Uchaguzi 2020 TBC, sasa tumewachoka kwelikweli, mnachochea hasira kubwa msiyoweza kuizima

Uchaguzi 2020 TBC, sasa tumewachoka kwelikweli, mnachochea hasira kubwa msiyoweza kuizima

share

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2008
Posts
6,064
Reaction score
10,468
Matangazo ya TBC hususani kampeni za Uchaguzi Mkuu ni utopolo mtupu uliokosa weledi na busara za kiutangazaji kama chombo cha umma kinachogharamiwa na kodi za wananchi wote.

Tumevumilia sana, sasa tumechoka. Ni ujinga, hata kama mnalazimishwa, kuitangaza CCM pekee na Wagombea wake kuanzia Asubuhi mpaka jioni kana kwamba ndiyo chama pekee.

Hili limezua hasira kuu, chuki mbaya, na kimsingi badala ya kuieneza CCM mmeiua kabisa CCM kwenye mioyo ya wananchi. Badilikeni haraka, la sivyo, mnachokitafuta, kwa ujinga wenu, mtakipata.
 
Yaani kuanzia Asubuhi hadi jioni ni CCM tu. Vipindi vingi wanavyoviandaa ni lazima vihusiane na mambo ya Chama. Yaani imekuwa ni kama TV ya Chama. Chombo cha umma kilipaswa kiwe Neutral na kiwe kwa manufaa ya watu wa vyama vyote.
 
Ungeeleza with e.g.
 
Sasa wewe hutaki watupandishe hasira! Waache watuongezee chuki ila wakawaulize Malawi Broadcasting Corporation waliokifanya inachofanya TBC na kilichowakuta baada ya uchaguzi.
Ilikuwaje mkuu am curious to know
 
Mimi sio mfuatiliaji wa vipindi vya t.v. lakini ninachojua tbc wana vipindi vingi sana vinavyohusu maswala ya maendeleo ya nchi, vikielezea miradi tofauti katika sekta tofauti tofauti, changamoto na mabadiliko chanya katika jamii.

Ila sababu hivyo vyote vimefanyika chini ya serikali ya chama kilichopo madarakani wapinzani wanaona kama ni kampeni huku wakisahau wananchi wana haki ya kuhabarishwa maendeleo yao
 
Back
Top Bottom