada ya mda mfupi sana

Siyo Kweli kuwa ukiwa na ngiri ndio utashindwa kulirudia tena tendo la mapenzi kitandani .Ninavyojuwa mimi Mshipa wa Ngiri ni ugonjwa kama magonjwa mengine yanayowapata Wanaume, ila inategemea wakati ukiwa unafanya tendo la kimapenzi na kwa gafla Mshipa wa ngiri ukakupata hapo hutaweza kulirudia tena tendo la Kimapenzi, utakuwa unaumwa na nguvu zinatokana na uzima wako.

Matatizo ya nguvu za kiume yanatokana na Mambo mengi lakini iliyokuwa kubwa ni Vyakula tunavyokula vinachangia sana ukosefu wa nguvu za kiume, ikiwa wewe kila siku utakuwa unakula chakula kimoja siku zote nafikiri hutaweza kulirudia tena tendo la kimapenzi kitandani .

Itabidi tuwe tunakula vyakula vya kila aina mboga za majani matunda, samaki na kadhalika. Tutaweza kuwa na Nguvu za kiume. Na kitu kingine tuache sisi wabonge kujichuwa chuwa ukiwa wewe upo Toilet kupiga Punyeto hiyo inachangia sana kupunguza Nguvu za kiume ikiwezekana tuache mtindo wa kupiga Punyeto.

Huo ndio Ushauri wangu asante.
 
Asante Sana!

Mzizimkavu! Inakuwaje sasa kwa mwanamke mwenye mataitizo kama hayo ama yule asiyetaka kurudia baada ya round ya kwanza ilhali unajua kuwa hakufika kileleni?
Mchezee chezee sehemu zake za siri huku unamnyonya maziwa yake kwa taratibu huku ukipapasa mwili wake wote na vidole vyako vipo sehemu zake za siri uwe unafanya kwa taratibu huku ukitafuta wapi panpomfanya awe na nyege kimapenzi ndipo utampata vizuri kimapenzi na yeye mwenyewe atakuambia umfanye kimapenzi yaani umuingilie ndipo hapo utakapomfanya kimapenzi.
 
Mambo yanayochangia Upungufu wa nguvu za kiume

LEO ninataka tuangalie kwa kina mambo yanayochangia tatizo hilo upungufu wa nguvu za kiume. Ningependa tulio katika ndoa, ukishaisoma makala hii tuwahusisishe wenza wetu nyumbani au mpigie rafiki yako na kumueleza kuwa ana nafasi ya kujilinda kupoteza

nguvu za kiume na hivyo kuwa na uhakika wa amani nyumbani.
Nasema amani kwa sababu tatizo hili huingilia amani nyumbani kwani kuna kuhisiwa kuwa mwanaume anajihusisha na nyumba ndogo maarufu. Uzoefu katika vituo vyetu vya Marie

Stopes kina mama ndio huja kutafuta ushauri kwa nini mzee kabadilika na wafanye nini ili kumrudisha nyumbani. Zifuatazo ni sababu amabazo kitaalamu zinatajwa kuchangia kupungua kwa nguvu za kiume na nyingi kama si zote zinaepukika.

Msongo wa mawazo: Ni dhahiri kuwa akili na tendo la ngono vinategemeana sana. Inajitokeza mara nyingi sana kwa watu wenye matatizo katika biashara, kazini na sehemu nyingine hujikuta hawako katika hali ya kuwa na hamu ya tendo la ndoa mpaka pale

watakapotulia. Hii inaweza kuwapata watu wa rika zote na tatizo hili linaweza kuisha haraka kutegemeana na shughuli zao zinavyorudi katika hali ya kawaida

Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu. Mzunguko wa damu mwilini una maana sana kwani kama damu haizunguki vizuri itachangia uume kutosimama vizuri kwa sababu usimamaji hutegemea kiasi na kasi ya damu inayoingia kwenye mishipa ya sehemu hiyo. Dawa zinazotumika kutibu shinikizo la damu huchangia pia kupungua kwa nguvu za kiume.

1. Unywaji pombe kupita kiasi: Pombe inaweza kuathiri mishipa ya damu na mishipa ya fahamu kwa wakati mmoja. Wakati mwingine mtu akilewa sana huathiri ubongo na kukata mawasiliano kisaikologia na hivyo kushindwa kuwa katika hali ya kuwa na hamu ya ngono na hivyo kutosimamisha.

2. Unene. Unene huwa unaambatana na mafuta mengi mwilini. Mafuta hayo wakati mwengine huzidi kwenye kuta za ndani za mishipa ya damu na hivyo kupunguza ukubwa wa mrija kiasi kwamba damu inipita kidogo na kwa shida. Hii huchangia kupungua kwa nguvu za kiume kwa sababu kiasi cha damu kinachotakiwa kisimamisha uume kitakuwa kidogo sana. Wakati mwingi uume unaweza kusimama kidogo na kulala kabla shughuli haijakamilika.

3. Kutokufanya mazoezi: Tusipofanya mazoiezi pia mzonguko wa damu kutokuwa mzuri na hivyo kutoparuhusu damu ya kutosha kusimamisha uume. Kwa watu wanaotembelea magari na shughuli za kukuaa maofisini mda mrefu na hasa kama hawafanyi mazoezi asubuhi au jioni wako kwenye hatari zaidi kuliko watu wanotembea kwa miguu mwendo mrefu na kufanya kazi ngumu za kuuchosha mwili.

