Tetesi: Tawi jipya la CRDB Chato, Idadi ya wateja inadaiwa ni ya kuvunja moyo

Wateja ni saba kwa siku, mateller wanashinda wakipiga story
Muda anaoutumia Teller kuperuse JF na kupost picha FB ni mrefu kuliko anaoutumia kuhudumia wateja watatu per day. Ila mzee Magu atakuja na plan B. Usishangae wafanyakazi wote wa Serikali pale Chattle wakapewa agizo na Mkurugenzi wafungue accounts pale na mishahara yao kila mwezi iwe inapitishiwa hapo
 
Unaandika mipasho huku GT tunaongelea uhalisia wa maisha ya watz wengi.
Uharo mtupu!!
Cc:Sheiza
 
Unachosema ni kweli kabis mkuu ila kitu ambacho hukifahamu ni kuwa kuna taratibu za ujumla zinazofanya mji kukua. Na moja ya hivyo vitu ni accessibility.. Ukikaa huko ndani unaweza ukafanikiwa kukua kama mji ila utakuwa kwa nguvu nyingi sana. Resource ambazo zitatumika kuijenga chato ikiwa zitawekwa Geita itakuwa Mara tatu zaidi..

Na kukua kwa miji kunaongeza development catchment area.. Mfano kwa accessibility ya dar na majirani zake.. Mkuranga mpaka rufiji na Kibaha mpaka Chalinze na morogoro.. Bagamoyo msata hats mpaka Handeni.. Zanzibar na pemba zote zina access huduma za dar.. Kwa sababu inafikika kirahisi na IPO kwenye uelekeo..

Chato imejificha sana.. Inaenda kinyume na mpango wetu Wa makao.makuu ya mikoa yakae wilaya za katikati.. Dodoma IPO katikati ya Tanzania, ukifuatilia makuu ya mikoa mingi yapo katikati ya mikoa kurahisisha ufikikaji. Kwa suala LA biashara chato inachangamoto.. Uzalishaji sio mkubwa.. Sio transit town.. Hats ukiifanya manufacturing hub bado itapokea ushindani kutoka katika miji iliyoko katika mabarabara makuu..

Kwa sababu miji iliyoko katika mtandao Wa Barbara kuu za kitaifa unacatchment area kubwa kwa maana ya rasilimali.. Usafiri ni cheap na options ni nyingi.. Viwanda katika maeneo haya vinaweza kusambaza bidhaa sehemu kubwa kwa gharama ndogo. Na vitapokea rasilimali nyingi kwa gharama ndogo maana vitafikika kirahisi.

Chato inaweza kukua kama tutaamua ku- suppress maendeleo ya competing towns.. Hiyo ndio njia pekee. Na hapo itaanza kuwa sio fair kwa watanzania wengine. Tusihadaike hakuna njia ya mkato na ukiiachwa umeachwa tu. Hats uhangaike vipi.
 
Miji ni kama watu.. Wanakuwa.. Unadhani kwann serikali haikujrnga skyscrapers dar es salaam mwaka 1970?! Hatukuwa na uhitaji wakati huo!

Huwe kumnunulia mwanao gari ya kutembelea akiwa na miaka 2.. Kwa maana hana uhitaji wakati huo.. By the time anauhitaji itakuwa imepitwa.. Na hats kupata vipuri itakuwa shida..

Hii inatuleta kwenye dhana ya double loss... Unaponunua kitu ambacho haukihitaji inakuwa umepoteza pesa na unakitu ambacho ukitumii ambayo ni kama hauna tu..

Chato ni kijiji.. Hakina hata watu 30,000 kwa hapa mjini ni kata.. Huwezi ukatumia pesa ya watanzania tena wanaohitaji sana hizi huduma ukaenda kuziweka kichochoni wasipoweza kuzifikia..

Tumbi kibaha hospitali kubwa.. Lakini wagonjwa wa mkuranga, rufiji, bagamoyo wanaishia CCBRT .. Why ? Its more accessible.. Magari mengi tayari yanakuja uelekeo huu.. Watu wanapata urahisi Wa kupata kufika katika huduma.

