Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Umuhimu wenu ni kipindi cha kampeni tu baada ya hapo tunafanya ziara wilaya za mkoa wa Dar na Mawingu TV....
 
Kuna siku kwa bahati mbaya king'amuzi kiliisha salio,ile watoto kufungulia tv channel zote hazionekani inaonekana tbc tu, watoto wakaanza kulia kama wamechomwa sindano kuuliza nini wanasema tumeona mizimu....ikabidi nirecharge fasta!!
 
Chereko tu ndio kipindi kizuri na kuna uwezekano hata Chereko ikahama huko TBC maana TBC hakuna anae ipenda
 
Waseme niwadondoshee wataalam wa vipindi na vichwa kama vitano ambavyo vitafanya mapinduzi katika media competition
 
Uonngozi wa juu wa TBC na wafanyakazi wengine wa kituo hicho usiku wa kuamkia leo wamefanya kikao cha dharura kuangalia sababu za kudorora kwa kituo hicho kikubwa cha TV ambacho kimemalizika saa 11 alfajiri.

Pamoja na mengine kitu kilichoonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni jinsi gani kituo kikubwa kama hicho kinachopata ruzuku kubwa kutoka serikalini kinakuwa na ratings za mwisho huku kikizidiwa na vituo ambavyo havina hata miaka mitano hewani.

Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC.
HATA VIONGOZI WA SERIKALI HAWAITAKI TBC WANATAKA CLOUDS TV NA VITUO BINAFSI. HAYO NDIYO MATOKEO YA KUTANGAZA HABARI ZA CHAMA TAWALA KAMA VILE WATU WOTE NI WANACHAMA WA CCM. WAFANYAKAZI WA TBC WAMEVIMBIWA NA RUZUKU WANAFICHAFICHA TAARIFA, HAYA ANGALIENI NYIE WAFANYAKAZI WA TBC PEKE YENU.
 
A lot of errors are there on TBC. They real need to change.
Starting from the management to personnels. Hata hiyo agenda ya kikao ilichelewa hii inaonyesha ni jinsi gani watu wanashindwa kustuka mapema mpaka wastushwe na jambo fulani. Its very bad
 
Yani hao jamaa duu taarifa ya Habari Mara wakosee...Mara warushe taarifa ya 3 badala ya 2 shida tupuu
 
Tatizo wanalijua wasitake kuhangaika, waache ubaguzi wa wazi wa kutoa habari za wapinzani wa kisiasa.
Wasipo acha hilo wasimtafute mchawi.
Habari zao ni kusifia chama kimoja tu, vya upinzani vinapotezewa wakati watu wote wanalipa kodi.
 
Walau hao TBC redio na TV yake wana afueni, hawa vilaza ZBC ndio tiro kabisaaaa, aibu , haki ya mungu watu wengi hawaitazami wanaaangalia zaidi TV za nje .
 
Chombo kinacho baguwa hata habari......lazima kitaoza tu. TBC imekuwa kama chombo cha Uenezi CCM, hivyo wapinzan wameipa tbc kisogo, wasio penda siasa na wasio kuwa na vyama nao wameipa tbc kisogo.

Tukiacha siasa bado mambo ya msingi kama live coverage, wao huyapa mambo ya hovyo kipaumbele kuliko matukio muhimu, mfano ajali ya Meli pale Nungwi, wakati vitu vingine vikiripot hizo habari wao TBC walikuwa wanapiga Taaribu tu.
 
Wakati Alipo kuepo Tido Muhando Aliludisha Iman Kwawatazamaji Lkn Alipo Ondoka Wakaludi Ktk Mfumo Wao Kama Chombo Cha Kisiasa Mimi Kwangu Imekua Nikama Mwiko Kutadhama Chombo Icho Mpaka Watakapo Jirekebisha
Wamwage fungu kwa Tido na chaaaazzzz Hilari waache ubahili
 
TV inaendeshwa kwa kodi za watanzania wote bila kujali itikadi za vyama, kabila wala rangi, but kutwa kucha inatangaza habari za CCM tu, Mimi nilisitisha kuangalia hii TV tangu enzi za Tido Mhando.
 
HUYU MKURUGENZI MPYA KIJANA SIJUI ANAKWAMIA WAPI?...
-->>AONDOE BIASIMENT
-->>PROGRAM ZA VIPINDI TVs,RADIO WAVIPANGILIE UPYA...
-->>WAITE DAMU CHANGA, ZENYE UBUNIFU KAMA GERALD HANDO.
-->>VIPINDI VYAO VILENGE KUNDI LA VIJANA WALIOWENGI KWA SASA...
-->>WAIBE WAFANYAKAZI MAHIRI KUTOKA VITUO VINGINE...

Mkuu, kituo kinapata RUZUKU KUBWA kutoka serikalini, Kama alivyotudokeza mtoa mada, kwahiyo hiyo mipango yote unayowapa haina nafasi kwani, kituo kipo kwa sababu ni cha serikali. Kama wanataka watanzania wawaangalie basi wajiendeshe kibiashara na kuacha kutegemea ruzuku.

Mimi mwenzio huwa naogopa hata kusimama kwenye hiyo channel pindi ninapo "scrow down" kusearch channels. (Mwaka wa 4 Huu Nadhani)
 
nilikuwa naangalia bunge tu! ila tokea wafute live coverage nimeshasahau tbc ni namba ngapi!
 
Back
Top Bottom