Salaam,
dar es salaam siku za karibuni umeibuka mtindo mpya wa kunadi biashara kwa njia ya matangazo ya kwenye vitambaa.
Ukipita mitaa kadhaa utakutana na mabango yameandikwa 'dawa ya nguvu za kiume muone dr manyuki', manyigu na waganga wengine wengi.
Pia wapo wamaasai ambao wanapita bar na kuwauzia watu hizo dawa za kuongeza nguvu za kiume na kurefusha uume.
Je nini madhara ya hizo dawa ambazo hazijapimwa na wala hazijatafitiwa??
Kwa nini wote wanao jitangaza kwenye magazeti, kwenye mabango na wanaouza mitaani hayao madawa wasikamatwe kwa kuhatarisha afya za watu??
Kwa mtazamo wangu watu wengi hawana matatizo yanayohitaji dawa za kuongeza nguvu, cha zaidi wapatiwe ushauri wa kisaikolojia, waelekezwe namna ya kula chakula bora na kuzingatia mazoezi.
Ikishindikana ndipo daktari aandike dawa, lakini si hawa waganga waanze kuwashawishi watu wanunu hayo ma mikuyati