5. Matatizo ya kisukari: Kisukari ni ugonjwa unaoathiri mishipa ya fahamu na kufanya mishipa ya damu kutofanya kazi yake viuri ili kuruhusu damu kujaa kwenye uume. Hii himfanya mgonjwa wa kisukari kushindwa kusimamisha hata kama ana hamu ya kufaya tendo hilo.

5. Umri: Inaelezwa kuwa kadri umri unavyopanda ndio uwezo wa nguvu za kiume utaendelea kupungua. Baadhi ya watu huanza kuona tatizo hili wanapofikia umri wa miaka 40 na kuendelea na hasa kama maisha yao hayakuwa na mazoezi ya mwili. Sababu

nyingine ni kama utumiaji madawa ya kulevya, kuumia katika uti wa mgogongo, uvutaji sigara nk. Sababu nyingi zinachangia kupungua kwa nguvu za kiume zinaepukika kwa hiyo tunashauriwa kuwasiliana na wataalamu ili kujifunza jinsi ya kujikinga au kutibu matatizo

hayo. Kwa ushauri piga simu 0655744433 kuanzia jumatatu mpaka ijumaa saa kumi mpaka saa kumi na mbili jioni au tuma email kwenda info@mst.or.tz

Chanzo: Mambo yanayochangia upungufu wa nguvu za kiume.
 
Ahsantwe mkuu, shule tosha kabisa. I gotta lecture from your writtings.
 
Nasikia punyeto pia hupunguza nguvu za kiume,kama ndio plz fafanua.
 
Dawa ya kuongeza nguvu ya kiume, Dawa ya kuongeza nguvu ya kiume nambari moja barani Africa, ina vitamini na virutubisho. Dawa hii haina madhara yeyote, watu wengi wametumia imeonyesha mafanikio makubwa, kwa kazi tatu:-
1. Kukakamaa kwa uume wakati wa tendo la ndoa.
2. Uzalishaji wa mbegu za kiume yaani kuwa na manii mengi.
3. Kuchelewa kukojoa manii.
Dozi
Dawa yenyewe iko katika hali ya maji iliyochanganywa na asali mbichi na dawa inaitwa
HARAI.
GHARAMA:
USD. 250 kwa dozi ya siku 21.
Tiba ya kurefusha maumbile kwa urefu na uneneHii dawa hutumika kwa watu wenye maumbile madogo ya uume wa nchi mbili kurefusha mpaka nchi saba, dawa hii haina madhara na watu wengi wametumia kwa jili ya kurefusha maumbile yao na kuonyesha mafanikio makubwa
Vitu visababishavyo mtu kuwa na maumbile madogo ni:-
1. Wakati akiwa bado mdogo alikuwa hapashwi maji ya moto sehemu ya siri.
s
2. Kuwa mnene sana.3
3. Kuishiwa nguvu za kiume

Dozi
Kwa wenye matatizo haya dawa yao ya kutumia ni

1. Kuchanja sehemu ya siri
2. Kunywa
3. Kupaka
Gharama ya tiba hii ni USD 350

source: tovuti ya dk manyuki
 
Dawa ya kuongeza nguvu ya kiume, Dawa ya kuongeza nguvu ya kiume nambari moja barani Africa, ina vitamini na virutubisho. Dawa hii haina madhara yeyote, watu wengi wametumia imeonyesha mafanikio makubwa, kwa kazi tatu:-
1. Kukakamaa kwa uume wakati wa tendo la ndoa.
2. Uzalishaji wa mbegu za kiume yaani kuwa na manii mengi.
3. Kuchelewa kukojoa manii.
Dozi
Dawa yenyewe iko katika hali ya maji iliyochanganywa na asali mbichi na dawa inaitwa
HARAI.
GHARAMA:
USD. 250 kwa dozi ya siku 21.
Tiba ya kurefusha maumbile kwa urefu na uneneHii dawa hutumika kwa watu wenye maumbile madogo ya uume wa nchi mbili kurefusha mpaka nchi saba, dawa hii haina madhara na watu wengi wametumia kwa jili ya kurefusha maumbile yao na kuonyesha mafanikio makubwa
Vitu visababishavyo mtu kuwa na maumbile madogo ni:-
1. Wakati akiwa bado mdogo alikuwa hapashwi maji ya moto sehemu ya siri.
s
2. Kuwa mnene sana.3
3. Kuishiwa nguvu za kiume

Dozi
Kwa wenye matatizo haya dawa yao ya kutumia ni

1. Kuchanja sehemu ya siri
2. Kunywa
3. Kupaka
Gharama ya tiba hii ni USD 350

source: tovuti ya dk manyuki
Mkuu dawa yako inaonyesha ni nzuri lakini mbona Ghali sana?
 
mkuu unairecommend dawa hii?
Sija ku recommend hiyo dawa kama una matatizo kama hayo jaribu kuni (PM) nitaweza kukusaidia tu usiwe na wasiwasi lakini unieleze kwa kirefu matatizo yako ndio naweza kukusaidia kuliko kunificha asante.
 
vipi masterbution nayo haimo? km haimo nini madhara yake kitaalam?
 
Nimeulizwa swali hilo"kuongeza Nguvu za Kiume hasa ni nini kinacho lengwa?" Je,

i) Ni kuongeza uwezo wa kucheza round nyingi ktk mechi?
ii) Ni kuongeza uwezo wa kuhimili kwa muda mrefu ili kukamilisha raound ktk mechi?
iii) Ni kuongeza kiasi (volume) ya vitu vinavyokuwa discharged wakati wa kukamilisha round?
iv) Ni kuongeza uwezo wa mzee wakazi kusimama kwa u imara kama ukuni mkavu nasi kuwa legelege

Wana JF msaada tafadhali
 
Back
Top Bottom