Uchaguzi 2020 Tatizo lenu CHADEMA ni kuwa na mgombea Urais bila Wabunge

Uchaguzi 2020 Tatizo lenu CHADEMA ni kuwa na mgombea Urais bila Wabunge

MchunguZI

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,011
Reaction score
2,185
Lissu ana mapungufu yake tena mengi tu! Vivyo hivyo kwa Magufuli. Kampeni ni kutoa ahadi za matumaini. Kwa upande wa Magufuli ana nafasi nzuri kwa kuwa ni rahisi kuthibitisha utendaji wake kwa yale aliyokwishafanya. Kwa Lissu kazi ni kubwa zaidi maana uzuri wa ahadi hautoshi.

Wanasiasa wote hutoa ahadi nzuri, hata zile za Hashim Rungwe ni nzuri. Tatizo ni uthibitisho kwamba utaweza timiza ahadi hizo. Kwa maana nyingine lazima uwe mwangalifu kuchagua ahadi. Kwa wanaojua uchumi ukiahidi kupandisha mishahara mara mbili kwa kiwango cha sasa, iwe ndio njia ya kuwasaidia waajiriwa, najua tu huyo ni boya!

Kila mtu tumpe nafasi ya kushinda uchaguzi je, Baada ya Lissu kushinda wabunge anao? Sioni wanaoweza kuwa ndani ya Bunge la CHADEMA, siwaoni kabisa! CHADEMA mliijisahau kutafuta watu makini kushika nafasi za ubunge. Baadhi ya majimbo yanashilkiliwa na wenzenu na hawakutaka kushindanishwa, yaani ni majimbo yao. Hata kama Lissu hatashinda, ilistahili kuwa na kundi bora la wabunge. Kwa kifupi baada ya uchaguzi huu, ikitokea Lissu ameshindwa, huo ndio mwisho wa CHADEMA.
 
Ni kwa sababu bado ni mchana kwa huku kwetu Kigoma. Vinginevyo tungekuambia kojoa ulale huna hoja.

Magufuli anadhibitisha nini wakati kwa maisha ya mtanzania mmoja mmoja amefeli kabisa na nchi inaelekea kuwa kama Ethiopia ambako watu wa Marika yote wanakimbia nchi kwenda nje kutafuta maisha hata kwa kusafirishwa kama ng'ombe.
 
Haya niliyasikia kwa Lissu, lakini leo kapanda mwendokasi, 2015 Lowassa wa CHADEMA alipanda daladala.
 
Lissu hata yeye anajua fika hawezishinda, ndio maana anawaanda wanyanyembe wake mapema na zengwe la kuibiwa kura iwe ndo sababu ya msingi yeye kushindwa.
 
******** anatoa ahadi kwa imani yake kuwa yeye ndiye mmiliki wa raslimali zote za nchi hii.
Lissu ananadi sera ya kumilikisha wananchi mamlaka ya kuamua mustakabali wa rasilimali zao kwa uhuru.
Kuhusu wabunge tusubiri uamuzi ya sanduku la kura. Ila nimekuelewa kuwa Lissu ni rais anaye 2020.
 
Uongozi ni kama biashara, mfanyabiashara huwa haogopi kuanzisha biashara nyingine kama aliyonayo hailipi.
 
Poleni sana Wana Upinzani.

Hivi CHADEMA ikianguka tunahamia wapi??

Je, ACT au CHAUMA kwa Mzee wa ubwabwa??

Tuambiane Mapema kama taarifa za Awali za Muungano wetu[emoji23]
 
Hapa ndio unaona thinking yetu watanzania ilivyo narrow.

CHADEMA wameeleza kinagaubaga kwamba katika majimbo yote ya Tanzania bara walikuwa wameweka wagombea. Mwishowe baadhi yao wameenguliwa na tume kwa sababu wanazojua wenyewe.

Ningekuona kuwa mtu objective Kama ungeilamu tume kwa kuengua wagombea wa CHADEMA.

Kuna swala ambalo linanijia mara nyingi kichwani, hivi watanzania wanataka upinzani na hasa CHADEMA wafanye nini ndio wajue wako serious? Wapigane, wajikate mpaka damu au wakatambike?

Just put yourself in their shoes. Nionavyo Mimi Hawa ni watu wa kuhurumiwa Sana manake kufanya siasa ktk mazingira ya Africa Ni Jambo gumu. Kuna watu wasemee na kuwapongeza manake nadhani ungelikuwa wewe ndo una vibano hivyo, ulishakufa tayari.
 
Mkuu kwa miaka hii mitano tunayomalizia umeona bunge likiwa na umuhimu wowote wa kuwepo?

Bunge imebaki kuwa ni session ya kuwabadilisha watu maisha. Aliingia Hana utajiri anatoka na utajiri. Ifikie wakati Kama bunge litaendelea kuwa la mfumo wa hili lililopita Bora tuu Raisi aendelee kufanya anavyoona inampendeza kuliko kuwa na bunge la design ile.
 
