Uchaguzi 2020 TBC kurusha live uzinduzi kampeni za CHADEMA leo Zakhiem

Uchaguzi 2020 TBC kurusha live uzinduzi kampeni za CHADEMA leo Zakhiem

Status
Not open for further replies.
Kama hizi ni taarifa za kweli basi muda wa Dr Ayoub Ryoba kuwa mkurugenzi wa TBC unafikia tamati.

Jamaa ajiandae kurudi kufundisha vyuoni, lazima atatolewa hapo.
Kweli CCM mmeliharibu hili taifa!!! Mnaongea haya kwa uwazi kabisa mchana kweupe huku TBC ikiwa inaendeshwa kwa kodi za watanzania wote??? Kosa la Dr Lyoba ni nini??
 
Wakithubutu yale yalofanywa na bashite klauz TV kuivamia akiwa na A.K 47 kipindi hiki atakuja nyangogo akiwa na rocket ranger tena yeye mwenyewe huku akimwaga ung'eng'e wa gambosi " Bhebhesi nang'ho nawawilaga ndoho kutangaja i kampeni ya wangi than that of unene ntale mbumbazu

Aisee!
 
Kuna Askofu mmoja mahiri ambaye hashikiwi akili na mtu anatumia upeo na akili yake kutoa maoni alipata kuandika kwamba
Hii miezi miwili ya kampeni ndio wakati wa wale waliofungiwa kufanya siasa wafanye siasa haswa haswa kuongea waliyofungiwa kwa miaka 5 walionyimwa haki hii

Ntashangaa sana hata hii miezi miwili nayo wakianza kubaniwa baniwa
Maana ikiwa jpm atashinda hawatafanya tena siasa hadi miaka 5 ipite
 
Inawezekana hii ni geresha wanawaaminisha watu wakae majumbani kufuatilia kwenye tv halafu baadae wakate matangazo,lengo likiwa wahudhuriaji wa uzinduzi wawe wachache
Una akili sana wewe!Una Masters?
 
Na ikiwa kweli watarusha basi itakuwa na delay kama ya dk 5 hadi 10 ili kuedit nondo zote zitakazo kua na muelekeo wa kuisambaratisha ccm
 
Du vinega hamkosi kukosoa kila jambo kwenu sio jema
 
Wakuu nawasalimu wote,
Nimeona kwenye page ya tbc wakitoa taarifa kuwa watarusha mkutano mkubwa wa kihistoria uzinduzi wa kampeni jijini DSM

===

TBC1 leo tutakuwa mbashara katika uzinduzi wa kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka viwanja vya Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam.

Matangazo hayo yatakuwa mbashara pia kupitia tovuti (tbc.go.tz), App (TBC Live) na YouTube (TBCOnline).


View attachment 1550441
Fake news hiyo
 
Wakuu nawasalimu wote,
Nimeona kwenye page ya tbc wakitoa taarifa kuwa watarusha mkutano mkubwa wa kihistoria uzinduzi wa kampeni jijini DSM

===

TBC1 leo tutakuwa mbashara katika uzinduzi wa kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka viwanja vya Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam.

Matangazo hayo yatakuwa mbashara pia kupitia tovuti (tbc.go.tz), App (TBC Live) na YouTube (TBCOnline).


View attachment 1550441
Wanaogopa kupigwa mawe kesho watakaporusha uzinduzi wa fisiemu. Ni full kupumbaza watu.
 
TULIWAAMBIA MKIFUATA UTARATIBU MTAKUWA LIVE

Acheni kudekadeka mnaongoza kwa kudeka duniani. Sasa muongee point mnaongea katika television ya Taifa muonyeshe utaifa na uzalendo

Sasa MTAKUWA MUBASHARA mutumie airtime kuwaambia watanzania mambo ya maana sio kutafuta kiki mje na agenda kiki hazitusaidii sisi wapiga kura tunataka kusikia usalama na ulinzi wa nchi amani kwanza, tunataka kusikia Muungano wetu mnaudumisha, tunataka kusikia Mnakubali kuwa CCM awamu hii imefanya mambo makubwa sana nchini ya kuenziwa na DR. JOHN POMBE Magufuli mtaongoza mijadala ya kumuongezea muda kwa jinsi ameweza kuwa Nyerere wa sasa??

Kumbukeni wakati tuna asisi vyama vya Upinzani nchini mwaka 1992 lengo kubwa lilikuwa ni kupata mawazo mbadala sio kukimbilia Ikulu. Ikulu ni mahali patakatifu ndio maana kuna wameenda tukatamani muda ukatike na kuna wameenda hasa Dr. John Pombe Magufuli watanzania mitano tena tunaona haitoshi tunahitaji aongezewe muda ili pia kama nchi tutulie na kujifunza siasa za makundi yaliokuwa yanataka Ikulu yetu halikuwa jambo jema na kuelimishana upya Ikulu sio mahali pakukimbilia.

Hivyo mubashara wa kuongea na dunia muiambie dunia tuko na Dr. John Pombe Magufuli kiboko cha mafisadi wa rasimali wa ndani na nje, Mwalimu wa nidhamu kwa watumishi wa umma, Mwanamapinduzi adimu na adhimu wa kuweza kutumia rasilimali za nchi kwa maendeleo ya Wananchi.

Muwape salamu tutapunguza utegemezi na kuwakaribisha Tanzania kununua Tanzanite na madini na muwaambie treni ya umeme soon itaanza kazi waje kupanda sio ziko kwao tu ila muwajuze sasa watanzania wanalipa kodi.

Waambie Ndoto kubwa mwananchi wa kawaida anzia Jana na Leo amekosa ticket ubungo hata za Mabasi ya Champion na Kamwana kwenda Dodoma ufunguzi wa Kampeni za Rais wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli.

Haijapata tokea kwenda kwa ajili ya kufungua kampeni za Mhe Rais usafiri ukakosekana.

Waambie hata ninyi sasa mnakaaa na kunyosha mikono mikono sasa mnafanya siasa za mawazo mbadala sio za Ikulu ni mahali patakatifu na maisha ni kazi haiwezekani kuwa ni kuwaza kwenda Ikulu Ikulu.

Na,
Mwl. Cleopa E. Soi

Ndoto Kubwa
 
Kisa TBC inarusha live Basi mnataka kuwapangia Cha kuongea, kwanza Chadema walishajiandaa kisaikolojia kupiga kampeni bila tv.
Au labda wakuu wameishiwa bundle za kuwa wanaingia Whatsapp kuwafiatilia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom