Enzi za Nyerere ATC iliwahi kukodi ndege marehemu toka kwa mpalestina George Hallack, siku ya uzinduzi wa safari yake ya kwanza toka Dar es Salaam kwenda London ndege ilikuwa kama Dar Express, ilikwenda mpaka mwisho wa uwanja ikagoma kuruka! Ilibidi basi la uwanja wa ndege likawachukue abiria na kuwarudisha mjengoni, hiyo ndege iliishia hapo uwanjani na hakuna mtu yeyote aliyechukuliwa hatua. Magufuli, aliagiza meli kwa ajili ya abiria kati ya Dar na Bagamoyo, meli ilianza safari kwa mbwembwe zote za kiccm, ilichukua saa mbili toka bandarini Dar mpaka Kunduchi! Magufuli akateremka na kurudi mjini, meli ilitelekezwa bandarini na hakuna aliyechukuliwa hatua, pia kuna manyangarakasha mengine mengi tu yaliyokula pesa zetu huku tukiongezewa kodi kufidia hasara.