Masikini Television na Redio ya Taifa:.
Tuna kila sababu ya kumkumbuka Rais aliyetawala kwa kufuata taratibu na misingi ya utawala bora, Licha ya madhaifu machache kama binadamu.
Ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika mambo makubwa juu ya vyombo vya habari na kituo cha habari cha taifa.
Lakini leo tunae anaemini katika utawala wa upendeleo. Na anaeamini kuinua chombo kimoja cha mtu binafisi cha habari.
Huku akidhorotesha vyombo vingine binafisi vya habari na hata kituo cha habari cha taifa.
Na angali akijua, kuwa vyombo vyote vya watu binafisi ni sawa, na ni sawa kabisa katika ushindani. Na vyote vinawajibika katika kodi na pato la taifa kwa ujumla.
Na ndio maana tukawa na chombo cha Taifa ili kuleta usawa kwa wadau wote wa habari.
Au ndio mkakati wa kupunguza gharama za TBC?
Kwa upande wangu nasikitika , Na ni ishara mbaya kwa maendeleo ya taasisi yetu ya vyombo vya habari.
Huu mwenendo si sahihi hata kidogo, kwa kuamini kuwa JPM ni rais wa watu wote na si kundi la watu fulani.
Hivyo basi aisimamie TBC ili kuwaunganisha watanzania wote. Kujiona wako sawa katika taifa lao na juu ya biashara wanazozifanya hususani upande wa habari.
Mungu ibariki Tanzania.