Magufuli alisema upinzani hakuna, wewe unasema baada ya uchaguzi utakuwa mwisho wa upinzani, tumuelewe nani?
 
Mf
Uongozi ni Kama biashara mfanyabiashara huwa aogopi kuanzisha biashara nyingine kama aliyonayo hailipi
Mosi je kwa akili yako finyu umejuaje chadema haina wabunge makini ye kati ya hao 200+ Wanaogombea unawajua wote? Je hawana sifa zinazohitajika? Je mbona ccm walikuwa na wabunge 200+ ila maguful alichukuwa waliokuwa upinzani na kuwapa vyeo? Aliteua 10 na kuwapa uwaziri je lissu atashindwaje kwa hilo? Je hujui watanzania wengi hawana vyama?

Pili.... Magufuli alipoingia 2015 alikuwa na ushahid upi alioufanya? Kias wengine hawana?

Tatu... chama hakifi kirahisi hivyo, mbona mlisema toka 2015 cdm imekufa ila ndy inachanua? 2005 walikuwa na wabunge kidogo sana ila waliishi. ACT ina mbunge mmoja ipo tu mbona. Upinzani sio wabunge ni wananchi.
 
Angalia MPUUZI mwingine huyu aliyekuja hapa kujifanya naye ni Sheikh Yahya kutaka kutabiri kifo cha Chadema kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu!
 
Uko sahihi mleta mada ukiwa na wabunge nchi nzima kazi yao kubwa namba moja ni kunadi mgombea uraisi maaeneo yao Lisu pesa za wafadhili anakula peke yake harushii wenzie wagombea ubunge na udiwani Mpesa Tigo rusha nk kwa wagombea ubunge ili wamnadi anataka watumie gharama zao atasubiri sana anaenda sehemu chache wenzie wote waliowahi gombea walimwaga pesa sana kwa wagombea ubunge

Safari hii hata uwezekano wa Chadema kupata wabunge mdogo sababu madiwani wanatakiwa wamwagiwe pesa na wabunge ili wawanadi maeneo yao na kumnadi mgombea uraisi Chadema wamewatelekeza Lisu anakula mwenyewe pesa za wafadhili hagawii hata chama halafu anatarajia ushindi ni ndoto safari hii Chadema wagombea uraisi ubunge na udiwani watapigwa chini na CCM sio mchezo Lisu anadhani aweza pata kura nyingi bila kumwaga pesa za wafadhii kwa wagombea ubunge na udiwani ili wapate uwezo wa kumnadi na kujinadi
 
Ni kwa sababu bado ni mchana kwa huku kwetu Kigoma. Vinginevyo tungekuambia kojoa ulale huna hoja.
Magufuli anadhibitisha nini wakati kwa maisha ya mtanzania mmoja mmoja amefeli kabisa na nchi inaelekea kuwa kama Ethiopia ambako watu wa Marika yote wanakimbia nchi kwenda nje kutafuta maisha hata kwa kusafirishwa kama ng'ombe.
Ulitaka akupe mpaka pesa ya kuhonga?
Maisha magumu kwa sababu gani, hilo ni swali kwako, inatakiwa ukae chini utafakari kisha uanze upya ila kama hutaki na unajifanya ulizoea kunywa pombe za kutosha, usipoangalia utaolewa tu.
Hikini kipindi cha kujenga nchi timechoka na maisha ya kubahatisha miaka yote..
 
  • Thanks
Reactions: K M
Uko sahihi mleta mada ukiwa na wabunge nchi nzima kazi yao kubwa namba moja ni kunadi mgombea uraisi maaeneo yao Lisu pesa za wafadhili anakula peke yake harushii wenzie wagombea ubunge na udiwani Mpesa Tigo rusha nk kwa wagombea ubunge ili wamnadi anataka watumie gharama zao atasubiri sana anaenda sehemu chache wenzie wote waliowahi gombea walimwaga pesa sana kwa wagombea ubunge

Safari hii hata uwezekano wa Chadema kupata wabunge mdogo sababu madiwani wanatakiwa wamwagiwe pesa na wabunge ili wawanadi maeneo yao na kumnadi mgombea uraisi Chadema wamewatelekeza Lisu anakula mwenyewe pesa za wafadhili hagawii hata chama halafu anatarajia ushindi ni ndoto safari hii Chadema wagombea uraisi ubunge na udiwani watapigwa chini na CCM sio mchezo Lisu anadhani aweza pata kura nyingi bila kumwaga pesa za wafadhii kwa wagombea ubunge na udiwani ili wapate uwezo wa kumnadi na kujinadii
Cha ajabu hata huku Tabora, washenzi wamekwisha jua hela, yaani kampeni bila hela haiwezekani. Laa kuna njaa sana ya hela huku.
 
Magufuli alisema upinzani hakuna, wewe unasema baada ya uchaguzi utakuwa mwisho wa upinzani, tumuelewe nani?
Ukiangalia kuwepo kwa Lissu kama mgombea ni dalili za CHADEMA kukosa mgombea. Wabunge wako wapi kwenye majimbo?
 
Back
Top Bottom