Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume: Chanzo cha tatizo na ushauri wa jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo

Dini zote zinapinga. Tamaduni za kiafrika zote zinapinga. Huo ni upuuz, acha mara moja.
 
<br />
<br />
khaa.!hii kiboko. Bao 42..! Inaelekea alikula mkuyat b4.
...Haaahaaahaaahaaahaaa inawezekana dogo alitaka kuweka record ili aingie kwenye Guiness book of the world..Bao 42 ni wazi kuwa itafika hatua hatoi sperms tena ingawa atakuwa anasisimka...Dah hatari sana...
 
Jar&#305;bu kumsh&#305;r&#305;k&#305;sha Mungu kwa kumwomba hakuepush&#305;e na tamaa za mw&#305;l&#305;.
 
TATIZO la nguvu za kiume linaonekana kukua kwa kasi huku wengi wakiwa hawajui nini la kufanya. Kati ya wale ambao wanasumbuliwa na tatizo hilo ni vijana, hali inayofanya baadhi yao kubaki katika kitendawili wakijiuliza nini hasa kinasababisha wanakuwa katika hali hiyo.

Kuna kesi nyingi za wanaume kukimbiwa, sababu mojawapo ni baadhi yao kutokuwa na uwezo ambao mwanaume anapaswa kuwa nao, yaani kuwa imara. Wapo ambao kwa sababu ya tatizo hili, wamejikuta wanalazimika hata kujiua au kuchukua hatua yoyote mbaya.Lakini ukweli ni kuwa msingi wa maisha yenye mafanikio si kujiua wala si kujilaumu kwa kusumbuliwa na tatizo fulani, bali kuchukua hatua ili ulishinde tatizo hilo.

Tangu umezaliwa hadi leo umesumbuliwa na matatizo mangapi? Bila shaka ni mengi, na suluhu ya matatizo si kujiua, kujipa adhabu kwa kutokula ama kujilaumu kwa kuzaliwa, bila shaka hayo hayana msaada.

KWANINI KASI YA WANAUME KUWA NA TATIZO HILI INAONGEZEKA?
Ziko sababu nyingi, lakini zilizo kuu ni hali ya maisha, kwa maana ya mabadiliko makubwa ya matumizi ya vyakula, kwa mfano zamani wengi walikuwa wakitumia vitu vya asili, sasa wengi wanatumia vyakula vya kiwandani ambavyo kwa bahati mbaya baadhi yake havina ubora.Badala ya kutumia juisi za kutengeneza kwa kutumia maembe kutoka mashambani, wengi wananunua juisi za viwandani ambazo baadhi yake ni mchanganyiko wa rangi usio na faida yoyote katika mwili.

Tatizo hili pia linatokana na ulaji usiofaa na usiofuata misingi ya afya bora; wengi wanakula ili tumbo limejaa, si wengi ambao wanaangalia kwanza chakula kabla ya kula. Ukweli ni kwamba kila chakula kina msaada wake, vingine vinasaidia mafuta, vingine nguvu, chuma na kadhalika.Lakini pia tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wengi wanaolalamikia kupungukiwa nguvu za kiume, hawajui hasa sababu na nini wafanye. Lakini ukweli ni kuwa baadhi yao wana tatizo hili kwa sababu wenzi wao si wenye kuwasaidia, si wajuzi.

Ndio kusema kama mwanaume anasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume, ni vizuri kuangalia limeanza lini, na kwanini. Wakati fulani wanawake kwa kauli zao zisizo za ushirikiano na matendo yao, yaweza kuwa ni sababu mojawapo ya kusababisha wanaume kutokuwa na nguvu katika tendo.Maana utakuta wanawake wengine wanawaambia waume zao "haya unataka, njoo basi nataka kuwahi au hutaki niondoke"&#8230;kauli kama hii haitii raha. Pia wengine hawana ushirikiano, yuko tu kama hayuko.

