Hii ndio habari iliyoko mtandaoni kwa sasa kuhusu lile tawi jipya liliofunguliwa hivi karibuni huko maeneno fulani ambapo japo mwanzo ni mgumu,lakini mwanzo huo unaonekana si dalili njema hata kidogo.
Maelezo yanayotolewa mtandaoni nashindwa hata kuyaamini kuhusu hilo tawi na kama madai kuhusu idadi ndogo sana ya wateja wanaofika katika tawi hilo ni ya kweli,basi ni wazi ule utafiti haukua utafuti bali ulikuwa utafuti jina tu.
Mtoa habari amewaambia waandishi wafike kujionea hali halisi.
kwa sasa najua tutajipa moyo kuwa tawi bado ni jipya ila uzuri ni kwamba hatuwezi kuendelea kujipa moyo iwapo hali kama hii itaendelea hata kwa miezi mitatu tu.
Anyway,labda tuwape muda.
Nawaza tu kama watu wataruhusiwa kupiga picha eneo hilo katika siku zijazo.