Uchaguzi 2020 TBC kurusha live uzinduzi kampeni za CHADEMA leo Zakhiem

Uchaguzi 2020 TBC kurusha live uzinduzi kampeni za CHADEMA leo Zakhiem

Status
Not open for further replies.
Duh! Sijaamini. Ngoja tuone muda ukifika kama hawata kata matangazo kwa matatizo yaliyo nje ya uwezo wao. Au kukata sauti.

Nb. Muandae mabango yenye sera zenu. Ili wakikata sauti muwe mnayapitisha mbele mbele hapo. Au lissu avae tisheti iliyoandikwa sera zake.
TBC ya kikwete ilikuwa na makada wa upinzani lakini TBC ya chato imejaa makada wa CCM watupu
 
Hawaaminiki hao.. Bora wananchi walio dar wakajazane uwanjani kusikiliza... Tegemea kukatwa katwa matangazo na kupotea kabisa hewani...
 
Wakuu nawasalimu wote,
Nimeona kwenye page ya tbc wakitoa taarifa kuwa watarusha mkutano mkubwa wa kihistoria uzinduzi wa kampeni jijini DSM

===

TBC1 leo tutakuwa mbashara katika uzinduzi wa kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka viwanja vya Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam.

Matangazo hayo yatakuwa mbashara pia kupitia tovuti (tbc.go.tz), App (TBC Live) na YouTube (TBCOnline).

View attachment 1550441
Hivi kweli hii imekua ikinifanya nitafakari sana, kwanini wamechukua muda sana kufanya hili, yani kuonyesha vyama vingine vya upinzani kampeni zao ilihali kituo hicho kinaendeshwa kwa pesa za walipa kodi, kituo cha tbc ni kituo cha umma
 
TBC ni chombo cha wote hutaki chadema walalamikie mapungufu yao?
TBC 1 wamesema watarusha matangazo ya mkutano wenu mubashara lakini mumeshaanza kulalamika kua huenda ni hujuma ili watu wasiende uwanjani.
 
Labda waurushie mawe si kuuonyesha amini nakwambia.
Acheni upumbavu. TBC ni chombo cha habari cha Serikali kinachofanya biashara kama vyombo vingine vya habari. Chama chochote cha siasa kikilipia gharama za matangazo lazima tu watarusha matangazo hayo. Hata CCM huwa wanalipia matangazo yao yote.
 
Tundu Lissu ajaribu kuongelea issues(maswala) pasipo kutaja jina la mtu, watu wataelewa tu kuwa ni nani alifanya hata kama hatamtaja mtu na baadaye aeleze wao watafanya nini kama watashinda uchaguzi. Kuna watu wana mahaba na mtu na wengine pengine wanafaidika naye hivyo wakisikia anakosolewa na kutajwa jina lake wanaweza kumchukia Lissu lakini akiongelea maswala(issues) hata hao wanaweza kuamua kusikiliza na pengine wanaweza baadaye kubadilika.
 
Wakuu nawasalimu wote,
Nimeona kwenye page ya tbc wakitoa taarifa kuwa watarusha mkutano mkubwa wa kihistoria uzinduzi wa kampeni jijini DSM

===

TBC1 leo tutakuwa mbashara katika uzinduzi wa kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka viwanja vya Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam.

Matangazo hayo yatakuwa mbashara pia kupitia tovuti (tbc.go.tz), App (TBC Live) na YouTube (TBCOnline).

View attachment 1550441
Au kituo cha tbc wamefanya hivi kwa minajiri ya kufanya biashara zaidi na kuongeza ushindani na kupata wafuasi wengi
 
Acheni upumbavu. TBC ni chombo cha habari cha Serikali kinachofanya biashara kama vyombo vingine vya habari. Chama chochote cha siasa kikilipia gharama za matangazo lazima tu watarusha matangazo hayo. Hata CCM huwa wanalipia matangazo yao yote.
mkuu usiniite mpumbavu maana mm ni mtanzania na ninajua mambo yanavyoenda kwa hiyo peleka upumbavu wako huko huko TBC.

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Kurusha sawa Ila Ile Tabia ya mitambo kukatakata ndo itakuwa kero,tuombe Mungu mitambo na hari ya hewa isiwe kikwazo watanzania Wana hamu yakusikia wasiyoyasikia kwa miaka Mitano,riport za cag, namna rushwa ilivyoshughurikiwa, namna Hali zawananchi zilivyo Sasa, uchumi wa nchi Deni la taifa tunataka kujua Kila mmoja anadaiwa shingapi, mwisho namuhimu kabisa tunataka kumsikia atatufanyia Nini sisi watanzania atatumia njia gani kutatua matatizo yetu sisi watanzania ambayo yameshindwa kutatuliwa na CCM kwa miaka 50 Sasa,, atawezaje kufanya elimu yetu iwe ya kujiajili, atawezaje kufanya kuwe na kilimo Cha biashara,atawezaje kupunguza mfumuko wabei nchini,atafanyaje kumaliza tatizo la afya Bora,maji,ajira, Kodi,kupunguza ukuaji wa Deni la taifa, rushwa, naatawezaje kuifanya iwe kituo chakibiashara kutokana na wingi wa bandari tulizonazo, aseme kwanini tunatumia gharama kubwa kuvuta umeme na maji wakati tunaripia gharama zakuutumia, aseme atafanyaje kupunguza tozo kubwa bandarini ,mwisho aseme tutawezaje kupata Kodi japo asilimia30 kwa madini yetu, aseme kwanini anaekopeshwa kusoma nimtoto wamasikini wakati uhakika wakulipa Hana tunatamani kusikia wasio nakipato wasome bure na wenye kipato ndio wakopeshwe elimu, namengine mengi maana dah!!!!
 
Wakuu nawasalimu wote,
Nimeona kwenye page ya tbc wakitoa taarifa kuwa watarusha mkutano mkubwa wa kihistoria uzinduzi wa kampeni jijini DSM

===

TBC1 leo tutakuwa mbashara katika uzinduzi wa kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka viwanja vya Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam.

Matangazo hayo yatakuwa mbashara pia kupitia tovuti (tbc.go.tz), App (TBC Live) na YouTube (TBCOnline).

View attachment 1550441
Thubutu mkuu,hii ni janja ya CCM kupunguza wananchi kwenda Zakheem,hawarushi hao ni propaganda tu na Jambo msilojua wanataka akianza lisu kumpiga mawe Meko wakatishe matangazo.
 
Weka mfano!
Mfano kusema serikali ndio ilimpiga risasi bila ushahidi wa mahakama au kusema tume wezi wa kura bila ushahidi wa mahakama au kusema CCM huwa wanaiba kura bila ushahidi wowote wa kesi ya wizi iliyowahi thibitishwa na mahakama yenye kutamka wazi kuwa CCM wezi wa kura au kutamka kuwa Magufuli hapendwi Wakati CCM kwenye uteuzi alipata kura asilimia 100 nk kifupi kusema hovyo Ni kuongea vitu visivyo na ushahidi wa kisheria kimahakama vya kushambulia wengine hapo usitarajie mtangazaji akuache Live lazima akuzimie maiki
 
Hivi D.r Rioba kazi bado anaitaka au kaichoka!!!
 
Lissu akianza kuongea tu mitambo itakatika kutokana na sababu silizo nje ya uwezo wao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom