TBC ni TV ya waislam na wakristo wakatoliki?

TBC ni TV ya waislam na wakristo wakatoliki?

Tusome wakiyapa air time madhebu yote Kuanzia walokole mpaka ma budda itachukua muda gani,kutakua na taarifa ya habari kweli na ziara mbalimbali za kiserikali zinazorushwaga mubashara?
Kila Dhehebu na siku yake.
 
Wewe ni mjinga,hatuachi kukuelewesha,kwa nini Mali ya umma itumike kuhubiri dini mbili tu,mbona wahindi,wapagani dini zao hazitangazwi kwenye vyombo vya umma
Mchungaji wako ndio kakutuma useme hivyo?
 
Siwezi kulalamika maana alishawahi kufuatilia mtu akaambiwa nafasi hata kwa wasabato ilikuwaga ipo Jumamosi sema viongozi na watu wa kufuatilia ndio walikuwa butu. Sijui siku hizi.
 
Binafsi kuna jambo sielewi kuhusu hii television ya umma/taifa- TBC

Hii ni television ya kutangaza dini ya Uislam na Ukristo kupitia ukatoliki au ni television ya umma isiyo na mafungano na dini yoyote ?

Nashindwa kuelewa kwamba hawa waislam na wakatoliki wamelipa pesa ili dini zao zitangazwe kupitia television ya umma au ni tabia ya kijinga tu ya uongozi wa TBC na serikali kulifungamanisha hili taifa na hizi dini mbili Uislam na Ukristo ?

Binafsi naomba kupewa muongozo ni nini kipo nyuma kwa TBC kwa utaratibu huu wa miaka nenda rudi kwa television ya umma kutangaza dini hizi mbili Uislam na Ukristo huku ikitambuliwa kama television ya umma wote ?

Na hawa waislam na wakristo kwani wao wenyewe hawana television zao binafsi za kurusha maudhui yao huko na sio kwenye television ya umma ?
Jamaa una moyo, tbc nayo ni tv?
 
Ni dini mbili kubwa.
Nyingine ni copy tu na za mchongo.
 
Binafsi kuna jambo sielewi kuhusu hii television ya umma/taifa- TBC

Hii ni television ya kutangaza dini ya Uislam na Ukristo kupitia ukatoliki au ni television ya umma isiyo na mafungano na dini yoyote ?

Nashindwa kuelewa kwamba hawa waislam na wakatoliki wamelipa pesa ili dini zao zitangazwe kupitia television ya umma au ni tabia ya kijinga tu ya uongozi wa TBC na serikali kulifungamanisha hili taifa na hizi dini mbili Uislam na Ukristo ?

Binafsi naomba kupewa muongozo ni nini kipo nyuma kwa TBC kwa utaratibu huu wa miaka nenda rudi kwa television ya umma kutangaza dini hizi mbili Uislam na Ukristo huku ikitambuliwa kama television ya umma wote ?

Na hawa waislam na wakristo kwani wao wenyewe hawana television zao binafsi za kurusha maudhui yao huko na sio kwenye television ya umma ?
Waislamu na wakatoliki ni sehemu ya umma, shida iko wapi kwani
 
kesho utasema na wasanii wanapaswa kutumia platform zao, keshokutwa utasema walemavu na wenye mahitaji maalumu watumie platform zao pia, kwasabb hii ni Tv ya Taifa....

Hutaishia hapo bado utasema wavuvi, wafugaji na wakulima wasaitumie TV ya taifa kutangaza mipango yao ya kilimo watumie platform zao kufanya mambo yao....

Ukiona wasanii na kazi zao utasema hao nao watafute platform yao hii ni Tv ya Taifa.

Hutaishia hapo utakuja kusema tena wanasiasa wasitumia Tv ya Taifa watumie platform zao huko mtaani....

Baadae utasema watu weusi na weupe kila moja atafute platform zao maana hii ni Tv ya Taifa.....

Ubaguzi hautaishia hapo ntaendelea baada ya muda kidogo...
Hakika
 
Back
Top Bottom