TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Bunge lenyewe linaoneshwa muda wa kazi,,ivi nani anapata muda wakuangalia bunge? Humu ndani inaonekana watu wengi ni mahouse girl ndo mnaolalamika manake mnakuwa nyumbani muda mwingi basi Nape amewasikia atawafikiria..!!
Na wewe sa hizi unatakiwa uwe kazini, au ndo uko kazini hivyo?
 
Sasa hizo Gharama anazosema Nappe 4bil za wapi? Ndio hizo zitalipwa kwa kodi zetu yeye(Nappe) asiwe na wasiwasi maaana serikali ina hela nyingi sana ndio maana tumepigwa bil 129 na NIDA.
Yani ndo tatizo lakuwa na watu wasiofikiria hv TBC inavipindi vingapi vya ovyo kwann wakati wa Bunge wavifute vyote na hzo pesa waelekeze kurusha live bunge. Kwanza hzo bilion nne nyingi sana sahz technolojia ni kubwa mno labda km wanalipana maposho makubwa makubwa
 
Huoni tatizo? Kuna kitu kinaitwa KUCHUJWA KWA HABARI.


Hakuna Habari isiyochujwa hapa Duniani, habari zote unazozipata Dunia hii huwa zimeshachujwa kulingana na matakwa ya mleta habari, na Hii ni Dunia nzima hata Biblia ilichujwa kwanza kabla ya kuandikwa, kuna baadhi ya vitabu viliachwa na watawala!
 
Kuna hoja ya msingi hapa zaidi ya watu kufanya kazi muda kazi na siyo kuangalia Bunge? Kama Serikali ingekataza kuonyeshwa Bunge kabisa hapo sawa lkn litaonyeshwa lote jioni baada ya kazi, tatizo liko wapi hapo?

Mkuu Barbarosa.....
Kwa kauli hii ya Nape, ikisikilizwa na yeyote mwenye upeo mpana inaleta maana zaidi ya alicho kitamka.
Kwamfano mimi binafsi nineelewa kwamba kuna hoja ya kuhariri au kuchuja matukio yanayo rushwa moja kwa moja toka bungeni ili watazamaji wapate habari (makapi) baada ya kuhariri.
Chukua mfano wa kinacho fanyika hapa jf, iwapo Mod wanapo hold hoja au mawazo ya mchangiaji, then wanakuja kuyaleta kwa jinsi watakavyo wao. Hua hauoni minyukano na malalamiko ya jf member iwapo panatokea mambo kama hizo!?
Naaaa...
Kuwanyima wapigakura fursa ya kuwaona wawakilishi wao wanavyo wa wakilisha live, pia ni kosa na sioni hoja ya msingi kwa waziri Nape kuleta sheria hii kwa kisingizio cha Bilioni 4
 
Kuna hoja ya msingi hapa zaidi ya watu kufanya kazi muda kazi na siyo kuangalia Bunge? Kama Serikali ingekataza kuonyeshwa Bunge kabisa hapo sawa lkn litaonyeshwa lote jioni baada ya kazi, tatizo liko wapi hapo?
Litaoneshwa lote ndani ya lisaa limoja? How? Jana nimeona marudio yakiwa yamekatwa na hoja ya uchaguzi wa zanzibar ikiondolewa kabisa! Hicho ndo tunataka?
 
Hujawahi sikia TV au Radio za Tanzania zikisema sasa tunajiunga na BBC kusikiliza taarifa za habari? Ina maana BBC akizima mitambo yake wewe huwezi kujiunga naye kurusha hicho kipindi.Kama Star tv walikuwa wakijiunganisha na TBC kurusha matangazo automatically TBC wasiporusha Star TV hawezi rusha kwa sababu hawi na mitambo yake eneo husika.Kama BBC wasiporusha kipindi wewe huwezi rusha kwani huna mitambo yako eneo husika ulijiunga tu
Sio kweli....Star TV huwa wanarusha wao moja kwa moja, na ndio maana kama ukichunguza, utakuta picha za star TV zinakuwa tofauti na za TBC kimatukio kwenye Bunge...huyu anaweza kuwa anaonyesha kiti cha Spika, wakati mwingine anaonyesha Mbunge anayezungumza. Wanaojiunga na TBC huwa ni ITV, Channel 10, etc, amabao hata nembo ya TBC huwa inaonekana.
 
Bunge lenyewe linaoneshwa muda wa kazi,,ivi nani anapata muda wakuangalia bunge? Humu ndani inaonekana watu wengi ni mahouse girl ndo mnaolalamika manake mnakuwa nyumbani muda mwingi basi Nape amewasikia atawafikiria..!!
Acha kashifa kijana tupo humu ndani watu wenye miladi yetu na tunaweza kukupa kazi ukafanikiwa maishani mwako..
 
Zitto Kabwe


TBC walikuwa na fedha ya
kurusha hotuba ya Rais 'live'
ila hawana fedha ya kurusha
mjadala wa hotuba hiyo!
Nilisema. Dola inataka Bunge
kibogoyo


Source: FB Page.
 
Kuna hoja ya msingi hapa zaidi ya watu kufanya kazi muda kazi na siyo kuangalia Bunge? Kama Serikali ingekataza kuonyeshwa Bunge kabisa hapo sawa lkn litaonyeshwa lote jioni baada ya kazi, tatizo liko wapi hapo?
Sijui kama umesoma tangazo na kulielewa. Wamesema wataonyesha sehemu tu ya bunge na sio kipindi chote
 
Litaoneshwa lote ndani ya lisaa limoja? How? Jana nimeona marudio yakiwa yamekatwa na hoja ya uchaguzi wa zanzibar ikiondolewa kabisa! Hicho ndo tunataka?


Litaonyeshwa tu, wewe fanya kazi muda wa kazi ili tuongeze uzalishaji na ktk hapa, Zanzibar inakusadia nini? Inakulipia bili zako?
 
Hakika hii nchi tunapoelekea sasa naamini tunaanza kuingia katika zama za kidictator kwa kubana uhuru wa kupata habari pamoja na kupata habari sahihi kwa muda muafaka.
Tangia rais mpya (JPM) aingie madarakani, ilionekana ameanza vizuri kwa kasi ya ajabu katika mambo mbali mbali iliyoamsha mategemeo mengi ya wananchi wa Tanzania walioamini kweli sasa amepatikana rais bora atakayeweza vusha watanzania katika wimbi hili la umaskini uliokithiri miongoni mwa watanzania wengi, zaidi ya nusu.
Ila cha kushangaza democrasia ikaanza kukandamizwa taratibu na sarakasi za hawa wanaojiita watenda haki (ccm) kwa ujumla wake katika chaguzi za mameya hapa jijini dar es salaam katika wilaya mbili muhimu lakini baadaye ukawa waliibuka kidedea kutokana na mshikamano wake katika kuamini kuwa hawa wezi (ccm) watakondolewa tu umoja wao usipotetereka. Na cha kushangaza wakati haya yanatendeka aliyejiita rais wa wote wala wasaidizi wake hawakujitokeza kukemea hujuma za wanachamama wao katika hili suala, huku sheria zikionekana wazi kujaribu kupindishwa ili tu kuwabeba.
Pili likaja suala la gazeti la mawio kufungiwa moja kwa moja kwa sababu dhaifu kuwa habari zake zinachochea vurugu. sasa hapa unajiuliza, hivi hii nchi kweli ni yenye kujali democrasia na uhuru wa vyombo vya habari, maana imeonekana wazi kuwa magazeti yanaoandika habari na makala za kipelelezi (investigative journalism) zenye kugusa moja kwa moja serikali na madudu yake hayatakiwi katika nchi hii. Hili liliwahi kujitokeza huko nyuma kwa gazeti la mwanahalisi kufungiwa kwa sababu kama hizi ila baadaye likaja kushinda kesi na kurudi mtaani huku watu wakiendelea kulisoma.
Tatu ni hili la leo kusema kuwa vikao vya bunge havitakuwa vinarushwa live tena bali vitakuwa vinarekodiwa na kurushwa kwa saa limoja usiku, sababu ikiwa dhaifu mno (bilioni 4 kwa mwaka ni nyingi sana). katika watu walio na mtindio wa akili, huyu jamaa au aliyemtuma, mtindio wake ni wa hali ya juu. Katika zama hizi, zinazosemekana ni za ukweli na uwazi, bilioni 4 kwa mwaka kurusha matangazo ambayo ni roho ya nchi, ni pesa gani? Na bado hapo hapo tbc inapokea ruzuku kutoka serikalini ambazo ni kodi zetu sisi wananchi. Hii nchi ni kituko sijawahi ona. Hakika naona taratibu tunafungwa midomo pamoja na kutotakiwa kusikiliza mijadala mbali mbali inayoendelea bungeni ambako ndiko hoja mahsusi na nzito zinapoibuliwa na wabunge mbali mbali kutokana na accessibility yao ya taarifa na pia sisi wananchi kupata taarifa ambazo tunaweza kuwahoji tuliowapigia kura pale tunapokuwa na mashaka na mambo kadha wa kadha yaliyoibuliwa katika chombo hiki nyeti nchini.
Kwa mwenendo huu, wa kuminya democrasia kila kukicha kinachofanywa na hawa ccm, kitakuja kuzua tafrani kubwa sana nchi hii, maana mtu anapojiona kama mungu na kuamuru kuwafanyia watu anachoamua tu bila kujali mapokezi ya upande wa pili hakika athari zake ni kubwa mbeleni. Zanzibar washindwe lakini bado wang'ang'anie, bado huku bara waje na kauli kama hii.
Amani huletwa na haki na usawa, na sheria iliyopindishwa sio sheria hata kidogo.
Mungu naomba utupe nguvu na ujasiri wa kupinga hizi hujuma kwa watanzania unaofanywa na hawa mafisiemu.
 
itv
whazap zipo tutaona tuu

Kwani si wengine wote walikuwa wanapata feed kutoka tbc? Sio kwamba ndio maana hata star tv nao wameshindwa kurusha? Kwa maana hiyo hata itv wakipata si itakuwa hiyo hiyo edited version ya tbc? Unless watu bungeni warekodi wenyewe kwenye smartphone zao, je inawezekana?
 
Sasa hizo Gharama anazosema Nappe 4bil za wapi? Ndio hizo zitalipwa kwa kodi zetu yeye(Nappe) asiwe na wasiwasi maaana serikali ina hela nyingi sana ndio maana tumepigwa bil 129 na NIDA.


Hata kina Masamaki wamepiga fedha nyingi lkn bado tunaishi.


Nape asiwe na wasiwasi
 
Back
Top Bottom