TB Joshua hakuwahi kubatizwa wala kumpokea Yesu! Nimeshangaa sana

TB Joshua hakuwahi kubatizwa wala kumpokea Yesu! Nimeshangaa sana

Kifalsafa hii hoja ni " A Priori fallacy".

Umeanza na jibu la uongo. Halafu mzigo wa kuthibitisha unawapa wengine.

Ni sawa na mimi nikuambie hapa unajibizana na Jeff Bezos tajiri mkubwa, bilionea wa Kimarekani. Mimi ni Jeff Bezos.

Ukibisha kosa si langu, kosa ni lako uliyeshindwa kuthibitisha mimi ni Jeff Bezos bilionea wa Kimarekani.

Yani nasema kitu cha uongo ambacho hakiwezi kuthibitishika, halafu mzigo wa kuthibitisha nakupa wewe.
Tumia hata mfano wa Chalamila bana 😅😅
 
Hii dini ya ukana Mungu uongo mtupu mwanzo mwisho. Hakuna hata mmoja anayeweza kuthibitisha Mungu hayupo.
Unaelewa ukisema hakuna anayeweza kuthibitisha Mungu hayupo hujathibitusha Mungu yupo?

Unaelewa huu ulimwengu uliopo unaoruhusu mabaya unathibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo?
 
Unataka uthibitishe kuwa MUNGU yupo?? imani huja kwa njia ya kusikia neno la MUNGU ni hakika ya mambo yatarajiwayo na bayana ya mambo yasioonekana.
Hayo ni mahubiri.

Thibitisha Mungu yupo.

"Hakika ya mambo yatarajiwayo na bayana ya mambo yasiyoonekana" is oxymoronic abracadabra.

Yatarajiwayo hayana hakika, ndiyo maana yanatarajiwa. Yangekuwa na hakika yasingetarajiwa, yangejulikana kwa hakika. Ukitarajia maana yake unacheza na probability, huna hakika.
 
Hao wanaomhukumu nao watahukumiwa, kwanini hawakutujuza haya mwaka jana⁉️
Haya ni ya miaka mingi sana hata kabla hajaanza intetnational ministry. Sio baada ya kufa
 
Unaelewa ukisema hakuna anayeweza kuthibitisha Mungu hayupo hujathibitusha Mungu yupo?

Unaelewa huu ulimwengu uliopo unaoruhusu mabaya unathibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo?
Kama Mungu hayupo hakuna kitu kinaitwa mabaya wala mema. Hakuna upendo wala kutokupenda na binadamu ni muundo wa kemikali tu. So hakuna swali wala jibu. That simple.

Huwezi kuthibitisha Mungu hayupo. Unaamini tu hivyo!
 
Nimekuwa nikifuatilia kifo cha gwiji huyu wa gospo tangu kilipotokea.

Jana nilishangaa hoja ambazo Jumuia ya makanisa ya kikristo ya Nigeria na Jumuia ya makanisa ya kipentekoste kumkataa kabisa TB Joshua kama Mkristo mwenzao.

Alipoulizwa sababu ya kumkataa, mwenyekiti mmoja wa jumuia hiyo aliwahi kusema.

TB hajawahi kubatizwa, au kuonyesha alimpokea Yesu lini na wapi na kwa pastor yupi. Hawakubaliani na agenda yake kuwa yeye Yesu alimalizana naye tangu akiwa tumboni mwa mama yake mimba ambayo ilikaa miezi 15.

Kwa kanuni za kikristo na Kibiblia mtu akiwa na akili timamu ndio anatakiwa amchague Yesu sio tumboni. Lakini pia kwa wengine akiwa mtoto hubatizwa. Lkn sio tumboni na angalau aonyeshe ushahidi wao hawatapata shida kabisa.

Huyu ndiye Gwiji wa injili aliyekuza sekta ya utalii nigeria kwa njia ya injili. Kuna mwaka ulifika ndege ikitua na wazungu 10 nigeria zaidi ya sita wote walikuwa wanaenda SCOAN kulamba upako.

Mkuu matunduizi habari.

Mkuu matunduizi jina lako linaweza kuwa linaongea mengi kuliko uliyosema umeyasikia.

Biblia katika Warumi 10: 9-10 inasema "Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu"

Pia Biblia inasema katika mathayo 28: 19-20 kwamba " Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati.”

Pia biblia inasema katika Marko 16: 15-16 kwamba " Basi, akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri Habari Njema kwa kila mtu. Anayeamini na kubatizwa ataokolewa. Asiyeamini atahukumiwa"

Hata bila kuingia ndani sana naomba kueleza kwamba mistari niliyoandika hapo inasisitiza kwamba:-

1. Kumpokea Yesu kama ni Bwana ni uamuzi binafsi ambao unaweza kuufanya ukiwa pekee yako au katika hadhara mfano kanisani au katika Crusades kama zinazoendelea wiki hii chini ya "Christ for All Nations - CFAN"

2.Ili kuukulia Wokovu unahitajika kuanza maisha ya uanafunzi wa Kristo kwa njia ya kusoma Biblia mwenyewe au kuwa chini ya kiongozi fulani wa kiroho mfano Mchungaji. Hili ni jambo lililowachukiza wachungaji wengi wa Nigeria kwavile T.B Joshua hakuwahi kuwa chini ya Mchungaji yeyote (Mentor) kama wao walivyokariri kwamba ni formula ya kiblilia ambayo hawajasema imeandikwa wapi?

3. Kubatiza kiblia i.e Immerse au kiswahili kuzika ni kitendo cha nje ambacho mtu mzima sio mtoto anaudhihirishia ulimwengu kwamba kwa kumpokea Yesu kama ni Bwana na Mwokozi wake amekufa katika dhambi na HIVYO BASi anaonyesha ishara ya kuuzika mwili wa DHAMBI kwa njia ya UBATIZO

Kwa uzoefu wangu wa kufuatilia mambo kiroho ya makanisa ya Nigeria, viongozi wengi wa kikristo wamekuwa na chuki binafsi na T.b Joshua kwa miaka mingi sasa. Wanachojaribu kukifanya ni kufuta "Legacy" aliyoiacha T.B Joshua.

Ahsante
 
Nimetoa mfano wa wegner ambae idea yake baada ya karne 1 ilithibitika ni kweli.

Mungu ni idea ambayo kwa sasa haina uthibitisho, hivyo kusema yupo au hayupo zote ni imani. Wewe unaposema Mungu hayupo hiyo ni imani yako, imani ambayo huwezi kuithibitisha kama hao unaosema wanadanganywa.
naona unapata shida sana kumwelezea mtu asiyetaka kuelewa

Muulize yeye alijiumba alivyokkuwa ndani ya tumbo la mama yake?
alijiwezesha kujitoa akawa mwanadamu akama alivyo hapo
ACHANA NA HUYO ASIYEKUBALI UKWELI WA MUNGU YUPO atakusumbua tu
 
Kama Mungu hayupo hakuna kitu kinaitwa mabaya wala mema. Hakuna upendo wala kutokupenda na binadamu ni muundo wa kemikali tu. So hakuna swali wala jibu. That simple.

Huwezi kuthibitisha Mungu hayupo. Unaamini tuhivyo!
Kama Mungu hayupo hakuna mabaya wala memq kwa mujibu wa nani?

Na unahakikishaje hilo?

Mbona hata mnaosema Mungu yupo hamkubaliani mabaya ni yapi na mazuri ni yapi.

Wengine wanaoa wake wanne, hilo ni zuri, wengine kuoa mke zaidi ya mmoja ni vibaya.

Unakubalije kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu unaoruhusu mabaya yanayoumiza viumbe wake?

Kama naweza kuthibitisha square root ya 2 si 10, kwa sababu 10 kuwa square root ya 2 kuna contradict kanuni kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, naweza kuthibitisha hivyo hivyo kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote ambaye kaumba ulimwengu huu unaoruhusu mqbaya hayupo, kwa sababu Mungu huyo kuumba ulimwengu unqoruhusu mabaya kunq contradict habari ya Mungu huyo kuwa na upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote.

Ukikubali uwepo wa Mungu huyo, kimsingi huna sababu ya kutokukubali kwamba 10 ni square root ya 2 katika base 10 math.

Habari zote ni za uongo na hilo linaoneshwa kwa contradiction.

Na proof kwamba habari hizi ni za uongo inawezekana.

Proof by contradiction.
 
Ukiingia kule kwa zumaridi hauwezi kusikia "tumsifu yesu kristo" ni mwiko kisema hivyo ,wao ni atukuzwe zumaridi so siwezi shangaa kwa Tb joshua.
 
Hizi dini uongo mtupu mwanzo mwisho.

Hakuna hata mmoja anayeweza kuthibitisha huyo Mungu yupo.
Tatizo sio dini bali ni wewe ambaye unalazimisha jambo mahali ambako si pake, yani unajua kwamba suala la kuwepo Mungu ni imani kwamba watu wanaamini hivyo ila wewe unataka upate ushahidi wa nje wa hiyo imani.
 
Imani ukiileta JF umeruhusu ihojiwe.

Kama unataka isihojiwe, baki nayo kanisani, msikitini etc kwako.

Motto ya JF hapo juu imeandikwa.

"Where We Dare To Talk Openly".

Wewe ndiye unalazimisha censorship mahali ambapo si pake.

Peleka censorship yako kanisani, msikitini etc.

Mpaka sasa hujathibitisha Mungu yupo.

Unaruhusiwa kuamini uongo wowote unaotaka, lakini ukiuleta uongo wako hapa tutasema huu ni uongo.
 
Si vyote visivyoweza kuthibitisha havipo.

Lakini wewe unajuaje hiki hakiwezi kuthibitishwa kwa sababu hakipo na hiki hakiwezi kuthibitishwa lakini kipo?

Mathalani, unajuaje Mungu yupo, hawezi kuthibitishwa tu?

Umeshawahi kufikiri kwamba pengine Mungu hawezi kuthibitishwa kwa sababu hayupo, ni hadithi za kutungwa na watu tu?

Siyo tu Mungu huyu hawezi kuthibitishwa kuwepo, bali pia uwepo wake unakuwa contradicted na hali halisi kwa namna ambayo inaonesha hayupo.

Unaambiwa Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Aliweza kuumba dunia isiyo na kifo, mabaya, magonjwa, etc.

Lakini hakuumba hiyo, akaumba hii ya ma pandemic na matetemekonya ardhi na ma tsunami.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote awe mkatili hivyo kwa viumbe wake?
Wewe umekaririshwa hiyo contradiction na kuhitimisha kuwa hakuna Mungu ila ukiambiwa ufafanue ni vp hiyo contradiction inahitimisha kuwa hakuna Mungu unaingia mitini.
 
Imani ukiileta JF umeruhusu ihojiwe.

Kama unataka isihojiwe, baki nayo kanisani, msikitini etc kwako.

Motto ya JF hapo juu imeandikwa.

"Where We Dare To Talk Openly".
Sijazungumzia kuhoji mbona kuhoji watu wanahoji sana mambo ya dini na hadi wanatofautiana masuala mbalimbali kutokana na uelewa, ila mimi nazungumzia suala la wewe kutaka uthibitisho kuwa Mungu kweli yupo nje ya imani yenyewe hapo ndio kwenye tatizo.
 
Sijazungumzia kuhoji mbona kuhoji watu wanahoji sana mambo ya dini na hadi wanatofautiana masuala mbalimbali kutokana na uelewa, ila mimi nazungumzia wewe kutaka uthibitisho kuwa Mungu kweli yupo nje ya imani yenyewe hapo ndio kwenye tatizo.
Kwani nikitaka uthibitisho sijahoji?

Halafu unataka nihoji uongo ndani ya uongo huohuo?
 
Matapeli huwa hawabatizwi.
Nimekuwa nikifuatilia kifo cha gwiji huyu wa gospo tangu kilipotokea.

Jana nilishangaa hoja ambazo Jumuia ya makanisa ya kikristo ya Nigeria na Jumuia ya makanisa ya kipentekoste kumkataa kabisa TB Joshua kama Mkristo mwenzao.

Alipoulizwa sababu ya kumkataa, mwenyekiti mmoja wa jumuia hiyo aliwahi kusema.

TB hajawahi kubatizwa, au kuonyesha alimpokea Yesu lini na wapi na kwa pastor yupi. Hawakubaliani na agenda yake kuwa yeye Yesu alimalizana naye tangu akiwa tumboni mwa mama yake mimba ambayo ilikaa miezi 15.

Kwa kanuni za kikristo na Kibiblia mtu akiwa na akili timamu ndio anatakiwa amchague Yesu sio tumboni. Lakini pia kwa wengine akiwa mtoto hubatizwa. Lkn sio tumboni na angalau aonyeshe ushahidi wao hawatapata shida kabisa.

Huyu ndiye Gwiji wa injili aliyekuza sekta ya utalii nigeria kwa njia ya injili. Kuna mwaka ulifika ndege ikitua na wazungu 10 nigeria zaidi ya sita wote walikuwa wanaenda SCOAN kulamba upako.
 
Wewe umekaririshwa hiyo contradiction na kuhitimisha kuwa hakuna Mungu ila ukiambiwa ufafanue ni vp hiyo contradiction inahitimisha kuwa hakuna Mungu unaingia mitini.
Neno la Mungu linasema hivi,Kama tukistahimili,tutamiliki pamoja naye;kama tukimkana yeye,yeye naye atatukana sisi.2Timotheo2:19,sasa huyo kwakuwa keshaamua kumkana Mungu asitegemee kumuona,atabakia kila siku kupinga kuwa hayupo ni kwakuwa alishakanwa siku nyingi...
 
Kwani nikitaka uthibitisho sijahoji?

Halafu unataka nihoji uongo ndani ya uongo huohuo?
Nazungumzia imani sizungumzii uongo labda kama kwa tafsiri yako wewe ni kwamba imani ni uongo.
 
Back
Top Bottom