Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Uonngozi wa juu wa TBC na wafanyakazi wengine wa kituo hicho usiku wa kuamkia leo wamefanya kikao cha dharura kuangalia sababu za kudorora kwa kituo hicho kikubwa cha TV ambacho kimemalizika saa 11 alfajiri.

Pamoja na mengine kitu kilichoonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni jinsi gani kituo kikubwa kama hicho kinachopata ruzuku kubwa kutoka serikalini kinakuwa na ratings za mwisho huku kikizidiwa na vituo ambavyo havina hata miaka mitano hewani.

Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC.

Kuna baadhi ya taasisi kama TBC zinahitaji watu ambao ni wataalam na ambao wameishi ndani ya vyombo hivyo.

Ayubu Rioba anafaa kuendelea kufundisha chuoni lakini siyo kuendesha TBC, haiwezi.
 
wanarikodi kwa kutumia kamera.gani sijui?? picha hazina ubora video mchele kibao,waliniharibia flatskrini yangu ya kwanza!! siitazami tena
 
Huo ulikuwa in mkesha wa kuzimalizia pesa za OC za mwaka huu kabla ya kuingia mwaka mpya. Anayebisha akague pesa za OC uone kama hawakujilipa miposho, Ninyi huku mnazugwa ka mazuzu et kikao cha kujua sababu za mdororo wa TBC!!Wajinga ndo waliwao.Hivi Hugo Mkurugenzi ni kweli hajui chanzo cha mdororo wa TBC? Hata ile clip ya video iliyopo kwenye Uzi huu ambapo mtangazaji anasoma vichwa vya magazeti tofauti na habari iliyotawala kwenye gazeti husika? Ikiwa kweli hazijui sababu za mdororo wa TBC basi hapo alipo sio sehemu yake.
 
Hicho kilikuwa kikao cha upigaji wa Pesa, Siamini hata kidogo kama ni kweli hazijui sababu ya mdororo wa TBC, Hiyo clip ya video si inajieleza wazi kabisa? Sababu zipi wanazozitaka wao? Siku aliyoondoka Tido Mhando na ndo siku niliachaga kuitizamaTBC,Taarifa zao ni za upande mmoja, Enzi ya TIDO MHANDO taarifa ya habari ilikuwa unaipata live na haiachi chembe ya maswali,nini kimetokea,wapi,kwanini, Kivipi n.k yote hayo ulikuwa unayapata TBC ya mhando, Mhando hakufungamana na Tabaka tawala, Akizingatia aliombwa na Rais wa wakati arudi Tz aitumikie Nchi yake, Ndo akarudi kwa heshima ya Rais, kwahiyo Mhando hakujikomba kwa Rais ili kuipata ile nafasi, Sasa hawa waliopo sasa wapo bize kujikomba kwa Tabaka tawala kitu wasichojua ni kwamba Rais wa sasa anataka ukweli, Na ndiyo maana akiwa kwenye gazeti LA Uhuru aliwalaumu waandishi wa habari kwa kutokuiandika habari ya kuuzwa kwa mtambo wao wa kuchapia magazeti kwa bei ya kutupwa, Pia na ndio maana hata Card ya kuwatakia heri ya xmass na mwaka mpya kawapa Clouds TV ,Na zaidi ya yote alithubutu kupiga Simu Clouds TV akawapongeza kwa jinsi wanavyochambua magazeti!! Swali LA kujiuliza, kama Rais angekuwa anapenda mfumo wa uchambuzi wa magazeti wa kwenye TBC SI NA WAO ANGEWAPONGEZA NA KUWAPA CARD YA X MASS? SI ANGEWAPIGIA SIMU NA KUWAPONGEZA THE WAY WANAVYOCHAMBUA MAGAZETI YA KUACHA KUSOMA TAARIFA ZA UPINZANI KWENYE KIPINDI CHAO CHA MAGAZETI? Huenda hata kuitazama huwa haitazami hiyo TBC.!! Na ikiwa kweli haitazami, Hebu jiulize kapuku kama Mimi na wewe unawezaje kuitazama chombo kama hiki kisichofuata misingi ya habari?
 
