Ndugu zangu Watanzania,
Tuseme nini muelewe ya kuwa CHADEMA ni chama cha kitapeli na ubabaishaji? Tuwaonyeshe nini muelewe ya kuwa CHADEMA ni genge la wasaka Tonge na wachumia tumbo? Tuongee na kuzungumza nini muelewe ya kuwa hiki ni chama cha madalali wa kisiasa tu wasio na mipango wala mikakati ya aina yoyote ile ya kugusa Maisha ya watanzania, zaidi ya kusaka madaraka ya ubunge na udiwani kwa ajili ya kushibisha matumbo yao?
Inawezekana vipi ndugu zangu hizi ndio zikawa ofisi za chama na kufanyia vikao vya kanda kwa ajili ya mafunzo ya viongozi wake wapya wa kanda? Kweli chama chenye watu wenye utimamu wa akili na mwili na wanaojitambua wanaweza kukaa kwenye chumba hiki chenye giza na kuita ofisi?
Hivi hii ni ofisi au mgahawa wa uchochoroni au gest bubu au mahali wanapokutania watu wanaopanga matukio ya uhalifu? Hivi chama kinacho pokea Ruzuku ya Milioni 107 kwa mwezi kinaweza kukaa katika ofisi ya namna hii? CHADEMA miezi michache iliyopita walipata Ruzuku ya Billion 2.7. inakuwaje wakae kwenye chumba hiki cha kihuni huni kisicho hata na madirisha ya kueleweka kiasi hiki?
Hivi mnyika aliye katibu Mkuu anajitambua kweli? Haoni aibu? Wameshindwa hata kukodi au hata kuazima ukumbi makanisani wakafanyia kikao chao? Kuliko Aibu hii ya kukaa kwenye chumba cha kihuni ambacho hakina mwanga wa kutosha wala hewa nzuri wala mpangilio wa kueleweka?
Ni vipi watu waliopo humu watakuwa huru kutoa mawazo yao yenye kujenga wakati mazingira yenyewe ni mabaya na ya hovyo kiasi hicho? Wamebanana Utafikiri watu waliosombwa na difenda ya police. Halafu unakuta bila aibu wanabetua midomo yao wanasema eti wanaweza kuongoza Nchi.
Tazama tu nyuso zao walivyojikatia tamaa ,kupoteza matumaini,kujawa na msongo wa mawazo na kuwa hapo walipo kimwili tu lakini kiakili unaona kabisa hawapo hapo kabisa. Kwa hakika CHADEMA ni chama cha hovyo kuwahi kutokea hapa Nchini.
Tufike mahali kama Taifa tukubaliane kuwa ni CCM pekee yenye uwezo wa kuongoza Taifa letu na ni CCM pekee yenye uwezo wa kutoa Rais bora na hakuna sababu ya kufanya uchaguzi wa Urais zaidi ya kumuidhinisha tu yule aliyepitishwa na CCM
View attachment 3081557.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.