Raha ya ndoa haiko hivi, ni lazima mshirikiane vizuri, si ndio jamani? Raha ya ndoa ujuzi.Kwa bahati mbaya baada ya ndoa, si wengi ambao wanaendelea na ubunifu, tena kuna wengine ukiwaambia leo twende na ubunifu wa aina hii utasikia "eeeh weee unataka kunivunja kiuno mwenzako, haya mambo ya vijana haya". Je, hali ya ndoa yako ikoje?
&#8232;&#8232;Mapenzi yanahitaji usafi, lakini wapi bwana kuna mwingine ukiwa naye unaomba Mungu akuachie haraka&#8230;.ananuka, hakuna maandalizi, anakuvamia bora hata kuku atacheza huku atacheza kule.
Kwa bahati mbaya zaidi kuna wengine wakiambiwa ukweli utasikia wanasema kwa nyodo, aaah bwana eeeh wafuate hao wanaojua!Ndugu yangu raha ya ndoa mpate muda wa kucheza, kuzungumza mazuri na kuonyeshana upendo wa dhati, ikiwa ni pamoja na kutimiza mazuri mliyoahidiana wakati mnaingia kwenye ndoa.

Sio wanaume wengi wenye sababu za kibaiolojia zinazowafanya wakose nguvu za kiume, isipokuwa wengi wao huwa na matatizo ya kisaikolojia zaidi ambayo wahusika wanaweza kujiponya nayo bila hata kutumia dawa za miti shamba.

Kuna sababu kadhaa za wanaume kuwa na tatizo la nguvu za kiume kama vile matatizo ya kisaikolojia, kuwahi kujichua, baadhi ya matatizo ya magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya zinaa, unene wa kupita kiasi, umri mkubwa, ulevi, kuacha mazoezi na ulaji usiofaa.

Kimsingi ziko tiba za mchanganyiko wa vyakula, lakini pia ili kuondoa tatizo wakati unaendelea na tiba kama ambavyo nimewahi kuzitaja katika matoleo kadhaa yaliyopita, unapaswa kufanya mazoezi na kula vyakula, vinywaji vyenye nguvu ili kujipa nguvu zaidi.

Pia kama mwanaume ameishi na mwanawake kwa muda mrefu na amekuwa na desturi ya kufanya mepenzi mara kwa mara katika mazingira yale yale anaweza kukumbwa na kasoro hiyo.

Dismas Lyassa ni mtaalam wa uhusiano aliyesajiliwa na serikali (Social Welfare Counselor), kwa msaada zaidi wasiliana naye, 0653777700, http://dismaslyassa.com

chanzo: Njia za kulimaliza tatizo la upungufu wa nguvu za kiume
 
Mada ni nzuri inatia moyo kwa wanao amini kwamba hata ushauri ni sehemu ya tiba.
 
Asante kwa mada.

Matatizo ya Nguvu za Kiume yanasababishwa na mazingira ya sasa tunayoishi.

(i) Aina ya vyakula tunavyokula

(ii) Msongo wa mawazo kutokana na ugumu wa maisha.

(iii) Magonjwa

Sasa hivi tunakula vyakula vya viwandani. Vyakula vya viwandani vimepitia njia mbali mbali hadi kufikia mlaji. Pia kuna chemicali zakuhifadhi.

Katika mlolongo wote huo lazima chakula kinakuwa sio chenyewe, tayari chemicali zinaingia.

Chemicall ndo sumu zinaenda kukusanyika katika mwili wa binadamu hasa kwenye mifupa (ambapo kuna vacuum). Kumbuka kuwa mifupa ina born marrow ambazo ni muhimu kama hifadhi ya nguvu za kiume na pia ndipo white blood cells (kinga za mwili zinatengenezwa na kuhifadhiwa.

Sasa hizi sumu zinaenda kukusanyika pale kwenye born marrow, na unapotumia nguvu katika shughuli. born marrow inatumika na nafasi inapopatikana tu sumu zinaenda kule. Kwa hiyo ukila chakula, born marrow hazipati nafasi ya kukua.

Kumbuka kwenye testicals (yaani Ma pu .mbu) ambazo mbegu zinatengenezwa, mali ghafi hutoka katika born marrow.

