TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Matumizi mengine ya kijinga ni kulipa ruzuku kwa vyama vya siasa ambavyo vina zaidi ya miaka 20. Wafute hizi ruzuku vyama viendeshwe kwa ada na michango ya wanachama.

Nakubaliana na wewe hii itapunguza pia mzigo kwa mlipa kodi .Wanachama wa vyama husika waendeshe vyama vyao kwa gharama zao
 
Ni maafa, tena makubwa sana. Waziri Nape kaleta kauli ya serikali Bungeni kuwa maonyesho ya moja kwa moja Bungeni hayatakuwepo tena eti ni gharama na TBC1 hawana uwezo wa kugharamia shilingi Bil 4 kwa mwaka.
Dalili za kutoruhusu mijadala hiyo hasa kwa sasa wanapoijadili hotuba ya Rais ni kuwa hawataki wananchi waone wabunge wanavyo ichambua na kuiagiza serikali ifanye nini. Jee zuio hili lina baraka za Rais Magufuli?
Mbona yeye anapotumbua majipu anapenda kupata coverage ya Tv na Radio na awe hataki serikali yake kuwa kikaangoni watu waone? Hii ni dalili mbaya sana ya utawala wake na ni dhahiri anayoyafanya yana ashiria kuwa ni maigizo tuu na hana nia ya dhati ya uwajibikaji kwa mawaziri ambao tayari kaonyesha kutokuwa na imani nao kuweza kuwakabili wabunge.
Namsifu sana Mhe Zitto Kabwe kwa kuonyesha ujasiri wa kulipigania hilo ingawa amekumbana na vikwazo toka kwa Mwenyekiti wa Bunge Chenge. Chenge pamoja na kutajwa kuwa ni mweledi katika mambo ya sheria lakini leo kaonyesha ni mtupu kabisa na kawekwa pale kwa malengo maalum.
Sisi wananchi kama wamiliki wa TBC1 tupinge kwa nguvu chombo hicho kuzuiwa kutuonyesha Bunge live.
huku tunakoelekea sasa sio kwema kabisa. Hakuna kitu kibaya kama kuwanyima haki ya habari wananchi kkatika karne hii ya 21. Hili wasipoliangalia ndio litaiangusha CCM vibaya zaidi
 
Sasa gharama hizi zinawahusu mpaka Star Tv?

Hujawahi sikia TV au Radio za Tanzania zikisema sasa tunajiunga na BBC kusikiliza taarifa za habari? Ina maana BBC akizima mitambo yake wewe huwezi kujiunga naye kurusha hicho kipindi.Kama Star tv walikuwa wakijiunganisha na TBC kurusha matangazo automatically TBC wasiporusha Star TV hawezi rusha kwa sababu hawi na mitambo yake eneo husika.Kama BBC wasiporusha kipindi wewe huwezi rusha kwani huna mitambo yako eneo husika ulijiunga tu
 


Serikali imechukuwa uamuzi sahihi kabisa, ilikuwa inafikia wakati unakwenda ofisini kupata huduma wafanyakazi wamekodoa kwenye luninga wanaangalia Bunge, Nasema SAFI SANA NAPE!
Mbona kwenye banks wahudumu hawazitazami hizo tv wakati wa kipindi cha bunge? Tv zimewekewa wateja sio watoa huduma maofisini na sehemu nyenginezo.
 
Safi sana hiki kilikuwa ni kilio changu siku zote, Watu wafanye kazi na waache kuangalia Bunge, mkirudi nyumbani jioni baada yakazi mtaangalia Bunge tani yenu au kama mmechoka hata wkend!

Safi sana W. Nape!

