Tazama foleni hii ya wanunuzi wa sukari Morogoro. Juzi Waziri Bashungwa kapitishiwa bajeti ya hovyo iliyoungwa mkono na wanaccm wote Bungeni

Ni vita hiyo hiyo ila safari hii ni vita ya kibaiolojia ( Corona)
 
Kuna watu humu wanasema kwao inapatikana kwa bei elekezi 2600 kwa kilo. Sijui ni wapi huko. Jana niligundua sukari ambayo nilikuwa nimenunua kwa 3600 kwa kilo imeisha. Mitaani pia hakuna. Leo baada ya ibada nimee.kezwa kwa duka la mpemba. Bei yake ni nzuri tu ila ni km 3 toka ninakoishi. Huyu a afanya bei ya haki ya mfungo kwa 3000. Naskia hao wabei za jumla ndio wanawauzia wa rejareja kwa 128,000 kwa kiroba cha 50 kg. Sasa huyu wa rejareja atauza kwa bei gani? SERIKALI IFUATILIE WAUZAJI WA JUMLA. TUNAOMBA WAWEKE ULINZI NA KILA DUKA LA ENEO HUSIKA WAUZIWE HIYO SUKARI BILA ULANGUZI. Hao wanaogawia watu sukari ni siasa tu. Waingie mitaani waulize ktk maduka ya rejareja kama watapata sukari.HIVI NI KWA NINI INAKUWA HIVI KILA MWAKA? JE UAGIZAJI WA SUKARI NJE UNACHELEWESHWA KWA AJILI GANI? HILI SIO LENGO LA KKUFANYA BEI IWE JUU?
 
Kuna lockdown ya ndani na ya nje . ama Intra na inter lockdown.
Nchi inategemea supplies kutoka Zambia, Kenya, Brazil pia.
 
Kwani sisi tuna lockdown, yani kweli utetezi mwingine muwe mnaona aibu
Kuna lockdown ya ndani na ya nje . ama Intra na inter lockdown.
Nchi inategemea supplies kutoka Zambia, Kenya, Brazil pia.
 
Hata kama usemavyo ni kweli. Swali :Je sukari ipo mitaani?? Je ukibahatisha utauziwa kwa bei elekezi ya Serikali??
Acheni siasa kwenye masuala yanayowahusu au kuwaumiza Wananchi bila sababu za msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoa maamuzi wameshindwa kutambua kanuni ya "Supply and Demand". Supply ni kiduchu Demand ni bwerere. Unategemea nini? Bei juu. Hata utumie bunduki na majeshi huwezi kushinda nguvu ya soko.
 
Yaani mtu asote hivyo halafu umpangie bei?
 
Serikali ya awamu ya tano imejaa mbumbumbu watupu wanaojiita ni wasomi.

Useless politicians

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna lockdown ya ndani na ya nje . ama Intra na inter lockdown.
Nchi inategemea supplies kutoka Zambia, Kenya, Brazil pia.
Supply ya sukari kwenye soko itaendelea kuathirika kwa sababu nchi tunakoagiza ziko kwenye lock-down. Uzalishaji wa viwanda vya ndani ni mdogo. Kwa hali hiyo lazima bei ipande tu. This is the simple law of economics!
 
Supply ya sukari kwenye soko itaendelea kuathirika kwa sababu nchi tunakoagiza ziko kwenye lock-down. Uzalishaji wa viwanda vya ndani ni mdogo. Kwa hali hiyo lazima bei ipande tu. This is the simple law of economics!

Ndiyo mkuu, sasa mie nashangaa hawa wanaoshangaa.
 
Sukari ikikosekana mbali na hivyo viwanda unakuwa umeua biashara zote za kina mama ntilie ambao wanaendesha familia zao kwa kazi hizo.

Hii awamu ya tano imejaa watu useless kabisa wameshindwa kutatua suala la sukari tu masuala mazito wataweza hawa mbumbumbu ?

No wonder wamejificha vijijini kukimbia corona nchi inajiendea tu autopilot

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika kipindi hichi cha hili janga na hivi tulivyo kama mayatima vitu vingi sana vitapanda bei muda utaongea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…