MSAADA. NI KUONDOA SUMU TU MWILINI KWA KUTUMIA VIRUTUBISHO NA MAZOEZI HADI KUTOKWA NA JASHO. VIRUTUBISHO NI KAMA ALOE VERA KUTOKA FOREVER LIVING. KWA MAZOEZI MAANA YAKE, JASHO LINATOKA PAMOJA NA HIZO SUMU. SASA LAZIMA HIZO SUMU ZIPATE MSUKUMO WA KUZITOA NJE.

Mtu akitumia dawa za hosp kwa ajili ya matibabu kuna baadhi ya mabaki ya dawa yanabaki mwilini. na hiyo ni madhara.
 
Kwa hiyo ili kukabiliana na tatizo, ni kunywa virutubisho vya kuondoa sumu mwilini kama Aloe Vera kutoka Forever Living na virutubisho vya kurudisha nguvu.
 

itakuwa vizuri sana kama unatuambia kabisa jina la hicho chakula cha kiwandani chenye sumu na ni sumu zipi zilizomo humo, maana vyakula tu vya viwandani iko general sana, hata aloe vera inakuwa processed kiwandani!!!.
 
Asante Paulo kwa changamoto(challenge) Sio vyakula vyote, hatujui mazingira gani vyakula vinatengenezwa. Na sumu sio lazima iwe nyingi kiasi ambacho utapata madhara kwa muda mfupi.

It is just traces of chemicals which are might be used in some packaged foods.

Kwa aloe vera haiongezwi kitu na yenyewe ni against any poison, sasa sumu itaweza kukaa katika aloe vera??

Jaribu kusoma Biochemistry ya aloe vera Bardensis miller kwanza, ndo utaprove. Just google it.

Wewe unafikiri kwa nini watu wanapata upungufu wa nguvu za kiume nyakati hizi tofauti na zamani ambapo baba zetu na babu zetu?
 

Sasa mkuu mbona watu wengi siku hizi hapa mjini wanaona ni big deal kwenda kununua groceries Shoprite na grocery stores nyingine. sisi tunaonunua groceries masokoni mitaani tunaambiwa washamba! Organic food ndio yenyewe. Haya majunk ya stores yatatumaliza
 
Ndugu zangu wana JF ninayofuraha kuwashirikisha kuhusu mada hapo juu. Nilikuwa nasumbuliwa sana na nguvu za kiume kwa takribani miaka miwili, nilikuwa natumia dawa za kienyeji( miti shamba) nikiamini nitapona lakini zikawa zinanisaidia kwa muda tu na tatizo likawa liko palepale. Niliamua kwenda hosptali na kumweleza Dr juu ya tatizo langu, Dr alinipima na kunikuta niko fiti akanambia ni tatizo la kisaikolojia akanipa kidonge kimoja cha Viagra na akanambia nitumie siku tutakapofanya mapenzi na mpenzi wangu, akanambia nikitumie saa moja kabla ya tendo. Nilifanya kama Dr alivyonishauri, lakini kusema kweli kidonge kile hakikusaidia isipokuwa kilinikosesha raha kabisa maana siku hiyo uume haukusimama kabisa.

Nikabadirisha Dr, huyu Dr alinifanyia Ultra sound sehemu za viungo vya uume na aligundua kuwa kuna sehemu kwenye shina la uume kumevimba na alisema hii mara nyingine hutokea na kuwa hahisababishwi na kituchochote , aliniandikia dawa, nilimaliza doze week mbili zilizo pita na sasa niko fiti hadi shemeji yenu anafikiri natumia dawa, wakati hapo awali nilikuwa one minute nacheka.

Nimeamua kuandika hivi ili kuwashauri wanaume wenzangu wanaosumbuliwa na nguvu za kiume, wasikimbilie mitishamba wawaone wataalamu, waweza kuwa na tatizo dogo sana.

kila la heri ndugu zangu.
 
ungetoa ushauri ama reference dawa inapatikana wapi ili watu waweze kufuatilia
 
we tutajie aina ya dawa na dozi yake..si wengine kujieleza kwa hawa maDr tumechoka!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…