Siyo tu Mungu huyu hawezi kuthibitishwa kuwepo, bali pia uwepo wake unakuwa contradicted na hali halisi kwa namna ambayo inaonesha hayupo.
Unaambiwa Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.
Aliweza kuumba dunia isiyo na kifo, mabaya, magonjwa, etc.
Lakini hakuumba hiyo, akaumba hii ya ma pandemic na matetemekonya ardhi na ma tsunami.
Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote awe mkatili hivyo kwa viumbe wake?
Uwepo wa dunia na the whole universe and every living thing in it ni uthibitisho tosha kuwa MUNGU yupo. Kazi aliyoifanya ya uumbaji inathibitisha uwepo wake.
MUNGU aliumba dunia iliyokuwa nzuri, yaani it was a perfect creation. Hakukuwa na udhaifu wa aina yoyote, wala majanga (natural disasters) ya aina yoyote ile.
Isipokuwa, MUNGU siyo dicteta na wala hakuumba machines, bali alimuumba kiumbe ambaye anauwezo wa kuchagua, kufikiri na kutenda kwa uhuru. Kiumbe huyu ni Mwanadamu ambaye ndiye aliyekabidhiwa dunia yote iwe chini ya utawala wake. Katika viumbe vyote vyenye mwili ni Mwanadamu peke yake aliyepewa akili, ufahamu, hekima, busara na maarifa, na uhuru wa kuamua, free will. Hii ilikuwa ni hatua ya kwanza ya uumbwaji ya mwanadamu.
Baada ya uumbaji MUNGU alimweka huyu Mwanadamu katika dunia iliyokuwa perfect kabisa lakini MUNGU alimpa maagizo kisha akamwacha huyu Mwanadamu aamue mwenyewe, kufuata maagizo aliyopewa ili aendelee kuishi katika dunia njema au akiuke maagizo na kujitenga na MUNGU na kuingia kwenye dunia ya matatizo.
Ndiyo maana ya tunda la uzima au tunda la mema na mabaya.
Mwanadamu kwa ukaidi alichagua tunda la mema na mabaya na kuacha tunda la uzima. Matokeo yake ndiyo hayo kwamba leo hii dunia imejaa mambo mabaya na mambo mazuri, utajiri na umaskini, ugonjwa na afya, furaha na huzuni, ujana na uzee, uhai na mwisho kifo.
Hayo yote yapo kwasababu Mwanadamu wa kwanza alichagua mwenyewe.
Kwanini MUNGU aliruhusu iwe hivyo?
Kwanza kabla ya kujibu hilo swali, tunapaswa kujua ni nini lilikuwa dhumuni la MUNGU kumuumba Mwanadamu ?
Kwa kifupi sana ni kwamba MUNGU alimuumba Mwanadamu ili huyu Mwanadamu kwa kupitia utiifu wake ambao ni wa hiari akamilike awe kama MUNGU. Kwa lugha rahisi MUNGU aliwaumba Wanadamu ili hawa Wanadamu wawe Miungu yaani tuwe watoto wake, tukifanana naye kitabia kama yeye alivyo.
Baada ya Mwanadamu kuumbwa utaona alikuwa bado hajakamilika. Ili akamilike ilimpasa kwanza kwa hiari yake awe "mtiifu" kwa MUNGU. Na ndiyo maana utaona katika Biblia imeandikwa kuwa baada ya MUNGU kumuumba Adamu na kumuweka ndani ya bustani iliyokuwa timilifu alimpa maagizo; kwanza, kuitunza bustani, pili, kutawala kila kitu ndani ya bustani hiyo, tatu, azaliane aongezeke na nne, asile matunda ya mti uliokuwa katikati ya bustani.
Utaona kwa maagizo hayo Adamu alikuwa anaandaliwa kuwa "mtiifu" ,ili akifaulu basi aingie hatua ya pili ya uumbwaji yaani akamilishwe kuwa kama MUNGU. (hii nitaielezea hapo mbele).
