TAZARA inahujumiwa na viongozi?

TAZARA inahujumiwa na viongozi?

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Kwa kweli sielewi. Kama ni hujuma basi ni kubwa sana. Kwamba Serikali haioni jinsi malori ya wafanyabiashara wanavyoirarua babara ya TANZAM , haingii akilini.

Kwamba Serikali haioni jinsi TAZARA inavyozidi kudorora huku mizigo inachukuliwa na wafanyabiashara, haingii akilini.

Wafanyabiashara wa usafirishaji na viongozi fulani inaelekea wako dugu moja.

Kwamba Serikali ipo, na viongozi wapo na hakuna hatua yoyote inachukuliwa, haingii akilini.

Lawama zangu ni kwa viongozi wangu, tena wa kitaifa.

Ukweli na Uwazi.
 
Itakuwa haina faida kisiasa na pengine kiuchumi haichangii sana ndio maana inachukuliwa poa.
 
Kwa kweli sielewi. Kama ni hujumabasi ni kubwa sana. Kwamba serikali haioni jinsi malori ya wafanyabiashara wanavyoirarua babara ya TANZAM , haingii akilini.

Kwamba serikali haiini jinsi TAZARA inavyozidi kudorora huku mizigo inachukuliwa na wafanyabiashara, haingii akilini.

Wafanya biashara wa usafirishaji na viongozi fulani inaelekea wako dugu moja.

Kwamba serikali ipo, na viongozi wapo na hakuna hatua yoyote inachukuliwa, haingii akilini.

Lawama zangu ni kwa viongozi wangu, tena wa kitaifa.

Ukweli na Uwazi.
Naunga mkono hoja.
Wafanyabiashara wa njia hii wamewadhibiti viongozi?
 
Ukistaajabu Ya TANZAM Utaona Ya Treni Ya SGR Toka Dar Es Salaam ~Morogoro Kutotembea Zaidi Utaambiwa Anaupiga Mwingi
Viongozi Wengi Ni Ndumilakuwili Wanahujumu Maendeleo Wazi
 
Hii hujuma ni kubwa sana. mm wakati nikiwa Kijana Mdogo nilikua naishi Mkoani morogoro ambako kuna hiyo reli imepita jirani.

Nilizoea kuona Treni ikipita ikiwa imebeba Magari, Makontena na Matank ya mafuta.

Reli ya Tazara ni muhimu sana kwa Usafiri wa mizigo ya Kongo, Zambia na Malawi. Baladala yake tumeamua kutumia Tanzam
 
Mnafahamu hayo malori yanatoa ajira kwa watu wengi kiasi gani??kuanzia madereva,mafundi,wauza mafuta,matairi,spare parts,mama ntilie,waosha magari na wengineo.Mizigo yote ikibebwa na treni hiyo workforce yote mna sehemu ya kuipeleka???
 
Mawazo ya ujima!
Una gari halafu unahofia kulipanda kwa kuwa ukiacha kutembea mshona viatu atakosa kazi.
Very low.
 
Ukistaajabu Ya TANZAM Utaona Ya Treni Ya SGR Toka Dar Es Salaam ~Morogoro Kutotembea Zaidi Utaambiwa Anaupiga Mwingi
Viongozi Wengi Ni Ndumilakuwili Wanahujumu Maendeleo Wazi
Huu udumila kuwili wa viongozi ndio unakera.
 
Mawazo ya ujima!
Una gari halafu unahofia kulipanda kwa kuwa ukiacha kutembea mshona viatu atakosa kazi.
Very low.
Huo mfano wako hauna mantiki kabisa kwenye hili swala tafuta mfano mwingine.Suala la malori linagusa maisha ya watu wengi moja kwa moja tofauti na hiyo treni.
 
Inawezekana ushirikiano wa meli, reli na malori kufanya kazi pamoja na wote wakaendelea kupata faida endelevu, haitakiwi kuhofiana eneo la nchi za SADC, EAC ni kubwa kuwezesha wote kuendelea na shughuli zao bila hofu

24 October 2018
Gauteng, Republic of South Africa
Gauteng Roads and Transport MEC Dr Ismail Vadi outlines the need for intermodal transport systems in South Africa and the rest of the Southern African Development Community region

Habari zaidi :
Mexico city, Mexico
Amerika ya Kaskazini na Mexico

Usafiri wa multimodal

Usafiri wa aina hii ndio unaotumika kutoa bidhaa kutoka mahali ilipotoka hadi inaporudiwa. Lakini kutumia vyombo kadhaa vya usafiri kufikia lengo la kuhamisha bidhaa.

Kawaida hali hii inasimamiwa na waendeshaji wa usafiri wa multimodal. Ambayo kawaida ni kampuni za usafirishaji, waendeshaji wa reli ambao kwa ujumla sio wamiliki lakini ambao hufanya mkataba wa usafirishaji wa aina nyingi kuchukua majukumu kwa utimilifu wake.

Ili wakubaliane na mabadiliko na yasiwe mabadiliko tu muundo, lakini pia mabadiliko ya ndani hufanyika ili kunufaisha sekta mbalimbali zinazokuja kusafirisha bidhaa. Kwa kufanikisha michakato hiyo imerahisishwa, ili kukuza mauzo ya bidhaa na kutoka nje ya nchi, kwa hili tutahakikisha kuwa nchi inaendelea kukua kiuchumi.

Ikiwa unataka kujua faida na hasara za aina tofauti za njia zilizopo za usafiri, tutakuacha video hii. Kwa hivyo tunakualika kuiona kikamilifu, usisahau kushiriki data hii.

BNSF Mexico Intermodal service

Source : BNSF Railway
 
Huo mfano wako hauna mantiki kabisa kwenye hili swala tafuta mfano mwingine.Suala la malori linagusa maisha ya watu wengi moja kwa moja tofauti na hiyo treni.
Ukiwa unaamini ujima, huwezi kubadilika kuwa wa kisasa.
 
Kama ingekuwa haina faida biashara ya malori njia ya TANZAM haingekuwepo.

Kwa ambao hawajasafiri kwa barabara hii inayounganisha Tanzania na Zambia-Lubumbashi DR Congo, Malawi, Zimbabwe n.k Hali halisi ya usafiri barabara ya TANZAM road ni hii Tunduma - Dar es Salaam June 2022.

Kwahiyo mleta mada ulitaka serikali ipigd marufuku malori kubeba mizigo ndipo uridhike? Ukiritimba ktk biashara siyo fasheni ya karne hii.

TAZARA wanapaswa kujiongeza kwa kupunguza bei, kupunguza mlolongo wa upakiqji mizigo na kuongeza usalama wa mizigo. Vinginevya reli hiyo itaingia kwenye vyuma chakavu.
 
Watu walishalalamikiwa kwa jambo hili ila naona kama nawe umekumbushia.
Inauma inakera sanaaa.
Ulompa mwiko ndo kaufanya kuniii dah
 
Kwa kweli sielewi. Kama ni hujuma basi ni kubwa sana. Kwamba Serikali haioni jinsi malori ya wafanyabiashara wanavyoirarua babara ya TANZAM , haingii akilini.

Kwamba Serikali haioni jinsi TAZARA inavyozidi kudorora huku mizigo inachukuliwa na wafanyabiashara, haingii akilini.

Wafanyabiashara wa usafirishaji na viongozi fulani inaelekea wako dugu moja.

Kwamba Serikali ipo, na viongozi wapo na hakuna hatua yoyote inachukuliwa, haingii akilini.

Lawama zangu ni kwa viongozi wangu, tena wa kitaifa.

Ukweli na Uwazi.
Mkuu, kama viongozi waasisi walithubutu kung'oa reli ya Dar - Lindi, Nachingwea hivi unafikiri kuwa hawa viongozi makanikia wa sasa si ndiyo watakuwa ni mahoka "empty case" zaidi.
 
Kuna documentary nyingi sana za tazara na moja mwandishi wa bbc alisafiri na hilo treni toka kapirimposhi mpk dar na kurudi.
Ntaweka hapa hiyo
 
Huo mfano wako hauna mantiki kabisa kwenye hili swala tafuta mfano mwingine.Suala la malori linagusa maisha ya watu wengi moja kwa moja tofauti na hiyo treni.
Kama ilivyoandikwa, ukiwa na mawazo ya ujima ,kuelewa ni ngumu.
 
Back
Top Bottom