Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Nili.tune kwa bahati mbaya TBC, wife fasta akanambia nitoe, niweke hata channel ya kihindi! Nimekoma.
Dah Mpwa huyo ndio material wife, natoa rai ukaongeze mahari hapo ndio kuna Value for Money! Congratulations
 
Tatizo wanalikwepa wakati wanalijua.

Yaah, uko sahihi kabisa. Nadhan kama kweli kikao kinafanyika kutathimini hilo inakuwa ni kupoteza muda maana ttz linajulikana. Kama kuna nia ya dhati ya kukirejesha katika kiwango kizuri ilitakiwa kufanya uamuzi wa kubadili mtazamo tu na siyo kikao cha kujiuliza ttz ni nini. Mkakati wa Tido Mhando wa kukifanya kiwe kituo cha TV cha kiwango cha kimataifa ulikuwa unaenda vizuri sana. Lakini ndiyo hivyo tena
 
TBC waache Siasa wafanye kazi kama BBC.Waache kutumika kama chombo cha propaganda cha CCM.Hiyo kazi wawachie Redio uhuru.Hakuna mchawi ni wao wenyewe.Kutwa mzima CCM CCM,nani atapoteza muda kuangalia?
Nawashangaa sana. TBC inaendeshwa na kodi za wana chadema, wana ccm ,nccr,act na ambao hata hawana vyama lakini wao wanafanya kazi unadhani tawi la CCM. Nani aangalie huo uchafu. Watasubiri sana.
 
Hiyo ni laana ya Tido Mhando kwa kumdhalilisha kwani alikuwa kafanya jitihada mpaka TBC ilikuwa inaelekea International sasa wapi Wamezidiwa na TvE ya juzi tu
 
Walijitakia wenyewe kushuka chini siku walipomtimua Tido na kukubali kuwa TBCCCM
 
Hawajajiliza kwanini magezeti ya uhuru ,na radio Uhuru imekufa?
 
Waweke vipindi vyenye mvuto vya kuvutia rika lote...Sio kila mda wanaweka Tanesco inaangaza,mara jenga na TBA...
 
TBC inazidiwa na TVE ambayo bado iko kwenye majaribio ..at least Tido Muhando alikuwa anakibadilisha ila kwa kuwa hakufanya kinachowapendeza wakubwa basi wakamuwekea figisu figisu kama kawaida yao..
 
TBC hata wamiliki wake wenyewe huwa hawaipendi.
Embu fikiria haya, kama..
1/Kama Rais na mke wake wakiwa Ikulu huwa hawaangalii TBC, nani tena aangalie?
2/Waziri Mkuu huwa hataki kuangalia TBC, nani tena aangalie?
3/Kama makada wa CCM hawataki kabisa kuangalia TBC, nani tena aangalie?

Hata kwa kulazimishwa, hakuna mtu ataangalia TBC. Kile kituo kinapaswa kufungwa kabisa, inatumia pesa za walipa kodi bure.
Kwahiyo hao uliowataja ndio wamiliki wa TBC ?
 
Wanataka kujua matatizo, mie naanza na haya na wengine wataendeleza
1.Quality ya picha ni mbovu
2. Hakuna ubunifu wa vipindi
3. Coverage ya habari ni poor
4. Upendeleo katika kuripoti habari
Wakitaka tuangalie wawe wanaripoti na habari za ukawa,
 
Mpaka Leo sijamuambia mwanangu kama tbc ndio Taasis ya utangazaji ya Tanzania... Na bado sijamuambia kwamba Tanzania ndio nchi yetu kwa huu upuuzi wao
 
Tatizo lipo wazi, hii sio TV ya serikali (wananchi) tena, imekuwa ni ya chama dola, kutangaza habari zinazopendwa na wakuu tu, haiwezi kuwa positive tu ndio inatangazwa lakini negative hatupati. Wabadilike
 
Uonngozi wa juu wa TBC na wafanyakazi wengine wa kituo hicho usiku wa kuamkia leo wamefanya kikao cha dharura kuangalia sababu za kudorora kwa kituo hicho kikubwa cha TV ambacho kimemalizika saa 11 alfajiri.

Pamoja na mengine kitu kilichoonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni jinsi gani kituo kikubwa kama hicho kinachopata ruzuku kubwa kutoka serikalini kinakuwa na ratings za mwisho huku kikizidiwa na vituo ambavyo havina hata miaka mitano hewani.

Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC.
Siku Ryoba akitambua kuwa wananchi hawapendi ulaghai, uzandiki, uccm na umagufool-gufool hatalazimika kufanya vikao usiku badala ya kulala...Hatupendagi Ujinga sisi!
 
Naombeni msaada jinsi ya kuitoa kwenye kisambusi changu..inatia kinyaa
 
Back
Top Bottom