Tazama foleni hii ya wanunuzi wa sukari Morogoro. Juzi Waziri Bashungwa kapitishiwa bajeti ya hovyo iliyoungwa mkono na wanaccm wote Bungeni

Hiyo ni effect ya lockdown. Na wala si Tanzania hata nchi zingine watu hawaruhusiwi kununua zaidi ya packt 2 ya maziwa ama sukari tena in heart of europe.
Tanzania umesikia tumefunga viwanda na watu kuamliwa wakae nyumbani? Au umesikia Kenya na Rwanda wanapanga foleni japo waliwazuia watu kutaka? Tanzania hatuna kiongozi ndugu nchi inaenda kama gari bovu nikimnukuu maneno ya Rais mstaafu Mwinyi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mafisadi yanayohujumu yajiandae

Wale ambao baada ya vita ya nduli Idi Amin hamukuwepo basi hivi ndio tulivyopanga foleni kupata unga wa Yanga, Viberiti, Sigara, Bia, Betri za radio, Viatu vya bora (Raizone), Kununua radio cassete mshale au Phillips n.k lakini ilikuwa ni sababu ya vita na leo sijui dhahama hii imeletwa na nini naomba mnijuze.
 
Tujifunze kuishi bila sukari. Sukari nyingi inasababisha unene na magonjwa yasiyoambukiza.
 
Sukari sio kwamba haipo sema imejificha inaogopa yaliyowapata akina papai fenesi oil nk

Ikaona yasije yakawa makubwa afanywe sample ya covid19

Itarudi mkimalizana na corona yenu hata chumvi nasikia anataka amuige sukari


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni effect ya lockdown. Na wala si Tanzania hata nchi zingine watu hawaruhusiwi kununua zaidi ya packt 2 ya maziwa ama sukari tena in heart of europe.
Lockdown umeianzisha kwa amri ya nani wewe,wakati baba Jesca ameapa kutosikia kitu kama hicho aslani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi tz si tuna maviwanda elfu ngapi sijui...huwa yanatengeneza/yanazalisha nini
 
Za kuambiwa changanya na zako,

bei ya asali inalingana na bei ya sukari? Licha ya kuwa asali ni nzuri kiafya lakini je ni watanzania wangapi watamudu kutumia asali kama mbadala wa sukari?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo asali nyingi unayoiona inauzwa aidha barabarani sokoni au kutembezwa mitaani inakuwa imechakachuliwa na haifai kwa matumizi ya binadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ingeanzia kwa waagizaji wa sukari kutoka nje hapo sukari inaweza kupatikana wao wameanza tu kudhibiti bei bula kujua sukari imeingia kwa bei gani
 
Tunarudi enzi za ugawaji pindi gari la kugawa bidhaa likionekana lilikuwa lilikimbilia mtaa mzima Kama watu wameona ngekewa.
 
Hao jamaa hata hawajavaa barakoa, au wapo Lesotho nini? Hawana kabisa wasiwasi, sukari imewavuruga akili. Serikali ilipanga bei elekezi bila kujua upatikanaji wa sukari, acha tu waifiche, hakuna aliye tayari kupata hasara.

Magufuli ni janga la Taifa.
 
Zanzibar kuna kiwanda kikubwa cha sukari sijui kwanini wasiruhusu iletwe huku bara....

Kiroba cha sukari kilikuwa kinauzwa elfu hamsimi na sita kama sikosei lakini sasa imepanda hadi kufikia elfu 96
Znz ni nchi nyingine kwenye masuala ya kodi
 
Kile kiwanda cha sukari cha azam cha bagamoyo vipi akijaanza kutoa sukari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…