TULIWAAMBIA MKIFUATA UTARATIBU MTAKUWA LIVE
Acheni kudekadeka mnaongoza kwa kudeka duniani. Sasa muongee point mnaongea katika television ya Taifa muonyeshe utaifa na uzalendo
Sasa MTAKUWA MUBASHARA mutumie airtime kuwaambia watanzania mambo ya maana sio kutafuta kiki mje na agenda kiki hazitusaidii sisi wapiga kura tunataka kusikia usalama na ulinzi wa nchi amani kwanza, tunataka kusikia Muungano wetu mnaudumisha, tunataka kusikia Mnakubali kuwa CCM awamu hii imefanya mambo makubwa sana nchini ya kuenziwa na DR. JOHN POMBE Magufuli mtaongoza mijadala ya kumuongezea muda kwa jinsi ameweza kuwa Nyerere wa sasa??
Kumbukeni wakati tuna asisi vyama vya Upinzani nchini mwaka 1992 lengo kubwa lilikuwa ni
kupata mawazo mbadala sio kukimbilia Ikulu. Ikulu ni mahali patakatifu ndio maana kuna wameenda tukatamani muda ukatike na kuna wameenda hasa Dr. John Pombe Magufuli watanzania mitano tena tunaona haitoshi tunahitaji aongezewe muda ili pia kama nchi tutulie na kujifunza siasa za makundi yaliokuwa yanataka Ikulu yetu halikuwa jambo jema na kuelimishana upya Ikulu sio mahali pakukimbilia.
Hivyo mubashara wa kuongea na dunia muiambie dunia tuko na Dr. John Pombe Magufuli kiboko cha mafisadi wa rasimali wa ndani na nje, Mwalimu wa nidhamu kwa watumishi wa umma, Mwanamapinduzi adimu na adhimu wa kuweza kutumia rasilimali za nchi kwa maendeleo ya Wananchi.
Muwape salamu tutapunguza utegemezi na kuwakaribisha Tanzania kununua Tanzanite na madini na muwaambie treni ya umeme soon itaanza kazi waje kupanda sio ziko kwao tu ila muwajuze sasa watanzania wanalipa kodi.
Waambie Ndoto kubwa mwananchi wa kawaida anzia Jana na Leo amekosa ticket ubungo hata za Mabasi ya Champion na Kamwana kwenda Dodoma ufunguzi wa Kampeni za Rais wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli.
Haijapata tokea kwenda kwa ajili ya kufungua kampeni za Mhe Rais usafiri ukakosekana.
Waambie hata ninyi sasa mnakaaa na kunyosha mikono mikono sasa mnafanya siasa za mawazo mbadala sio za Ikulu ni mahali patakatifu na maisha ni kazi haiwezekani kuwa ni kuwaza kwenda Ikulu Ikulu.
Na,
Mwl. Cleopa E. Soi
Ndoto Kubwa