Tazama katika Picha, Ofisi ya CHADEMA Mkoani Mbeya

Tazama katika Picha, Ofisi ya CHADEMA Mkoani Mbeya

Ofisi za CCM usifananishe na huo uchafu. Hivi unaelewa kuwa hicho ni kikao cha kanda na chenye kuongozwa na katibu mkuu wake John mnyika? Hivi unaweza kumpeleka Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi kwenye pagala kama hilo akafanyie kikao kazi?
Kwamba nchimbi akikaa kama hapo makalio yake yataota miba au sio!! Kweli wewe ni Mwashambwa hasara kwa mama
 
Ujinga uko wapi kwenye comment yangu
Wewe si unaona ni sawa CHADEMA kinachopokea mamilioni kwa mamilioni ya pesa za walipa kodi kuwa kwenye chumba kama hicho kilichokosa hata hewa na kukiita ofisi?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Tuseme nini muelewe ya kuwa CHADEMA ni chama cha kitapeli na ubabaishaji? Tuwaonyeshe nini muelewe ya kuwa CHADEMA ni genge la wasaka Tonge na wachumia tumbo? Tuongee na kuzungumza nini muelewe ya kuwa hiki ni chama cha madalali wa kisiasa tu wasio na mipango wala mikakati ya aina yoyote ile ya kugusa Maisha ya watanzania, zaidi ya kusaka madaraka ya ubunge na udiwani kwa ajili ya kushibisha matumbo yao?

Inawezekana vipi ndugu zangu hizi ndio zikawa ofisi za chama na kufanyia vikao vya kanda kwa ajili ya mafunzo ya viongozi wake wapya wa kanda? Kweli chama chenye watu wenye utimamu wa akili na mwili na wanaojitambua wanaweza kukaa kwenye chumba hiki chenye giza na kuita ofisi?

Hivi hii ni ofisi au mgahawa wa uchochoroni au gest bubu au mahali wanapokutania watu wanaopanga matukio ya uhalifu? Hivi chama kinacho pokea Ruzuku ya Milioni 107 kwa mwezi kinaweza kukaa katika ofisi ya namna hii? CHADEMA miezi michache iliyopita walipata Ruzuku ya Billion 2.7. inakuwaje wakae kwenye chumba hiki cha kihuni huni kisicho hata na madirisha ya kueleweka kiasi hiki?

Hivi mnyika aliye katibu Mkuu anajitambua kweli? Haoni aibu? Wameshindwa hata kukodi au hata kuazima ukumbi makanisani wakafanyia kikao chao? Kuliko Aibu hii ya kukaa kwenye chumba cha kihuni ambacho hakina mwanga wa kutosha wala hewa nzuri wala mpangilio wa kueleweka?

Ni vipi watu waliopo humu watakuwa huru kutoa mawazo yao yenye kujenga wakati mazingira yenyewe ni mabaya na ya hovyo kiasi hicho? Wamebanana Utafikiri watu waliosombwa na difenda ya police. Halafu unakuta bila aibu wanabetua midomo yao wanasema eti wanaweza kuongoza Nchi.

Tazama tu nyuso zao walivyojikatia tamaa ,kupoteza matumaini,kujawa na msongo wa mawazo na kuwa hapo walipo kimwili tu lakini kiakili unaona kabisa hawapo hapo kabisa. Kwa hakika CHADEMA ni chama cha hovyo kuwahi kutokea hapa Nchini.

Tufike mahali kama Taifa tukubaliane kuwa ni CCM pekee yenye uwezo wa kuongoza Taifa letu na ni CCM pekee yenye uwezo wa kutoa Rais bora na hakuna sababu ya kufanya uchaguzi wa Urais zaidi ya kumuidhinisha tu yule aliyepitishwa na CCMView attachment 3081557.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kuna ka kauli kao kuwa "Chama Kiko mioyoni mwao na sio kwenye majengo" Ahahahahaha!!! Halafu baadae wanakejeli miundombinu ya Serikali! Ahahahahaha!!!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Tuseme nini muelewe ya kuwa CHADEMA ni chama cha kitapeli na ubabaishaji? Tuwaonyeshe nini muelewe ya kuwa CHADEMA ni genge la wasaka Tonge na wachumia tumbo? Tuongee na kuzungumza nini muelewe ya kuwa hiki ni chama cha madalali wa kisiasa tu wasio na mipango wala mikakati ya aina yoyote ile ya kugusa Maisha ya watanzania, zaidi ya kusaka madaraka ya ubunge na udiwani kwa ajili ya kushibisha matumbo yao?
Ungekuwa una akili, ungetambua chochote wanachofanya Chadema kinatokana na jasho lao na mifuko yao wenyewe. Na hayo makubwa ya CCM unayatambia hukuna hata senti inayotoka katika mifuko yao.

