Tatizo la vijana waliosomea mafuta na gesi kuzagaa mtaani wakati kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa na Serikali

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Nimeona hili leo niliseme pengine viongozi wetu hawalifahamu swala hili:

Kweli kumekua na tatizo la vijana wetu waliosomea fani za mafuta na gesi kuzagaa mtaani tangu fani hizi zilipo anzishwa mwaka 2013. Asilimia 80 ya vijana waliosomea fani hizo hawaja ajiriwa mpaka sasa. Na walianza kuhitimu mwaka 2016.

Vijana wanahitimu lakini nafasi za kazi zinazotoka haziendani na idadi ya wahitimu.

Kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa lakini vijana hawa wa mafuta na gesi hawapati nafasi ya kwenye miradi hiyo.

Makampuni yetu ya serikali yakitangaza nafasi, zinazowahusu vijana wa mafuta na gesi zinakua ni chache sana hata kumi hazifiki.

Vijana wanazidi kuzeeka mtaani hawana pakujishikiza.

Viongozi wetu wanapaswa kuwatazama hawa vijana wa mafuta na gesi. Wengi wanajikatia tamaa kabisa hasa wanaposikia miradi inatangazwa kila siku ila ajira zinazotolewa na hiyo miradi hazihusu fani za mafuta na gesi.

Jamani jamani ni kweli keki ya mafuta na gesi ni tamu kiasi kwamba watu hupenda kung'ang'aniana lakini tunapaswa kuwapa ajira zao vijana hawa. Ajira zipo kote sekta binafsi na serikalini ila vijana hawa wanatengwa.

Serikali ingefanya jambo katika swala hili.

Mpaka nikawa najiuliza maswali ni kitu gani kinashindikana kuwaajiri vijana hawa. Walau ajira zilingane na idadi ya wanao hitimu kwasababu miradi tunaiskia kila siku.

Tuna mradi wa Helium. Na mingine mingi tu ya gesi na mafuta. Hivi ni kitu gani kinashindikana kuwakusanya hawa vijana wote wa mafuta na gesi na kuwatupia kwenye hiyo miradi.

Lakini wakati mwingine ikionekana fani zimeshakua na idadi kubwa ya wahitimu, pia ni jambo jema kuzibadilisha fani hizo ili ziendane na soko la ajira.

Hii ni orodha ya makampuni ambayo vijana wa mafuta na gesi wana nafasi ya kuajiriwa hapa Tanzania.
  • Shell Tanzania
  • Total Tanzania Ltd
  • East African Crude Oil Pipeline (EACOP) project In Tanzania
  • Swala Oil and Gas Tanzania Plc
  • Statoil Tanzania Limited
  • Ndovu Resources Ltd/Aminex Plc
  • CAROIL(T) limited
  • Equinor Tanzania
  • Songas Limited
  • Dodsal Resources & Mining Itingi (Tanzania) Pvt. Ltd
  • Maurel exploration Production Tanzania Limited
  • Artumas Energy Ltd. (Wentworth Resources Limited)
  • Lake Oil Ltd.
  • Pan African Energy Tanzania Ltd
  • Heritage Oil Tanzania Ltd
  • Tanzania Petroleum Development Corporation
  • Orca Exploration Group Inc.
  • Petrofuel
  • Barkat Gas
  • Oilcom (T) Limited Terminal
  • Swala Oil and Gas (Tanzania) PLC (SOGTP)
  • State Oil
  • Halliburton
  • Aminex PLC
  • Oryx Energies
  • Lake Group
  • PUMA
  • MOGAS
  • VIVO Energies
  • TPDC
  • EWURA
  • TBS
  • PURA
  • OIL COM
  • N.K
Ahsante sana
 
Vijana wewe na extra soft skills za kuwasaidia endapo changamoto za ajira zinapotokea.ni fikra potofu kusoma ili kuajiriwa ni lazima vijana watafute njia mbadala endapo wakikosa ajira mfano ujasiliamali, uandishi sanaa kilimo nk
Tunachozungumzia ni ukubwa wa miradi iliyopo kwenye sekta ya mafuta na gesi. Na idadi ya ajira zinazotoka. Ukiangalia sekta ya mafuta na gesi ndio sekta yenye miradi mikubwa kote duniani.
 
