Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Walianzisha bango wakati wa kikwete ilianza kupendwa ila alipokuja Faru John watu wote wamekimbia.
 
teh teh teh kanafanana na tv 1 kule zenj kanaitwa zbc sijiu nayo kama ingaliko maana kwa mara ya mwisho niliiona mwaka 94
 
HUYU MKURUGENZI MPYA KIJANA SIJUI ANAKWAMIA WAPI?...
-->>AONDOE BIASIMENT
-->>PROGRAM ZA VIPINDI TVs,RADIO WAVIPANGILIE UPYA...
-->>WAITE DAMU CHANGA, ZENYE UBUNIFU KAMA GERALD HANDO.
-->>VIPINDI VYAO VILENGE KUNDI LA VIJANA WALIOWENGI KWA SASA...
-->>WAIBE WAFANYAKAZI MAHIRI KUTOKA VITUO VINGINE...
Mbn hawataweza hata wafanye hayo mchawi siasa za upendeleo, kutetea uovu
 
Yaani tendo la kuondoa Bunge live ndio ilikuwa kuizika rasmi TBC. Hata waandishi na watangazaji nguli waluobaki TBC ni kwa kuwa wanategemea iko siku Rais atawakumbuka kwa nafasi za UDC/RC.

Vv
Wengine kama akina Shaaban Kisu ambaye aliwahi kuteuliwa kuwa DC unatarajia azungumze ukweli CCM ikivurunda? Huwezi choma nyumba ambayo ndani yake ndimo unaishi.
 
Wakitaka Wajiweke Kitaifa Zaidi. Warudishe Bunge Mubashara. Halafu Waajiri Damu Changa Na Wasijifanye Wana Maadili Sana
 
Clouds nao wajipime mwelekeo wanaelekea kwenye ukada. Sijui sasa hivi wanaweza kutoa coverage ya wapinzani sijui
 
Yan ktk televesion ambazo siwezi kuziangalia ni TBC na Star tv. Tangia wamtoe Tido Mhando wamepotea kabisa. Wanaleta siasa kwenye mambo ya muhimu.Hata ukipita mtaani utaona watu wanaangalia azam na ITV channels tu.
 
Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC.

Hahaaaaaaaaaaaaaa ! Hawajajua mpaka sasa mchawi wao ni nani?.
Kumbe hadi Raisi salamu na simu anapiga TV zingine?
 
Masikini Television na Redio ya Taifa:.

Tuna kila sababu ya kumkumbuka Rais aliyetawala kwa kufuata taratibu na misingi ya utawala bora, Licha ya madhaifu machache kama binadamu.
Ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika mambo makubwa juu ya vyombo vya habari na kituo cha habari cha taifa.

Lakini leo tunae anaemini katika utawala wa upendeleo. Na anaeamini kuinua chombo kimoja cha mtu binafisi cha habari.

Huku akidhorotesha vyombo vingine binafisi vya habari na hata kituo cha habari cha taifa.

Na angali akijua, kuwa vyombo vyote vya watu binafisi ni sawa, na ni sawa kabisa katika ushindani. Na vyote vinawajibika katika kodi na pato la taifa kwa ujumla.

Na ndio maana tukawa na chombo cha Taifa ili kuleta usawa kwa wadau wote wa habari.

Au ndio mkakati wa kupunguza gharama za TBC?

Kwa upande wangu nasikitika , Na ni ishara mbaya kwa maendeleo ya taasisi yetu ya vyombo vya habari.

Huu mwenendo si sahihi hata kidogo, kwa kuamini kuwa JPM ni rais wa watu wote na si kundi la watu fulani.

Hivyo basi aisimamie TBC ili kuwaunganisha watanzania wote. Kujiona wako sawa katika taifa lao na juu ya biashara wanazozifanya hususani upande wa habari.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Kwa hali hii nani atataka kuangalia TBC?Hata makada pia wanapenda kusikia na habari za upande wa pili!
Cheki video hii halafu uulize kama kuna haja ya kufanya vikao mpaka asubuhi!
 
Back
Top Bottom