New Designer
JF-Expert Member
- Aug 8, 2025
- 551
- 879
Habari,
Pagination ni nini ?
kitaalamu pagination ni zile buttons za next and prev hizi zinakuwezesha kuona comment zaidi zilizo hide mfano 1, 2, 3, 4, 5, 7 ambapo hapa jamiiforums zipo pale kwenye comment section tupo pamoja.
Mfumo wa pagination unaotumika sasa hivi kwenye JamiiForums (ule wa next, next kila mara) bado ni wa kizamani na una changamoto kadhaa kwa watumiaji. Kila unapobonyeza "next" ili kuona machapisho zaidi, ukurasa mzima unalazimika kupakia upya.
Hii inamaanisha kuwa mtumiaji anatumbukia kwenye matumizi makubwa ya bando au data kwa sababu maudhui yote yanajirudia kupakiwa tena, badala ya yale mapya pekee. ni sawa unatoka Facebook.com na unaelekea Instagram.com hiki ndicho hufanyika kwanini ?
Ukurasa mzima unapo loading upya kila unapobonyeza next next unakuwa ni sawa sawa na kufungua tu kitu kipya kabisa au mtandao mwengine nafikiri ninaeleweka, hapa namaanisha unapo bonyeza next next browser ya kifaa chako inachukulia kama unahama ukurasa mzima na kufungua mpya hapa bdipo inaamua kuloading ukurasa mzima upya ili wewe kuona machapisho zaidi.
Suluhisho linalopendekezwa ni kutumia mfumo wa kisasa wa infinite scrolling. Katika mfumo huu, mtumiaji anapoteleza chini kwenye ukurasa (scroll down), machapisho mapya yanaendelea kujipakia kiotomatiki bila kulazimisha ukurasa mzima kupakia upya. Hii itarahisisha matumizi, kupunguza muda wa kungoja, na zaidi ya yote, kuokoa data za watumiaji.
Mfano ni jinsi tunavyosoma maoni (comments) kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram — unashuka chini na machapisho mapya yanaendelea kuonekana bila kubonyeza "next". pale unakuwa unaokoa data, unapata realtime updates ect.
Hata hivyo, kuna kipengele muhimu cha kuzingatia: footer, bottom navigation na legal links hazitakiwi "kutiririka" na infinite scrolling. Vinapaswa kuwa fixed ili mtumiaji aweze kuvifikia kwa urahisi muda wowote, hata kama anaendelea kusoma machapisho zaidi chini ya ukurasa.
Kwa kifupi:
Pagination ya sasa: inasababisha kurudia kupakia ukurasa mzima → matumizi makubwa ya data.
Infinite scrolling: inapunguza matumizi ya data, inarahisisha urahisi wa kusoma machapisho, na ni mtindo wa kisasa unaotumika mitandaoni.
Marekebisho muhimu: kuweka footer na navigation links kwenye nafasi ya kudumu (fixed) ili zisipotee wakati wa kushuka chini kusoma.
Ndugu Maxence Melo asante kwa kutambua mchango wangu huu.