Ni lini ulimsikia Rais kapiga Simu TBC au kuwapa kadi ya Xmass na mwaka mpya wafanyakazi wa TBC? YOte hayo yamefanyika kwa Clouds TV na hii ni uthibitisho tosha hata Rais mwenyewe alishagundua hiyo dosari waliyonayo hao TBC.
 
hivi tbc kumbe haijafungwa bado.

Tatizo tbc hakuna kipindi kizur hata kimoja, wao ni taarifa ya habari tu na kuonesha makala za kuisifia serikali, ccm na mkulu. watu hawana hata tamthilia au maigizo igizo ya kuvutia watu, nyie kila saa makala tuu, tizameni wenyewe sasa.

Ukitaka vipindi vizuri vya burudani na kuelimisha we tune tu Azam, kule kunao tamthilia, habari za kuvutia na hata ligi kuu ya hispania na ligi kuu bara
 
Wakati Alipo kuepo Tido Muhando Aliludisha Iman Kwawatazamaji Lkn Alipo Ondoka Wakaludi Ktk Mfumo Wao Kama Chombo Cha Kisiasa Mimi Kwangu Imekua Nikama Mwiko Kutadhama Chombo Icho Mpaka Watakapo Jirekebisha
Sasa mkuu tbc utatizama nini cha maana? hakuna cha maana pale.
 
Wangekesha masaa 24 au 48 kabisa,hukitaka kujua kuna ubaguzi angalia tarifa zao za uchambuzi wa magazeti hutaona wakisoma guardian, nipashe, citizen ,mwananchi ,Tanzania daima ,mtanzania kwa manati manatiThe Eastern Africa magazeti ya week wao ni magazeti ya Uhuru,Habari Leo na Daily news wakijusahau kwamba kodi zetu ndio zinawaweka hapo.Waajiulize kwanini watamgazaji wa IPP Media wanachukuliwa na BBC,DW,Radio ufaransa kiswahili,VOA na UN Radio na sio kutoka hapo kwao.Kama awajui wajue sasa hata star time bundle likisha mtu ananunua bundle kwa ajili ya Chanel ya ITV na Chanel Ten,na Star TV Mara nyingi ni kwa ajili ya BBC Swahili.
 
Mimi natazama kifurushi kikiisha kwenye king'amuzi na kipingi cha chereko tu.
Mi kfurush kikiisha naweka liungo likubwa natizama TV za mengi. Tbc sigusi, sina muda wa kuharibu na kupoteza unit kijinga jinga
 
HIV BADO KUNA MTU ANAANGALIA TBC ZAMA HIZ? MM SIKUMBUKI MARA YA MWISHO NIMEANGALIA LINI TBC. Kazi kweli kweli
 
Uonngozi wa juu wa TBC na wafanyakazi wengine wa kituo hicho usiku wa kuamkia leo wamefanya kikao cha dharura kuangalia sababu za kudorora kwa kituo hicho kikubwa cha TV ambacho kimemalizika saa 11 alfajiri.

Pamoja na mengine kitu kilichoonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni jinsi gani kituo kikubwa kama hicho kinachopata ruzuku kubwa kutoka serikalini kinakuwa na ratings za mwisho huku kikizidiwa na vituo ambavyo havina hata miaka mitano hewani.

Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC.

Tatizo kituo cha TBC kinatangaza mambo ya chama kimoja tofauti na Enzi za Tido Mhando! ya kweli wanaficha or rather skip mfano uchambuzi wa magazeti ni the simplest criteria ya kipimo cha TBC. It's far better kuangalia Millard AYO tv than Tbc!!!! Truth is bitter but we have to swallow the bitterness.
 
Mi nawapenda ITV tu angalau kidogo wananifurahisha hasa kipindi kile cha saa 2 ucku weeee habari zote napata hao wengine wanaojifanya ndiyo television ya taifa, tv station ya kujipendekeza na kuwanyonya wasanii siwapendi basi tu
 
uwazi na uwajibikaji......wajaribu kufanya kwa kuzingatia kauli hiyo....
 
