Tatizo la Waraka wa shehe Ponda ni zile takwimu hazina uhakika na ni kinyume na sheria

Tatizo la Waraka wa shehe Ponda ni zile takwimu hazina uhakika na ni kinyume na sheria

Sheria za Nchi zipi? Huyo dikteta anafuata sheria za Nchi? Kuanzia lini? 😳😳😳

Ponda atapondwa asipofuata sheria za nchi vizuri.
 
Wana CCM kila atakae ongea "UKWELI" lazima apingwe. Tumewazoea.

Turudi kwenye "HOJA KUU" ya swala la "KUTENDA HAKI", dini zote zinalitilia mkazo hili swala. Na hata mungu awawaonya vikali na amewa ahidi kuwapa adhabu kali sana wale wote wanao wanao "PINDISHA/KUNYIMA/KUDHULUMU" haki.

Hata kama utadhulumu "PIPI MOJA" katika kontena zima la 40FT basi jiandae na adhabu kali sana kwa mola wako.

Kuomba "TUME HURU" ni kwasababu "HAKI ITENDEKE". Sio swala la kichama hilo.
Kiongozi wa dini ana haki ya kukemea maovu ktk jamii na kutoa mwongozo kulingana na maagizo ya mwenyezi Mungu.
Mbona viongozi wa kikatoliki wanapotenda makosa hawakamatwi?
 
Sheria ya takwimu ina kipengele kimoja kimekaa kimtego sana.

Kwamba takwimu unazozitoa kwa umma uwe umezipata kwa chanzo kinachoaminika chenye uhalali wa kutoa takwimu hizo kwa mujibu wa sheria.

Sasa kusema uwiano wa uteuzi ni 80% kwa 20% kwa dini zilizopo.....hii ina utata.
Kwanza Tanzania hakuna dini mbili pekee.

Niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama!
John...
Usitoe hukumu subiri kwanza hapana haja ya haraka.

Tusubiri mahakama.

Ikibidi Waislam tutaomba takwimu serikalini.
 
Ndio maana polisi wako naye ili athibitishe takwimu zake!

Ukweli wake hauhitaji kudhibitishwa na polisi maana uko wazi. Wanachofanya hao polisi ni yale yale yanayofanywa kwenye nchi zote za utawala kwa mabavu. Hata mitume wa kweli waliuwawa na watawala kutokana na ukweli wao. Hayo ni marudio tu, lakini ukweli wenyewe tumeujua. CUF nao waliunga mkono huo waraka, ngoja tuone kama mchepuko wenu nao mtaukamata.
 
John...
Ikiwa wafuasi wa dini moja ndio waliojaza nafasi nyingi kupita kiasi vipi serikali iwe haina dini?
Watu ndio wana dini lakini serikali haina dini ndio maana Zanzibar hakuna zamu bali walio wengi ndio wanaoongoza miaka yote!
 
Sheikh Ponda ni tatizo he needs to be put in his place na ni mropokaji ata hoja zake ni ovyo katiba gani inaandikwa kwa miezi mitatu kabla ya uchaguzi au anadhani katiba inaandikwa kama waraka.

Ni mchochezi wa muda mrefu anaestahili kuhojiwa for sedition crimes lakini serikali lazima iwe constitence kwenye kusimamia sheria; that is what the law demands uwezi kumkamata Sheikh Ponda peke yake wakati Gwajima is ignored for the crimes. Hapo ndio tatizo lilipo kwa watu wengine.

Katiba pendekezwa ipo, na ilikuwa kwenye hatua za kupigiwa kura, na ndani yake kuna muundo wa tume huru ya uchaguzi, lakini rais huyu aliikataa kwa sababu zake binafsi. Hivyo tafuta utetezi mwingine. Na kama serikali ikisimamia sheria kwa mantiki ya sheria, wengi sana wataenda jela ikiwemo viongozi wa serikali. Lakini serikali imejikita zaidi kwenye kukomoa wasioisujudia na wasema kweli.
 
Apigwe tu hizi chokochoko za ponda zilikuwa zimepoa baada ya kumsweka ndani. Teuzi haIfuati dini bali watanzania wenye uwezo na sifa za kuchapa kazi

Wakristo tu ndio wenye uwezo wa kufanya kazi? Ukweli huwa una nguvu sana. Mnaweza kumsweka ndani msemakweli, lakini hamuwezi kuusweka ndani ukweli wake.
 
Sheria ya takwimu ina kipengele kimoja kimekaa kimtego sana.

Kwamba takwimu unazozitoa kwa umma uwe umezipata kwa chanzo kinachoaminika chenye uhalali wa kutoa takwimu hizo kwa mujibu wa sheria.

Sasa kusema uwiano wa uteuzi ni 80% kwa 20% kwa dini zilizopo.....hii ina utata.
Kwanza Tanzania hakuna dini mbili pekee.

Niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama!
Ubaya n kuwa wenzie wameukana waraka sasa
Ponda bhana
 
Watu ndio wana dini lakini serikali haina dini ndio maana Zanzibar hakuna zamu bali walio wengi ndio wanaoongoza miaka yote!

