Uchaguzi 2020 TBC, sasa tumewachoka kwelikweli, mnachochea hasira kubwa msiyoweza kuizima

Uchaguzi 2020 TBC, sasa tumewachoka kwelikweli, mnachochea hasira kubwa msiyoweza kuizima

Mimi sio mfuatiliaji wa vipindi vya t.v. lakini ninachojua tbc wana vipindi vingi sana vinavyohusu maswala ya maendeleo ya nchi, vikielezea miradi tofauti katika sekta tofauti tofauti, changamoto na mabadiko chanya katika jamii.
Ila sababu hivyo vyote vimefanyika chini ya serikali ya chama kilichopo madarakani wapinzani wanaona kama ni kampeni huku wakisahau wananchi wana haki ya kuhabarishwa maendeleo yao
Of course wananchi wanatakiwa wapate Habari za maendeleo na pia wapate Habari za ubaya na dhulma inayofanywa na serikali
Shilling inatakiwa ionyeshwe pande mbili
 
Naichukia TBC! Huwa nawaangalia wale watangazaji najiuliza na suti zao na tai hizi hivi hawaoni aibu kweli! Hawajiskii vibaya hata kidogo! Yani TBC wanafanya mambo ya kinyaa kabisa
 
Maajabu haya utayapata bongo tu, katibu muenezi kupewa airtime na chombo cha taifa, Mali ya umma kutoa matusi kwa vyama pinzani, ni aibu kubwa sana kuzidi hata kidhungu alichotema juzi yule bwana
 
Of course wananchi wanatakiwa wapate Habari za maendeleo na pia wapate Habari za ubaya na dhulma inayofanywa na serikali
Shilling inatakiwa ionyeshwe pande mbili
Ndio maana nimesema changamoto na mafanikio
Mimi sio mfuatiliaji wa vipindi vya t.v. lakini ninachojua tbc wana vipindi vingi sana vinavyohusu maswala ya maendeleo ya nchi, vikielezea miradi tofauti katika sekta tofauti tofauti, changamoto na mabadiko chanya katika jamii.
Ila sababu hivyo vyote vimefanyika chini ya serikali ya chama kilichopo madarakani wapinzani wanaona kama ni kampeni huku wakisahau wananchi wana haki ya kuhabarishwa maendeleo yao
 
Wengine bado tunaipenda
Mkuu.. uwe tu mkweli! TBC1 Haikukifu?!! Kuna vyama 17 vitashiriki uchaguzi mkuu Oktoba, kutwa nzima kila siku uwe unaoneshwa maudhui ya chama kimoja tu tena mada za kujirudiarudia kama miradi mikubwa inayojengwa kila siku!

Ni kweli hutamani kuona hata Rungwe sera yake ya Ubwabwa anaitetea vipi? Hutaki kuona wenye sera ya 'uhuru haki na maendeleo' wanaitetea vipi? Huchoki kuona sare za kijani kila siku kwa runinga? Hujisikii vibaya chama kimoja tu kupewa "airtime" na tv ya taifa hata kama hao wengine hawana uwezo wa kulipia matangazo?
 
Sasa wewe hutaki watupandishe hasira! Waache watuongezee chuki ila wakawaulize Malawi Broadcasting Corporation waliokifanya inachofanya TBC na kilichowakuta baada ya uchaguzi.
😂😂😂 Eti hasira.
 
Ndio maana nimesema changamoto na mafanikio

Changamoto ni challenges
Tunataka tuone ufisadi uliopo kama vile kubomoa nyumba bila malipo
Hela za rambirambi za wahanga wa majanga mbalimbali
Watu wanauwawa na wasiojulikana
Kandarasi zote kupewa mume mwenza bila kutangaza zabuni huku makampuni mengine yakifilisika
Makampuni na wawekezaji wanaondoka baada ya kushindwa kufanya Kazi
Wakullma wa korosho wakopwa mazao bei chini mpaka Leo bado hawajalipwa
Wakullma wa mpunga na mahindi mazao Yao yamedoda
Hazina ya Tanzania ipo mikinoni mwa mtoto wa dadake rais
Mkaguzi wa mahesabu asema zaidi ya dola billion moja imepotelea ikulu bila kujulikana ikwapi
Rais anajimilikisha hekta 25000 na inalindwa na jeshi etc etc
Kuna uvundo mwingi Sana katika serikali hii Ndio maana kitu cha kwanza alichofanya ni kubana media
Kwa Mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu hatuwezi kusikia
BBC, VOA, DW wala Radio Japan
Why why why???
Mbona nchi zingine wanapata habari???
 
Matangazo ya TBC hususani kampeni za Uchaguzi Mkuu ni utopolo mtupu uliokosa weledi na busara za kiutangazaji kama chombo cha umma kinachogharamiwa na kodi za wananchi wote.

Tumevumilia sana, sasa tumechoka. Ni ujinga, hata kama mnalazimishwa, kuitangaza CCM pekee na Wagombea wake kuanzia Asubuhi mpaka jioni kana kwamba ndiyo chama pekee.

Hili limezua hasira kuu, chuki mbaya, na kimsingi badala ya kuieneza CCM mmeiua kabisa CCM kwenye mioyo ya wananchi. Badilikeni haraka, la sivyo, mnachokitafuta, kwa ujinga wenu, mtakipata.
Hii channel nina miaka 3 sijawahi kuitazama...

........Nishasema kupata wazo kichwani mwangu eti niwashe TV na kutune TBC heri hata nikanunue box la viberiti nikae nianze kuhesabu njiti kamoja kamoja mpaka viishe.
 
Mliwafukuza mlizani.mmefukuza chuma sio binadamu?
Rudini kwenye jukwaa kisha muwaombe msamaha kama mlivyowafukuza.
Nyie si ni wazee wa kutetea haki ya habali mnaogopa nini?
Fungueni midomi yenu kwa akiri kabla ya kukwaza watu.

Matangazo ya TBC hususani kampeni za Uchaguzi Mkuu ni utopolo mtupu uliokosa weledi na busara za kiutangazaji kama chombo cha umma kinachogharamiwa na kodi za wananchi wote.

Tumevumilia sana, sasa tumechoka. Ni ujinga, hata kama mnalazimishwa, kuitangaza CCM pekee na Wagombea wake kuanzia Asubuhi mpaka jioni kana kwamba ndiyo chama pekee.

Hili limezua hasira kuu, chuki mbaya, na kimsingi badala ya kuieneza CCM mmeiua kabisa CCM kwenye mioyo ya wananchi. Badilikeni haraka, la sivyo, mnachokitafuta, kwa ujinga wenu, mtakipata.
 
Mkiambiwa kuhusu katiba mpya yenye lengo la kupunguza mamlaka ya rais, hamuelewi. Hata ungekuwa wewe mleta mada ndio MD pale TBC, umeteuliwa na mgombea wa CCM, ungempigia debe mgombea wa CHAUMA kweli?
 
Walikimbia bunge la katiba mpya waliojiona wajanja
 
Back
Top Bottom