Waangalie jinsi BBC inavyofanya kazi hakuna kuipendelea serikali wala chama tawala habari inakuwa balanced kweli!!!
Haya mambo ya kuwa taasisi ya itikadi ndio inakuwa ya mwisho kwa kuangalia na jamii sasa hata watoto wadogo hawaitaki TBC!!!
 
Kwani CCM na Wao wameisusa TBC baada ya kuitumia kama toilet paper?
 
TBC ni chombo cha cha propaganda cha CCM na Seriksli yake. TBC iko kidiasa zaidi kwa ajili ya maslahi ya Wanasiasa!
Kwa sasa hakuna anayejali itakuja onekana tena ya maana Uchaguzi Mkuu 2020!
 
TBC ni imara na ndiyo yenye vyombo vya thamani kubwa sana ktk studio zake.

Wafanyakazi wake ni professional wote na ni TV inayojua nini inafanya ktk tasnia ya habari


TBC hawasubiri sifa za kupongezwa kwani wao wanawajibika kuwapa wanainchi taarifa,kuwaburudisha na kuwaelimisha.

TBC Obvan yao ni Kali sanaa na ziko chache nchi za Africa.

Ile ni TV ya Taifa na itaendelea kufanya kazi ktk kuitangaza Serikali kama Sera inavyosema.
Wewe ni NP katika Id tofauti, unaambiwa watu wamekaa hadi usiku Wa manane wanajadili kudorora kwa ufanisi Wa chombo hiki cha wananchi. Wanatafuta sababu za kwa nini watazamaji hawakithamini kama vyombo vingine wewe unakuja na ngonjera ya "wana OB van ya kisasa"? Ama kweli nyie wapigania 'UHURU" wa siku hizi ni vipofu. Na wewe Unadhani kwa maneno hayo umetoa mchango murua Wa kuboresha TV ya Taifa.? Hili liko wazi TV ya wananchi haipendwi na wananchi, ni wajibu Wa waliopewa dhamana ya kuisimamia kujiuliza kwa nini watu hawapendi chao. Tutoke na ushauri Wa kuwapa ili kurekebisha hii hali maana ni wazi kama TV hii isingekuwa inapata Ruzuku ikategemea mapato yake kujiendesha ingeshafungwa miaka 3 iliyopita. Baada ya Tido aliyeletwa kuondolewa ubunifu ulikosekana. Waliowashauri Viongozi wetu kumwondoa Tido kwa sababu za kisiasa hawakuangalia faida ya kibiashara na kimvuto waliyokuwa wanaipoteza kwa kumwondoa Mr. TM. Chombo cha habari kitavutia matangazo yanayokiingizia faida kwa kuwa kinapata watazamaji wengi, na kitapata watazamaji wengi pale tu kitakapokidhi matakwa na mapenzi ya watu wenye mitazamo tofauti. Kutangaza kwa kuremba habari za upande mmoja na wakati mwingine watazamaji wakiona wazi zinapotoshwa kwa masililahi ya upande huo ambayo obviously siyo maslahi ya taifa per se,kunawaondoa na kuwapoteza watazamaji makini hata Wa upande huo. Katika ulimwengu Wa sasa Wa utandawazi ambapo taarifa husafirishwa kwa njia mbalimbali si rahisi kuwadanganya watu. TBC angalieni mlipojikwaa msiangalie mlipoangukia, tafuteni kilichorudisha imani ya watazamaji wakati Wa Tido na mkiboreshe, hata kama kitakuwa kinaudhi baadhi ya wakubwa lakini kinaleta mvuto wenye manufaa na faida kwa shirika letu kichukueni na muwaeleze wakubwa wanaokwazwa na kitu hicho manufaa yake. Msikubali TV ya Taifa kuitwa TV ya Chama, ondoeni mawazo hayo vichwani mwa watazamaji kwa kubalance story zinazohusu pande zote na matokeo mtayaona. Iboresheni TBC kuwa TV halisi ya Taifa.
 
Kama Dr. Ayoub Ryoba naye hajui sababu ya kutopendwa kwa TBC Kuna haja ya Ben Saanane kupekua PhD yake. Hilo jambo liko uchi (crystal clear) kabisa

Akina Marina Hassan (?) ni afisa uenezi wa CCM tawi la TBC
 
Back
Top Bottom