Unfortunately Adam alishindwa kuwa "mtiifu", badala yake akawa "mkaidi".
In every action there are consequences. Kwenye "utiifu" kuna consequences zake na kwenye "ukaidi" kuna consequences zake. Kwenye utiifi utapata uzima na mema yote. Kwenye ukaidi utapata mema kidogo, mabaya mengi na mwisho kifo.
Dunia tunayoishi sasa hivi ni sababu ya UKAIDI wa Adam.
Je, malengo au dhumuni la MUNGU lilipotea baada ya Adamu kukaidi?
Jibu ni hapana. Dhumuni la MUNGU bado liko pale pale, kumfanya Mwanadamu kuwa kama Mungu. Hivyo basi baada ya Mwanadamu kukaidi, MUNGU hakutaka kumwangamiza kabisa Mwanadamu badala yake akaruhusu kipindi cha mpito, yaani kipindi cha shida, mateso, mahangaiko, magonjwa, na kifo ili miongoni mwa Wanadamu hawa wapatikane wale watakaochagua kuwa "watiifu" ili awakamilishe katika uumbaji wake. Na ndiyo maana utaona MUNGU ameweka kanuni na taratibu za kufuata na maagizo ya nini kifanyike ili Mwanadamu akamilishwe. Maagizo hayo, na taratibu hizo na kanuni hizo ni pamoja na kumwani YESU KRISTO kama BWANA na Mwokozi.
Ukizishika kanuni hizo, na taratibu hizo na maagizo hayo basi unakamilishwa kwa kujazwa ROHO WA MUNGU. Ukishajazwa huyo ROHO MTAKATIFU basi wewe umbwaji wako unakuwa umekamilika na hapo unakuwa mtoto wa MUNGU nawe utaishi milele kama MUNGU katika dunia mpya yenye mema pekee.
Adamu baada ya kuumbwa, uumbaji wake ulikuwa haujakamilika sababu hakuwa amejazwa ROHO MTAKATIFU.
Uumbwaji wa Adamu ulikuwa ni phase one, yaani ile ilikuwa ni hatua ya kwanza ya uumbwaji. Ili aingie phase two ya uumbwaji ilikuwa ni lazima kwanza afaulu kuwa "mtiifu" sababu kwa kanuni za MUNGU, mtu akiwa mkaidi hawezi kuingia phase two ya uumbwaji. Yaani hii ROHO YA MUNGU haiwezi kukaa ndani ya mtu "mkaidi".
Nitakupa mfano mdogo sana. Mwili wa Binadamu ni kama vessel, yaani chombo kinachoweza kuhifadhi kitu ndani yake. Na ROHO WA MUNGU ni kama "moto". Sasa basi Mwanadamu akiwa "mtiifu" kwa MUNGU, mwili wake unakuwa imara na utaweza kujazwa hiyo ROHO YA MUNGU ambayo ni sawa na "moto". Lakini Mwanadamu akiwa "mkaidi" kwa MUNGU, mwili wake unakuwa dhaifu hivyo huyo ROHO WA MUNGU hawezi kukaa ndani ya chombo dhaifu sababu chombo hichi dhaifu kikiwekewa "moto", kitateketea na kuungua.
Hivyo basi ndiyo maana utaona kuwa MUNGU alihitaji kwanza Mwanadamu awe MTIIFU ili akamilishwe kiuumbaji.
Ndugu yangu
Kiranga nafikiri kwa maelezo hayo utakuwa umeelewa kuwa MUNGU yupo na kwanini dunia ipo kama ilivyo na ni nini mpango wa MUNGU kwako.
Ni rahisi sana, uwe mtiifu uingie phase two ya uumbwaji na uishi milele kwa raha mustarehe au;
Uwe "mkaidi" na ufe kifo cha milele.
Uamuzi ni wako, kifo au uzima.