Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Greechie; inawezekana walikuwa wanajadili walikotoka na waliko sasa, ni kweli TBC inapoteza mvuto inachuja mmno habari na hawaiweki katika uhalisia, watu wanahitaji kusikia kitu kpya. Tido Mhando alipoiweka TBC kwenye chart wakamtumbua kwa hofu ya kuwafumbua macho watanzania, warudi kwenye strategic plan ya Tido waone kama TBC haitangara. lakini pia mambo ya kudharau tuache wizara ya habari inahitaji mtu makini sana mwenye upeo wa juu, na uwezo wa kuijua kesho si suala la mtu tu maadamu anajua kuchonga sana. wizara hii inalitangaza Taifa kimataifa.
 
Naombea kwny hivi ving'amuzi kuwe na option ya kudelete channel km kwny vile vya Madish makubwa hii ingekuwa ya kwanza kuifutili mbali
 
TBC ni sikio la kufa,tuwachie na chereko yao,na matangazo ya vifo.
Tv1 inawafunika kwa mbali
 
Hii tv inasimamia sera ya chama tawala, imeambiwa wafanyakazi wote wa serikalini wanatakiwa wasimamie ilani ya chama, hivyo chama ndio kinawapangia kila kitu
 
CONTENTS HAWANA sku ile muhim walikuwa wanaonesha twaarabu leo wasilaum
 
Uzi unatembea kama moto wa nyika!hii inaonyesha jinsi jamaa walivyochoka kwa michango inayotolewa humu.
 
Watangaji kila wakionekana wamevaa suti za kushonesha kwa Fundi yona sasa nani ataangalia watu waliochina hivyo haina ladha nyaaah!
 
Mi nawapenda ITV tu angalau kidogo wananifurahisha hasa kipindi kile cha saa 2 ucku weeee habari zote napata hao wengine wanaojifanya ndiyo television ya taifa, tv station ya kujipendekeza na kuwanyonya wasanii siwapendi basi tu
Angalia azam mkuu, ITV haifui dafu, kwa ubora sasa hivi Tanzania inaanza Azam two, ITV & channel ten, hawa ndio ambao hata ukiangalia taarifa zao za habari unazifurahikia.
 
Katika list ya channel zenye kila kitu hivi vituo vya television vinaongoza. Picha mbaya, sauti mbovu. Mtu unaangalia lets say music kwenye TBC2 unashindwa kujua hata sura ya msanii, sauti ndio usiseme utafikiri nyimbo wanazirekodi kabla ya kuzirusha.
 
Uonngozi wa juu wa TBC na wafanyakazi wengine wa kituo hicho usiku wa kuamkia leo wamefanya kikao cha dharura kuangalia sababu za kudorora kwa kituo hicho kikubwa cha TV ambacho kimemalizika saa 11 alfajiri.

Pamoja na mengine kitu kilichoonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni jinsi gani kituo kikubwa kama hicho kinachopata ruzuku kubwa kutoka serikalini kinakuwa na ratings za mwisho huku kikizidiwa na vituo ambavyo havina hata miaka mitano hewani.

Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC.
Itakuwa na ubora gani, wakati hata rais akienda kanisani kituo kizima kinahamia huko.
 
Bando langu la king'amuzi cha startimes likiisha..eti kuna TBC ndio bule..yaan kama nikiwasha basi TVI inahusika..sijui Mara ya mwisho kuangalia TBC zaidi ya robo SAA ni ln?
 
Kila leo ni safari ya kwenda Dodoma na Marin Hassan mshauliza hata maoni ya Watanzania ama watumishi kuhamia huko?Dodoma kuna nini hadi tuwe interested kuwatch tbc!?
Mmetoa bunge live tuwangalie wa nini?
Watangazaji wa habari hawavutii hawavai vizuri tuwaangalie wa ninii?
Wenzenu wote ni commercial based nyie mnaotegemea ruzuku mtapata wapi morale ya kuwa kama wao?
Mnadilike.,
 
Back
Top Bottom