Kwahiyo huku Tanganyika wakristo ndio wengi? Naona unazidi kujichanganya.
 
Serikali ilikataa kuweka kipengele cha dini ya mtu kwenye sensa, waislamu walikitaka, Wakiristo wakasema hapana kisiwemo kwa madai kuwa haina maana kujua dini ya mtu na kwamba serikali haina dini. Ni dhahiri hilo lingewekwa wazi ni dhahiri serikali ingewekwa kikaangoni kujibu mambo mengi ya waislamu, ikiwemo why wako underepresented katika ajira na teuzi wakati wako asilimia kadha wa kadha nchini?

Lakini cha ajabu serikali hiyohiyo inayojifanya haichukui takwimu za dini za Watu kwenye sensa inafanya kinyume chake kwenye huduma nyingine za msingi, kwa mfano ukifungua faili la Kliniki, utaulizwa dini yako, Ukienda polisi utaulizwa dini yako na sehemu nyinginezo. Kwa hiyo serikali inachukua taarifa za dini za watu, lakini kwenye sensa inajifanya haitaki kuzichukua, Je kwenye sensa setikali inakataa kuchukua taarifa za dini za watu ili kufichaficha madudu kama haya ya 80% by 20% kwenye teuzi?
 
Ubaya n kuwa wenzie wameukana waraka sasa
Ponda bhana

Wenzie lazima waukane huo waraka kwa ajili ya usalama wao, lakini ukweli ulio ndani ya waraka haukaniki. Halafu ukweli hauhitaji kutetewa na watu wengi, maana ukweli huwa unajitetea wenyewe.
 
Ni simple, tembelea misiba, harusi, shughuli za kijamii zinazohusu waislamu, pindi wakijadili mustakbali wao katika nchi. Hawafurahishwi na namna teuzi zinavyofanywa. Hawafurahiswi na teuzi ambazo kila wakati wao ni kiduchu sana. wanahoji kuwa mbona haziakisi demography ya nchi, mbona inaonekana kundi moja liko over represented kuliko jingine, kwa nini?
Haya wanayazungumza wazi miongoni mwao bila kificho.
Alichokifanya Sheikh ni kukiweka public kwa wider audience tu
Nimeusoma na waraka pia. Nakiri ni kweli katika awamu hii kumekuwa na bias kubwa ya kijinsia, kikanda na hata kidini hasa katika teuzi za kazi za uongozi wa serikalini, na ninapenda niseme labda ni bias (probably unintended) kwa sababu wakati yote hayo yanaonekana sijapata kuona wala kusikia waathiriwa wakilalamika na badala yake nawaona wakiwa mstari wa mbele kumwaga sifa tuuu! Awamu zilizopita pia nilisikia malalamiko lakini nashangaa sana kwani awamu zilizopita hali hii ya 'bias' haikuwa mbaya hivi lakini malalamiko yalikuwa makubwa disproportionately.
Lakini niseme pia katika ule waraka kuna malalamiko mengine nadhani watu walishauriwa tu vibaya. Mfano ile kesi ya UDOM iliyozungumzwa, kwanini watu walalamikie kuondolewa watu wa qualifications ndogo na kuwekwa wa better qualifications (nimeona majina yaliyochukua nafasi ni professors na doctors, na waliotolewa ni chini ya hapo), hayo mbona ni maboresho ya kawaida? Ningesikitika kama system inafanya purging ya watu kwa udini na kuingiza watu wa inferior qualifications alimradi tu ni wa dini wanayotaka! Hilo la UDOM nitawaomba ndugu zagu waislam walitafakari tofauti.
Huko kwenye mambo ya teuzi na kwingineko, wacheni mambo ya kusifia tu badala yake leteni data (kuna sheria ya takwimu siku hizi, kuweni waangalifu), wekeni data mbele ya wanaohusika (siyo hapa mtandaoni, hapa njooni kuleta taarifa ya jitihada na matokeo), semeni waziwazi mbele ya anayetakiwa kuchukua hatua mnazotaka, msimwogope, mwenyewe anawaambia siku zote msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 
Hao uliowataja hawana maamuzi yoyote, wao ni walinda vyeo tu. Huyo mwenyekiti lazima aukane kwa ajili ya usalama wake. Kitu ambacho hawezi kukikana, ni ukweli ulio ndani ya huo waraka fullstop.
Kama na wewe nimuislamu basi waaislamu mna akili ndogo sana

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Hao uliowataja ni wachache sana katika asilimia nyingi za waislamu nchini.

Mwenyekiti wa shura kuukana waraka haufanyi waraka usiwe wa shura, kaukana yeye binafsi siyo shura iliyoukana.

Hata Petro alimkana Yesu mara tatu hii haimaanishi kuwa ni kweli alikuwa hamjui Yesu
Sasa kama hao ndio top yeye ponda alikuwa anataka uteuzi uweje? Au anataka zile sheria zao za kiislamu ziongoze nchi ndio ajue kuna usawa?

Alafu naona ni upumbavu mtupu kuanza kuwaza teuzi kidini karne hii

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom