Uchaguzi 2020 TBC kurusha live uzinduzi kampeni za CHADEMA leo Zakhiem

Uchaguzi 2020 TBC kurusha live uzinduzi kampeni za CHADEMA leo Zakhiem

Status
Not open for further replies.
Hao wana kwenda kuharibu kwa kufanya editing na kupiga picha sehemu walizo kaa watoto
 
Hii ndio picha ya Chadema sasa... Sio ile yenye rangi kama watu wako mpirani
 
Hata mimi nimewaza kama ulivyowaza wewe
Inawezekana hii ni geresha wanawaaminisha watu wakae majumbani kufuatilia kwenye tv halafu baadae wakate matangazo,lengo likiwa wahudhuriaji wa uzinduzi wawe wachache
 
wameanza kujirudi - TBC ambayo ni mali ya umma inapogeuka mali ya chama tawala!!
 
Watarusha lakini nina uhakika Lissu akianza kuongea tu watakata!!
 
Labda kama unazungumzia TBC ya inchi nyingine lakini sio hii tbccm ya bongo.
 
Wakuu nawasalimu wote,
Nimeona kwenye page ya tbc wakitoa taarifa kuwa watarusha mkutano mkubwa wa kihistoria uzinduzi wa kampeni jijini DSM

===

TBC1 leo tutakuwa mbashara katika uzinduzi wa kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka viwanja vya Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam.

Matangazo hayo yatakuwa mbashara pia kupitia tovuti (tbc.go.tz), App (TBC Live) na YouTube (TBCOnline).


View attachment 1550441
aa wapi!

watakata Tundu Lissu akishaanza kushusha nondo.....
 
TBC1 wako na weledi vichwani hawawezi kurusha kauli za kichochezi za tundu live
Uchochezi upi? Kuikosoa CCM siyo uchochezi na TBC wanalipwa mishahara kwa pesa za watanzania wote hawapaswi kubagua vyama vya upinzani
 
Duh! Sijaamini. Ngoja tuone muda ukifika kama hawata kata matangazo kwa matatizo yaliyo nje ya uwezo wao. Au kukata sauti.



Nb. Muandae mabango yenye sera zenu. Ili wakikata sauti muwe mnayapitisha mbele mbele hapo. Au lissu avae tisheti iliyoandikwa sera zake.
 
Inawezekana hii ni geresha wanawaaminisha watu wakae majumbani kufuatilia kwenye tv halafu baadae wakate matangazo,lengo likiwa wahudhuriaji wa uzinduzi wawe wachache
Uko sahihi kabisa. Wanapunguza watu uwanjani ili kati kati ya matangazo wakate steam
 
aa wapi!

watakata Tundu Lissu akishaanza kushusha nondo.....
Na hasa akiongelea chato Airport na ile mbuga ya kulazimishwa ambayo wanyama wote wameliwa na wanavijiji vya jirani wanaelekea kuisha na kuchukua fuso kwenda serengeti kubeba wengine kuwaleta humo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom