Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 40,828
- 99,523
Wananchi wengi ni wenye kipato cha chini hawana uwezo wa kulipia hiyo Azam, mimi nahisi ni serikali kutaka kuchagua nini waonyeshwe wananchi na nini wasionyeshwe katika yanayotokea bungeni.
Tutakosa fursa ya kuona na kusikia mambo mengi, kipindi kinapo kiwa recorded huko kunafanyika editing pale penye ukakasi basi pataondolewa ili kuuficha huo ukakasi, na hakuna tv nyingine yoyote inayolusha matangazo haya moja kwa moja, hi ni kuwakosea watanzania na kupoka haki yao ya kikatiba kupata habari
Hii ya jioni subiri kuangalia bunge ambalo watakuwa wameli edit kutokana na muongozo kutoka kwa waziri wa habari Nape, usidhani utashuhudia cheche za kina LISU, ZITTO, na wabunge wa upinzani wanapo ibana serikali, tuta nangalia ki makapi tu.
Minaona huyu Nape sasa anatafuta sifa aiseeee.....
Na kama haya ni maagizo kutoka kwa mkubwa wake, naanza kupata maswali na wasiwasi kwamba..... Ni kipi hasa ambacho serikali inakiogopa hasa waTanzania wasikijue kutoka bungeni..!?