Tazama katika picha watu walivyomiminika na kufurika kwa wingi katika Kumpokea Rais Samia Gairo Mkoani Morogoro

Tazama katika picha watu walivyomiminika na kufurika kwa wingi katika Kumpokea Rais Samia Gairo Mkoani Morogoro

Wakati wa kugawa 10k, kofia, khanga, vitenge na t-shirt imewadia. Na wananchi walivyo na utindio wa ubongo watahadaika kwa hivyo vijisenti.
Watanzania wanafahamu ni nani na chama kipi kinafaa kuwaongoza. Watanzania wanafahamu ya kuwa ni CCM na Rais Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan mwenye uwezo wa kuwaongoza na kuwaletea maendeleo endelevu
 
Wengine wamesombwa na malori, wakidaiwa kuwa eti ni wahamasishaji toka Morogoro mjini!

Siyo maneno yangu, hata Mama mwenyewe aliuliza wanyooshe mikono, waliokuja toka Morogoro mjini!😅
Fiksi
 
Watanzania wanafahamu ni nani na chama kipi kinafaa kuwaongoza. Watanzania wanafahamu ya kuwa ni CCM na Rais Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan mwenye uwezo wa kuwaongoza na kuwaletea maendeleo endelevu
Sawa chief, upitie Lumumba ukusanye kitita cha wiki.
 
View attachment 3059434
Ndugu zangu Watanzania,
Muwe Mnaelewa tunapowaambia ya kuwa Rais Samia anakubalika,kupendwa na kuungwa mkono ni haijapata Kutokea. Amekaa katika mioyo ya watu mpaka watu wanabubujikwa na machozi ya furaha wamuonapo. Watu wanakuwa na hamu na kiu kubwa sana ya kumsikiliza Mama ili wapate neno.

Embu angalia kwa picha tu namna alivyopokewa kwa wingi na maelfu ya wananchi waliofurika na kumiminika kwa wingi utafikiri mchanga wa bahari ,kumlaki Rais wetu mpendwa eneo la Gailo mkoani Morogoro ambako ameingia kwa ajili ya Ziara ya kikazi.

Ikumbukwe ni siku chache tu alikuwa na ziara ndefu mikoa ya nyanda za juu kusini ,ambako nako alipata mapokezi makubwa na ya kihistoria kwa kupokelewa na maelfu kwa maelfu ya wananchi kwa kila alipopita na kufika.

Kwa hakika nyota njema huonekana asubuhi na Rais Samia ni Nyota njema inayoendelea kung'ara, kuangaza na kuleta nuru na matumaini kwa mamilioni ya Watanzania.View attachment 3059665

Kazi iendelee Mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa Mama anatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.View attachment 3059670
Soma zaidi: Rais Samia anatarajiwa kufanya ziara ya siku sita mkoani Morogoro mwanzoni mwa mwezi Agosti
Mbona watoto wa shule ni wengi sana?
 
Mkutano ulifanyika kwenye uwanja wa shule. Wanafunzi walikuwa wengi mno.

Pia watu walisombwa kama kawaida. Bila kusomba watu na kutumia wasanii mkutano unakuwa na watu wachache mno.
 
Mkutano ulifanyika kwenye uwanja wa shule. Wanafunzi walikuwa wengi mno.

Pia watu walisombwa kama kawaida. Bila kusomba watu na kutumia wasanii mkutano unakuwa na watu wachache mno.
Naona mnaendelea kuhamisha magoli tu.
 
Back
Top Bottom