Mahotera
JF-Expert Member
- Mar 20, 2014
- 729
- 1,847
Koran
5;51. Enyi mlio amini!(waislamu) Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki...... 9;23. Enyi mlio amini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa vipenzi vyenu ikiwa wanastahabu ukafiri kuliko Imani....
Asante.
Ila kila mtu anahitaji kufahamu lugha ya kiarabu kidogo ili aweze kuielewa Quran. At least uweze kutumia tu kamusi au Google translator...
Kiswahili kina upungufu wa maneno ya kuitafsiri lugha ya kiarabu. Hivyo wanaoandika tafsiri hawawezi kuwasilisha maana halisi, you need an original text. Ila nitajitahidi kurahisisisha hapa:
Rafiki ni
صَدِيق، صَاحِب، رَفِيق، خَلِيل، نَصِير، مُعَاشِر، خدين، جَليس au
Aya ulizo nukuu zinataja أَوْلياء neno linalomaanisha watunza siri, au wandani, au walinzi (guardians), au wasimamizi wa mambo (patron), au watu wanaotegemewa (supporters).
یَـٰۤأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوۤا۟ ءَابَاۤءَكُمۡ وَإِخۡوَ ٰنَكُمۡ أَوۡلِیَاۤءَ إِنِ ٱسۡتَحَبُّوا۟ ٱلۡكُفۡرَ عَلَى ٱلۡإِیمَـٰنِۚ وَمَن یَتَوَلَّهُم مِّنكُمۡ فَأُو۟لَـٰۤىِٕكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ
[Surah At-Tawbah: 23]
یَـٰۤأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ ٱلۡیَهُودَ وَٱلنَّصَـٰرَىٰۤ أَوۡلِیَاۤءَۘ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِیَاۤءُ بَعۡضࣲۚ وَمَن یَتَوَلَّهُم مِّنكُمۡ فَإِنَّهُۥ مِنۡهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا یَهۡدِی ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِینَ
[Surah Al-Māʾidah: 51]
Sehemu nyengine wameitwa بِطانَة
یَـٰۤأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ بِطَانَةࣰ مِّن دُونِكُمۡ لَا یَأۡلُونَكُمۡ خَبَالࣰا وَدُّوا۟ مَا عَنِتُّمۡ قَدۡ بَدَتِ ٱلۡبَغۡضَاۤءُ مِنۡ أَفۡوَ ٰهِهِمۡ وَمَا تُخۡفِی صُدُورُهُمۡ أَكۡبَرُۚ قَدۡ بَیَّنَّا لَكُمُ ٱلۡـَٔایَـٰتِۖ إِن كُنتُمۡ تَعۡقِلُونَ
[3: 118]
Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwishakuwa wazi chuki yao katika midomo yao. Na yanayo fichwa vifuani mwao ni makubwa zaidi. Tumekubainishieni ishara ikiwa nyinyi mutazingatia.
Hizi zinakataza kutoa siri za waislamu kuzipeleka kwa wasiokua waislamu hata kama ni watu wa karibu, hazikatazi urafiki.
Ukitaka kuelewa zaidi angalia pia aya hizi:
لَّا یَنۡهَىٰكُمُ ٱللَّهُ عَنِ ٱلَّذِینَ لَمۡ یُقَـٰتِلُوكُمۡ فِی ٱلدِّینِ وَلَمۡ یُخۡرِجُوكُم مِّن دِیَـٰرِكُمۡ أَن تَبَرُّوهُمۡ وَتُقۡسِطُوۤا۟ إِلَیۡهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ یُحِبُّ ٱلۡمُقۡسِطِینَ (8) إِنَّمَا یَنۡهَىٰكُمُ ٱللَّهُ عَنِ ٱلَّذِینَ قَـٰتَلُوكُمۡ فِی ٱلدِّینِ وَأَخۡرَجُوكُم مِّن دِیَـٰرِكُمۡ وَظَـٰهَرُوا۟ عَلَىٰۤ إِخۡرَاجِكُمۡ أَن تَوَلَّوۡهُمۡۚ وَمَن یَتَوَلَّهُمۡ فَأُو۟لَـٰۤىِٕكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ (9)
[Surah Al-Mumtaḥanah: 8-9]
Allah hakukatazeni kwa wale ambao hawakupigeni vita kwa ajili ya dini, wala hawajakufukuzeni katika miji yenu, kuwafanyia wema na uadilifu. Hakika Allah anapenda uadilifu. Isipokua Allah anakukatazeni kuwafanya WANDANI wenu wale ambao wanakupigeni vita kwa ajili ya dini, au wanawasaidia wengine kukutoeni katika miji yenu. Na yeyote atakae wafanya hao kuwa wandani wake, basi hao ndio madhalimu.
Kwa hivyo, uislamu haukatazi rafiki mkristo wala myahudi, ila unakataza kuvujisha siri na mipango. Na hilo ni uhaini na usaliti katika jamii au taasisi yoyote ile, uislamu sio exception. [60:8-9].