Key ilikuwa ni kugenerate trips.. Kwa kuwekeza katika vitu anbavyo vingechochea uzalishaji na kuinua kipato cha eneo husika.. Ndio uanze kuweka huduma nzito kama hospitali za rufaa na makao makuu ya wilaya.. La si hivyo.. Watakuwa wanasafiri wagonjwa na wafanyakazi tu..
 
Kwahiyo Geita mkoa!, then tutarajie mkoa mpya!!! Tutapeleka mpaka treni lakin Chato iitabaki kua chato! na speed hii ya kukua huo mji huo unaweza kuingia kweny Jarida la Billboard! Next time tutapata mwingine kutoka tabora! Huko Kiliua! Atataka naye Kiliua iwe mkoa! HONGERA WANACHATO! Tumien fursa za mzee baba msije sema hakuwakumbuka!
 
Kwa maneno ya mitandaoni hata maandamano yametiingisha serikali.
Kwa hiyo kama imetingishika umepata nini?
Tukiwaambia kuwa nyie ni watu wa mizaha na wapigaji mnabisha
Hivi kweli unaweza kujisifia kuitingisha tu serikali bila ya matakwa yako kufanikiwa?
Kwa upinzani huu wa mitandani ccm inaweza kutawala hadi mwaka 3000
 
Kimsingi sipingi hoja zako lkn natamani tuwe tunajadili kwa mfumo huu.

yaani chato kutoa rais isiwe sababu tosha ya kutopata maendeleo, mleta thread na wengine wengi wanafanya kuwa ni kitu kibaya sana rais kupeleka maendeleo kwao! kitu ambacho si sahihi maeneo yetu mengi yalipaswa kuwa zaidi ya hivi yalivyo kama marais wetu pengine na sisi wenyewe tungetimiza wajibu wetu sawasawa hivyo juhudi za kuufikisha moja ya mji wetu kule ulikopaswa kuwa si tatizo mfano mtu analalamikia trafiki light na barabara ya lami kuwekwa chato unamshangaa si chato tu tanzania nzima hakuna sehemu inastahili kuwa na barabara ya vumbi tulipaswa kuwa na barabara nzuri za lami zinazopitika vizuri hasa sehemu zenye mazao ya kilimo ili yatoke huko kirahisi kuja mijini lkn mtu anapinga ukimuuliza tatito ooh ni kwao rais.
huduma za kibenki serikali inapaswa kuzifikisha kila mahari ili kuwezesha kwanza ukusanyaji wa kodi, kuwezesha uwekezaji hivi unampelekaje kijijini mwekezaji aliezoea kwao e.money kijiji kusikokuwa na benki akabebe mshahara kwenye masandarusi huku ukijua upungufu na uwezo wa polisi wetu katika kulinda na kusafirisha pesa hutaki benki ijengwe ukiulizwa aah nyumbani kwao rais.

angalau tuje na detail kama hizi za kusapoti hoja zetu sio sababu za kijinga kama kwao rais hizo ni tabia za kibaguzi tu.
 
Akili zako ni kubwa sana mkuu.
 
kinachonifurahisha ni kuwa inayojengwa ni tz na si kenya wala rwanda so pesa za watanzania zinarudi kwa watanzania. kingine tumempa dhamana ya kuendesha nchi na kwakusaidiana na wawakilishi wetu kuchagua ni wapi watawekeza kwa niaba yetu tuwaache waone wapi kunafaa wakichemka 2020 si mbali tutawaambia hamtufai mlitupa hasara sasa tunawapa wengine nao watuongoze hivyo tu lkn tukimzuia leo akichemka 2020 atasema nyie ndio mlinizuia ningewekeza kule pangelipa.
 
2020 ilishapita mazee, sasa tunajenga hospitali ya KANDA Chato, baada ya kumaliza kujenga chuo cha ufundi stadi (VETA).
 
Hatimaye yametimia, naskia bank kwasasa ni club
 
Sasa hivi imegeuzwa kuwa Chato Club
 
Katika mambo ya Uchumi, kwa Shirika kubwa kama CRDB, sio lazima kila point u- realize profit emedeately, hapana,
But, in the long run, unaweza kukuta pointi uliyokuwa unaidharau ndio best!
Ndio maana biashara nyingi za waswahili aidha ni za magendo au za magumashi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…