Sasa kwa ulinganifu huu, ni nani anastahili pongezi? Chadema wanafanya mambo ndani ya umasikini wao, wakijitolea kile ambacho kinapaswa kwenda kulisha na kusomesha watoto wao. Utajiri wa CCM ni kutokana na kujitolea kwa wanachama wao? Au hujui kwamba watu kama Wakurugenzi wa mashirika kama THA huwa wanaambiwa watoe fedha CCM na kuandika maelezo wataayojua? Sasa nikuambie ukweli, kuna hata consultancies wanapewa tenda hewa ili wakilipwa na srikali hela wazipeleke CCm na wabaki na 20%. Hivi unafikiri watu kama kina Nimrodi Mkono aliekufa alikuwaje tajiri? Unajua tenda hewa alizokuwa akipewa na serikali? Umejiuliza kwa nini alikuwa analipwa mabilioni kwa ajili ya kesi za serikali ambazo serikali ilijua hazina mshiko? Unafikiri zile fedha alichukua zote?

Sasa kwa taarifa yako, kuna watu waliachishwa kazi kwenye mashirika ya umma kwa kukataa kuchota fedha kwa ajili ya CCM na kuambiwa wazitafutie maelezo wao wenyewe.

Mambo mengine utaacha tuseme humu ambayo hatustahili kusema. Ukome kabisa kulinganisha uwezo wa fedha wa vyama vya upinzani na CCM. Unafikiri CAG anaposema trilioni 15 zilitumika hazina maelezo zilienda wapi? Unafikiri matumizi ya fedha ya CCM yanatokana na fedha halali wanazokusanya? Kwa miradi gani, kadi za wanachama? Unajua kina Mwiguliu wanavyoamriwa "watafute" fedha kwa ajili ya Chama? Unafikiri ni kwa nini kina Mwigulu wamekuwa matajiri sana? Akiambiwa "atafute" bilioni 200 za CCM ambazo hazina maandishi unafikiri anawakilisha zote huko CCM?

Ni mtu mpumbavu tu atawacheka Chadema katika umasikini wao akiwalinganisha na CCM.
 
Ungekuwa una akili, ungetambua chochote wanachofanya Chadema kinatokana na jasho lao na mifuko yao wenyewe. Na hayo makubwa ya CCM unayatambia hukuna hata senti inayotoka katika mifuko yao.

Sasa kwa ulinganifu huu, ni nani anastahili pongezi? Chadema wanafanya mambo ndani ya umasikini wao, wakijitolea kile ambacho kinapaswa kwenda kulisha na kusomesha watoto wao. Utajiri wa CCM ni kutokana na kujitolea kwa wanachama wao?

Ni mtu mpumbavu tu atawacheka Chadema katika umasikini wao akiwalinganisha na CCM.
Billion 2.7. za Ruzuku zimekwenda wapi? Ruzuku ya milioni 107 kila mwezi inakwenda wapi?
 
Acha kutetea ujinga wewe.kwa hiyo miaka zaidi ya 32 mmeshindwa kujenga ofisi? Mnazidiwa hadi na Act Wazalendo? Ruzuku mnapeleka wapo wakati kila wakati mnatembeza mabakuli kuomba misaada?
Usilolijua ni kwamba ofisi za ccm zilijengwa na watu wote enzi za chama kimoja. Baada ya vyama vingi ccm ikatwaa mali zooote vikiwemo viwanja vya mpira wa miguu.
Kwakuwa umejawa na ujinga hili nalo utabisha
 
Billion 2.7. za Ruzuku zimekwenda wapi? Ruzuku ya milioni 107 kila mwezi inakwenda wapi?
Umewahi kuomba matumizi ya Chadema ukaona zilivyotumika na kiasi gani cha ruzuku kinabaki ili uwashutumu? Omba mchanganuo wa matumizi ya ruzuku yao kila mwezi ukiona hayana mshiko njoo huku utuonyeshe, sio kupiga kelel bila lojiki utafikiri una mimba changa. Kama unaona ni aibu wao kuwa na ofisi hizo, unafikiri wao wanapenda kuwa na hizo ofisi huku hela za ruzuku zipo tu?

Labda anza na kuuliza ruzuku ya CCM ni shs ngapi, kisha uwaulize inatumika kwenye shughuli gani, na uone hata kama inatosha, na ulinganishe matumizi ya CCM ya ruzuku na yale ya Chadema
 
Usilolijua ni kwamba ofisi za ccm zilijengwa na watu wote enzi za chama kimoja. Baada ya vyama vingi ccm ikatwaa mali zooote vikiwemo viwanja vya mpira wa miguu.
Kwakuwa umejawa na ujinga hili nalo utabisha
Embu nijibu swali hili dogo.nini kimewafanya mshindwe kujenga ofisi licha ya kupokea mamilioni kwa mamilioni ya Ruzuku kwa miaka mingi?
 
Umewahi kuomba matumizi ya Chadema ukaona zilivyotumika na kiasi gani cha ruzuku kinabaki ili uwashutumu? Omba mchanganuo wa matumizi ya ruzuku yao kila mwezi ukiona hayana mshiko njoo huku utuonyeshe, sio kupiga kelel bila lojiki utafikiri una mimba changa. Kama unaona ni aibu wao kuwa na ofisi hizo, unafikiri wao wanapenda kuwa na hizo ofisi huku hela za ruzuku zipo tu?

Labda anza na kuuliza ruzuku ya CCM ni shs ngapi, kisha uwaulize inatumika kwenye shughuli gani, na uone hata kama inatosha, na ulinganishe matumizi ya CCM ya ruzuku na yale ya Chadema
Kwa hiyo Ruzuku mnajazia matumbo yenu tu? Pesa za Join the chain zipo wapi?
 
Back
Top Bottom