Tatizo la Waraka wa shehe Ponda ni zile takwimu hazina uhakika na ni kinyume na sheria

Tatizo la Waraka wa shehe Ponda ni zile takwimu hazina uhakika na ni kinyume na sheria

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Sheria ya takwimu ina kipengele kimoja kimekaa kimtego sana.

Kwamba takwimu unazozitoa kwa umma uwe umezipata kwa chanzo kinachoaminika chenye uhalali wa kutoa takwimu hizo kwa mujibu wa sheria.

Sasa kusema uwiano wa uteuzi ni 80% kwa 20% kwa dini zilizopo.....hii ina utata.
Kwanza Tanzania hakuna dini mbili pekee.

Niishie hapo.

Pia soma >
Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akamatwa na Polisi

Maendeleo hayana vyama!
 
Wana CCM kila atakae ongea "UKWELI" lazima apingwe. Tumewazoea.

Turudi kwenye "HOJA KUU" ya swala la "KUTENDA HAKI", dini zote zinalitilia mkazo hili swala. Na hata mungu amewaonya vikali na amewa ahidi kuwapa adhabu kali sana wale wote wanao "PINDISHA/KUNYIMA/KUDHULUMU/KUPUNJA" haki.

Hata kama utadhulumu "PIPI MOJA" katika kontena zima la 40FT basi jiandae na adhabu kali sana kwa mola wako.

Kuomba "TUME HURU" ni kwasababu "HAKI ITENDEKE". Sio swala la kichama hilo.
 
Kwani ametaja dini gani?..kama 80% ni hindu na 20% zilizobaki ni dini nyengine.
Bado huna hoja.njoo kivingine.
 
Sheria ya takwimu ina kipengele kimoja kimekaa kimtego sana.

Kwamba takwimu unazozitoa kwa umma uwe umezipata kwa chanzo kinachoaminika chenye uhalali wa kutoa takwimu hizo kwa mujibu wa sheria.

Sasa kusema uwiano wa uteuzi ni 80% kwa 20% kwa dini zilizopo.....hii ina utata.
Kwanza Tanzania hakuna dini mbili pekee.

Niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama!
Hii nchi kwa sasa inakoelekea ni kwenye "full dictatorship"

Hivi nyinyi maccm, mnashindwa nini kujibu hoja kwa hoja, badala yake mnalitegemea Jeshi la Polisi, litumie mabavu katika kuwajibia hoja za kisiasa?
 
Hii nchi kwa sasa inakoelekea ni kwenye "full dictatorship"

Hivi nyinyi maccm, mnashindwa nini kujibu hoja kwa hoja, badala yake mnalitegemea Jeshi la Polisi, litumie mabavu katika kujibu hoja za kisiasa?
Halafu hao polisi wanakukamata bila sababu ukifika kituoni ndio wanafikilia kosa la kukupa...
 
Ukweli hauhitaji sheria yoyote kusimama pahala pake.

Udini haufai, nchi hii ni yetu sote, tunahitaji kuwa fair kwa makundi yote ya kijamii.

80% kwa 20% ni too much, haijakaa sawasawa hata kidogo

Waislamu majority wanaunga mkono waraka
Bwashee serikali haina dini!
 
Hii nchi kwa sasa inakoelekea ni kwenye "full dictatorship"

Hivi nyinyi maccm, mnashindwa nini kujibu hoja kwa hoja, badala yake mnalitegemea Jeshi la Polisi, litumie mabavu katika kujibu hoja za kisiasa?
Yaani tuache kuwaza namna ya kuendelea kujenga uchumi wa kati tuanze kuumiza kichwa kwa hoja za hovyo hovyo kama hizi?
 
Ponda....? Sasa mbona hapa kuna wafipa wengi? Hivi nyie wafipa viiipi..! hoja mmekosa atakayejitokeza tu...kulaumu hata kama sio wa kwenu mnaanza kupiga mbinja..sasa huu ndo ule mwaka ruzuku inaenda kukata..!
 
Halafu hao polisi wanakukamata bila sababu ukifika kituoni ndio wanafikilia kosa la kukupa...

Wao polisi huwa wanatumwa wakukamate, kisha wanaambiwa wakupe kosa gani. Polisi wao huwa wanaenda kama robots, lakini wenye mashitaka ni viongozi wa ccm. Hivyo polisi wanasubiri wapewe muongozo, kisha ndio waandike kosa kutokana na watoa maagizo.
 
Ukweli hauhitaji sheria yoyote kusimama pahala pake.

Udini haufai, nchi hii ni yetu sote, tunahitaji kuwa fair kwa makundi yote ya kijamii.

80% kwa 20% ni too much, haijakaa sawasawa hata kidogo

Waislamu majority wanaunga mkono waraka
Hao majority ni akina nani? Dr Hussein Mwinyi yupo? Mama Samia? Selemani Jaffo? Hamisi Kigwangala? Kassim Majaliwa? Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma? Dr Bashiru Ally? Mufti Abubakar Zubeir? Sheikh Alhadi? BAKWATA yote? Akina nani?
Mwenyekiti wa Shura ameukana waraka.
Tuepukane na generalized sweeping statements kama hizo.
 
Ponda....? Sasa mbona hapa kuna wafipa wengi? Hivi nyie wafipa viiipi..! hoja mmekosa atakayejitokeza tu...kulaumu hata kama sio wa kwenu mnaanza kupiga mbinja..sasa huu ndo ule mwaka ruzuku inaenda kukata..!

Ccm ndio inategemea ruzuku maana haijawahi kuishi nje ya mbeleko ya serikali, toka enzi za mfumo wa chama kimoja. Wapinzani wengi wanajivunia kukubalika na umma kuliko ruzuku.
 
Back
Top Bottom