Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,921
- 4,683
Mimi siamini kama ubatizo wa maji ndio wokovu kwani ingekuwa hivyo wote walio batizwa wangeokoka ref. Yuda iskariote ni mmoja wao waliobatizwa.Nimekuwa nikifuatilia kifo cha gwiji huyu wa gospo tangu kilipotokea.
Jana nilishangaa hoja ambazo Jumuia ya makanisa ya kikristo ya Nigeria na Jumuia ya makanisa ya kipentekoste kumkataa kabisa TB Joshua kama Mkristo mwenzao.
Alipoulizwa sababu ya kumkataa, mwenyekiti mmoja wa jumuia hiyo aliwahi kusema.
TB hajawahi kubatizwa, au kuonyesha alimpokea Yesu lini na wapi na kwa pastor yupi. Hawakubaliani na agenda yake kuwa yeye Yesu alimalizana naye tangu akiwa tumboni mwa mama yake mimba ambayo ilikaa miezi 15.
Kwa kanuni za kikristo na Kibiblia mtu akiwa na akili timamu ndio anatakiwa amchague Yesu sio tumboni. Lakini pia kwa wengine akiwa mtoto hubatizwa. Lkn sio tumboni na angalau aonyeshe ushahidi wao hawatapata shida kabisa.
Huyu ndiye Gwiji wa injili aliyekuza sekta ya utalii nigeria kwa njia ya injili. Kuna mwaka ulifika ndege ikitua na wazungu 10 nigeria zaidi ya sita wote walikuwa wanaenda SCOAN kulamba upako.
Ubatizi wa maji ni dhamira safi kwa watu kwamba umemwamini Kristo ila sii uthibitisho maana Kristo mwenyewe ndie humpa/batiza mwaminiyo kama uthibitisho wa kuikubali imani yake.
Wala hili la kuongoza mtu sala ya toba kwa kumkaririsha kurudia kile unachomwambia sii la kimaandiko. Hakuna mahali mitume wala wanafunzi wa Yesu mwanzoni walipowahi kufanya hivyo zaidi ya kwamba walilihubiri neno na wale waliolisikia wakaliamini walibatizwa.
Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app