Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Kuna yule Mama anatangaza habari za michezo anazingua balaa sijui anaitwa nani??????
Sijui alisoma chuo gani cha Habari ni shida kweli kweli Tema mate chini
 
Kiukweli huwa nasahau kama kuna channel inaitwa TBC..
Kukubalika tena kwa hii, labda baadae sana..
 
Nashukuru kwa ushauri wako mzuri tu na unaonekana uko makini na kuna ujumbe unataka ufike mahali.

Lakini TBC itabaki na Sera yake ya kuhakikisha Serikali na majukumu yake kwa Wanainchi yanatangazwa na si ushindani wa mbwembwe na kibiashara na TV zingine.

Kile ni chombo cha umma kinatoa Huduma kwa umma kama ilivyo shule,hospitali. n.k

Waache hao ITV Clouds na wengine waendelee na mbwembwe na unayoyataka wewe kuyaona lakini TBC itabaki na msingi yake.

Labda ushauri tu ni kuongeza ubunifu zaidi ktk baadhi ya maeneo ili kuendana na technology.
 
Haina mvuto muonekano mbayaa,..watangazaji wenyewe hawana mvuto...vipindi ndio vinaboa kabisa
 
Unataka TBC ibakie na misingi yake hata kama ni ya hovyo? Iendelee na misingi yake hata hakuna mwenye hamu ya kukitazama kituo hicho?

BBC, CNN ni vituo vya TV vya kitaifa lakini vinapendwa na asilimia kubwa ya watu wote Duniani? TBC kama inataka kuwa chombo cha umma, ijifunze kutoka kwa waliofanikiwa kuliko kushikilia misingi isiyo na manufaa kwa umma.

Nini sababu ya viongozi wengi kutumia vituo vya umma kuliko TBC? Jibu ni wazi, kama unataka watu wengi wakusikie unaenda kwenye kituo kinachosikilizwa na watu wengi.

Hata ukiwa na biashara, utakuwa mjinga kama utapeleka tangazo lako la biashara kwenye gazeti la UHURU wakati unajua kuna wasomaji wachache sana wa gazeti hilo, tena wale ambao wanalazimishwa kulinunua.
 
Huwa najiuliza, kama kweli CCM inaungwa mkono na watanzania wengi, iweje sasa hao wananchi wengi wanaoipenda hawachangamkii kuvitazama na kusoma magazeti yake, hali inayofanya vidorore na kukosa watumizi. Ina maana mashabiki wa ccm hawavutiwi na habari za chama chao?
Something of an irony, isn't it?
 
Mkuu gazeti la uhuru halina tofauti karatasi ya kuchambia kinachooandikwa mle ni upuuzi mtupu
 
Bias kwenye habari zao nyakati za uchaguzi,ila hilo hata wao wanalijua wasitafute mchawi
 
Hamna vipindi vya kuvutia ndani ya TBC yaan azam amekuja na wamewapiku wamewaacha mbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…