Wewe ni NP katika Id tofauti, unaambiwa watu wamekaa hadi usiku Wa manane wanajadili kudorora kwa ufanisi Wa chombo hiki cha wananchi. Wanatafuta sababu za kwa nini watazamaji hawakithamini kama vyombo vingine wewe unakuja na ngonjera ya "wana OB van ya kisasa"? Ama kweli nyie wapigania 'UHURU" wa siku hizi ni vipofu. Na wewe Unadhani kwa maneno hayo umetoa mchango murua Wa kuboresha TV ya Taifa.? Hili liko wazi TV ya wananchi haipendwi na wananchi, ni wajibu Wa waliopewa dhamana ya kuisimamia kujiuliza kwa nini watu hawapendi chao. Tutoke na ushauri Wa kuwapa ili kurekebisha hii hali maana ni wazi kama TV hii isingekuwa inapata Ruzuku ikategemea mapato yake kujiendesha ingeshafungwa miaka 3 iliyopita. Baada ya Tido aliyeletwa kuondolewa ubunifu ulikosekana. Waliowashauri Viongozi wetu kumwondoa Tido kwa sababu za kisiasa hawakuangalia faida ya kibiashara na kimvuto waliyokuwa wanaipoteza kwa kumwondoa Mr. TM. Chombo cha habari kitavutia matangazo yanayokiingizia faida kwa kuwa kinapata watazamaji wengi, na kitapata watazamaji wengi pale tu kitakapokidhi matakwa na mapenzi ya watu wenye mitazamo tofauti. Kutangaza kwa kuremba habari za upande mmoja na wakati mwingine watazamaji wakiona wazi zinapotoshwa kwa masililahi ya upande huo ambayo obviously siyo maslahi ya taifa per se,kunawaondoa na kuwapoteza watazamaji makini hata Wa upande huo. Katika ulimwengu Wa sasa Wa utandawazi ambapo taarifa husafirishwa kwa njia mbalimbali si rahisi kuwadanganya watu. TBC angalieni mlipojikwaa msiangalie mlipoangukia, tafuteni kilichorudisha imani ya watazamaji wakati Wa Tido na mkiboreshe, hata kama kitakuwa kinaudhi baadhi ya wakubwa lakini kinaleta mvuto wenye manufaa na faida kwa shirika letu kichukueni na muwaeleze wakubwa wanaokwazwa na kitu hicho manufaa yake. Msikubali TV ya Taifa kuitwa TV ya Chama, ondoeni mawazo hayo vichwani mwa watazamaji kwa kubalance story zinazohusu pande zote na matokeo mtayaona. Iboresheni TBC kuwa TV halisi ya Taifa.