Mimi nashauri wajiunge na UVCCM ili wapate soft skills za kujikomba kwa wakubwa, kuvaa shati la Mbogamboga na kuhakikisha wapo online muda kuisifu serikali.

Kwasasa mtindo wa vimemo umerudi kwa kasi.

Wafanye hivyo watanishukuru baadaye, wafuate nyayo za yule Kijana wa UVCCM aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu TPDC na kutenguliwa muda mchache baadaye!
 
Nina mdogo wangu amemaliza mwaka huu shahada hii ya petroleum engineering pengine hii mada inanihusu sana. Ni miongoni mwa wale vijana bright kabisa division 1 point 4 form six aliyechaguliwa kusoma shahada hii selective pale mlimani.

Tunajenga nchi moja ya kijinga sana kuwaacha vijana wetu bora kabisa kusota mtaani. Nafikiri kama mzazi inabidi kumwandaa kijana wako kutopoteza muda na degree za wanasiasa bali mfundishe mapema stadi za maisha ikiwemo kilimo, biashara na ufundi mbalimbali.
 
Mtoto wa masikini Anabidi kusoma fani tatu tu
Udaktari
Ualimu
Kilimo

Kila siku nawaambia lakini mnashupaza shingo
Hapo kwenye ualimu nako changamoto kwa sasa, inategemea ualimu kasomea nini, labda masomo ya sayansi
 
Nitoshe kusema ewe kijana ambaye hujaenda chuo.....kabla ya kuapply fani fanya uchunguzi kwanza sio unaapply kwa kufuata mkondo.....!! Fani nzur kwa sasa ni
1) Ualimu wa awali shule ya msingi

Naweza sema hii ndio top inayohit kwa sasa mana serikal inawahitaji hawa kila shule na ni koz iliyoanzishwa mwaka juz watu wanakula ajila kaz yako kucheza na watoto wa chekechea mpunga unaingia hafu hauna daftar za kusahihisha. Pia waweza kujiajil kwa kuanzisha day care center ambazo kwa sasa zinalipa kutokana na watu kutokuwa na muda wa kuwalea watoto wao

2) Fani za kompyuta(all field)
Now tunaenda ulimwengu wa kidgtal tunahitaji wataaalamu weng wa kompyuta na hata serikal inampango wa kuanzisha koz za kompyuta kuanzia shule za msing na sekondar na uzuri vtabu vya ICT vimeshapokelewa na mashule wanaosubiriwa wataalamu. Hii pia unajiajil kama web developer na hata kutengeneza app janja kwa ajil ya kukuongezea kipato!

All in all aliyesomea field inayohusiana na kompyuta hafu akalalamika amekosa ajila ntamshangaa sana...!

3) Mechanical engineering(field zote). Nayo iko poa mana waweza kujiajil na kupata kipato! Watu wanazid kununua magar basi nawale wanaotengeneza wanatakiwa sana na hii kaz inaapply kwenye viwanda vyote unavyovjua lazma mechanical engineer wapo!

NB
Kama nngepata muda wa kuchagua now nngesoma mojawapo ya hizi kozi hasa compyuta
 
Kwa sasa haihitaji kuwa bright kusomea hizi kozi mtu anamaliza zake form 4 anaenda kusomea oil and gas pipeworks diploma hapo anakuwa sponsored na serikali anamaliza anaenda kuchukua uzoefu kwa cheti chake cha diploma .

Anamaliza anaenda kitafuta degree akiwa na kazi tayari KIKUBWA KWA SASA WANAOKOSA AJIRA NI WALE WALIOPOITA DIRECT YAANI FORM 6 KISHA WAKAENDA KUCHUKUA DEGREE sasa wakirudi kitaa ajira zinatoka ni DIPLOMA NA VETA ila pole sana mkuu atapata tu aangalie ishu nyengine .
 
Hapo kwenye ualimu nako changamoto kwa sasa, inategemea ualimu kasomea nini, labda masomo ya sayansi
Tuchangie mada inavyotaka jamani. Mada inazungumzia ukubwa wa miradi yenyewe. Swali la kujiuliza kwenye hiyo miradi wakina nani wanakaa. Ndio mada ilenge hapo.
 
Udaktari
Ualimu
Kilimo

Yaani hizo ndo fani sahihi dunia nzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…