Upungufu wa nguvu za kiume ni tatzo linalohusisha sehemu za maumbile ya kiume ya mwanaume kushindwa kufanya kazi zake kama inavyotakiwa.
Mara nyingi tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hutokea pale mzunguko wa damu unakua dhaifu hasa maeneo ya maumbile ya kiume hivyo kufanya maumbile hayo kusinyaa na kushindwa kukidhi haja za mwenza.
Kwa miaka ya hivi karibuni kumekua na ongezeko kubwa sana la wanaume wengi kupata tatizo hili, na hii natokana na mfumo mbovu wa maisha hasa katika vyakula tunavyokula, japo kuna baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza yanaweza kusababisha tatzo hili lakini leo tuzungumzie kuhusiana na swala la vyakula tu.
HIVI NDIVYO VYAKULA VITANO VYENYE UWEZO MKUBWA WA KUPAMBANA NA MATATIZO YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
1.TIKITI MAJI
tikiti maji lina virutubishi vingi ikiwemo lycopene, vitamin C na beta-carotene ambazo zina kazi kubwa katika kufanya mishipa ya damu irelax na kutanuka vizuri (vaso dilation) ili damu ipite vizuri sana katika mishipa hivyo mzunguko wa damu ukiwa vizuri katika mishipa ya damu itaruhusu maumbile ya kiume kuwa na nguvu ya kufanya kazi yake kama inavyotakiwa.
Sehemu ya muhimu zaidi kwenye tikiti maji ni ile sehemu nyeupe iliyo chini ya ile nyama nyama nyekundu hivyo kwa mwanaume unashauriwa kula kwa wingi zaidi hiyo sehemu.
2.NYANYA
kwenye matunda mengi yenye rangi nyekundu kuna kiwango kikubwa kirutubishi kinachoitwa LYCOPENE hasa hufanya mishipa iwe imara, irelax na kufanya kazi vizuri zaidi na kutokana na maumbile ya kiume kuzungukwa na mishipa ya damu ya kutosha hivyo itafanya kazi vizuri kama inavyotakiwa.
3.PARACHICHI
parachichi lina kiwango kikubwa sana cha madini ya potassium, vitamin K na vitamin B, virutubisho hivyo katika parachichi ambazo husaidia kuongeza homoni ya kiume inayoitwa TESTOSTERONE ambayo inazalisha mbegu za uzazi kwa mwanaume, inaipa nguvu misuli na uzito. hivyo ulaji wa mara kwa mara wa parachichi unamfanya mwanaume awe na afya kamili ya kiume
4.MBEGU ZA MABOGA
mbegu za maboga zina wingi wa vitamin B, C, D E na K, poa mbegu za maboga zina madini ya calcium, niacin, phosphorus, potassium na Zinc ambayo huzalisha kwa wingi homoni ya testosterone ambayo inazalisha mbegu za uzazi za mwanaume.
Ulaji wa robo kikomne cha mbegu za maboga kila siku kutafanya mwanaume aondokane na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
5.MCHICHA
mchicha una kiwango kikubwa sana cha vitamin B9 au folic acid, ambayo inaimarisha mzunguko wa damu pia inatengeneza seli nyekundu za damu. hivyo hufanya mwili uwe na uchangamfu. Kwa utafiti uliofanywa na NATIONAL INSTITUTE OF HEALTH mwaka 2014 ulionesha kuwa asilimia kubwa ya wanaume wenye upungufu wa nguvu za kiume walikua pia na upungufu wa vitamin B9 na utafiti mwingine wa NATIONAL OF HEALTH mwaka 2020 ulionesha wanaume 50 waliopatiwa falic acid walipata walipata nafuu kutoka kwenye tatizo lao la upungufu wa nguvu za kiume.
ulaji wa mara kwa mara wa mchicha ni mzuri sana kwa wmwanaume.
Pia kuna vyakula vingi sana ambavyo husaidia mwanaume kuepukana na tatizo hilo kama vile karoti, kahawa, matufaa, karanga n.k