Mkuu...
Pamoja na kwamba siipendi na siangaliagi TBC, Lakini sikutegemea kama haya ni maandiko yako aiseeee....😕
 
Tunaenda kwenye wakati mgumu sana kama hatutaweza kuwambia watawala ukweli hata kama unatuumiza sisi wenyewe
 
Ndio maana nilikuwa najilazimisha kuikubali hii serekali ya Magufuli ila moyo ukawa unakataa kabisa hii serekali inaweza kuwa ya kidikiteta kwanza bomoa bomoa pili wamezima tbc watu wasione udhaifu wao.. Hata mawaziri alio chagua ni wale wa hovyo tusiowatalajia.. Wallah nawaambia Kikwete alikuwa rais na tutamkumbuka.. Kikwete ambae tulipo lalamika kuhusu mawaziri wake kuwa wabovu aliwapiga chini nakuweka wengine kwa Magufuli hiyo hamna.. Leo tbc juzi mawio kesho sijui nn
Mkuu kweli watu wengi waliochagua upinzani tayari walishaanza kuikubali kazi anayoifanya jpm sasa kwa kuanzia kuminya uhuru wa habari

Mbaya zaidi kuzima tbc watu wasiangalie wabunge wao hili
Litakuwa kosa kubwa.
Ccm watalijutia.
 
Barbosa najua unaweza kufikiri zaidi ya hapo, too sad kuwa umeamua kuchagua upande wa kitu/MTU na wala Si upande hoja/misingi.


Kuna hoja ya msingi hapa zaidi ya watu kufanya kazi muda kazi na siyo kuangalia Bunge? Kama Serikali ingekataza kuonyeshwa Bunge kabisa hapo sawa lkn litaonyeshwa lote jioni baada ya kazi, tatizo liko wapi hapo?
 
Kama gharama ni kubwa hakuna haja ya kurusha mipasho hiyo, pesa hizo zielekezwe kwenye huduma nyingine za jamii mfano kununua madawati shuleni n.k
 
HAWA WAHESHIMIWA WANGEJUA TUKO BUZY TUNATAFUTA MKATE WASINGEHANGAIKA KUUZA SURA. WAO WAJADILI HOJA ZA MSINGI NA MA RIPOTA WATATUPA TAARIFA.

HIVI KWA KASI YA DR. JPM YA "HAPA KAZI TU" NANI ANA UJASIRI WA KUACHA KAZI AANGALIE BUNGE?? UNLESS NI HOTUBA MUHIMU.

HATA KWENYE MABAA WATU WAKO BUZY NA KWANZA HAWAENDI KUKAA BAA HAWANA HELA YA KUNYWA SAA HIZI.

KILA MTU ANAKIMBIZANA NA MAISHA APATE MKATE. MAMBO YA KUWA WANANIONA YAMEPITWA NA WAKATI.

WAPIGA KURA WAKO BUZY WANATAFUTA CHAKULA KUPITIA KAZI AU BIASHARA. MUDA WA KURANDARANDA NA KUKAA KUSIKILIZA MIPASHO YENU HATUNA #hapakazitu

Queen Esther


Katika kauli za Mawaziri, Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, ametangaza kwamba, Kuanzia tarehe 26 Januari mwaka 2016, TBC1 haitaonesha tena Mikutano ya bunge live kutokana na gharama za kuonesha live kufikia bilioni nne kwa mwaka.

Badala yake TBC1 watarekodi na kuonesha katika kipindi maalum usiku kuanzia saa nne hadi saa tano.

Hii itanyima wanchi fursa ya kuona kinachoendelea Bungeni.
 
Tbc mda huu wameweka mchezo wa kuigiza! Haaaaaaaah
 

Hilo nalo ni wazo lkn haliko chini ya uwezo Serikali, hili la Bunge ni rahisi kwa maana Bunge ni chombo cha Serikali na ndiyo kinaamua nani arushe matangazo yake!
Anyway, sio kosa lenu. Mmezoea kusifia Kila kitu hata kama ni utumbo. Kwa ushauri tu. Wasirushe hata kipindi cha maswali na majibu maana wanawafanya watu wasifanye kazi waangalie bunge
 
Katika kauli za Mawaziri, Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, ametangaza kwamba, Kuanzia tarehe 26 Januari mwaka 2016, TBC1 haitaonesha tena Mikutano ya bunge live kutokana na gharama za kuonesha live kufikia bilioni nne kwa mwaka.

Badala yake TBC1 watarekodi na kuonesha katika kipindi maalum usiku kuanzia saa nne hadi saa tano.

Hii itanyima wanchi fursa ya kuona kinachoendelea Bungeni.

Naona tunaelekea Kubaya yan karne ya leo watuonyeshe recording hasa ukizingatia mambo ya msingi sana yanayojadiliwa bungeni...Hapa nawasihi wabunge wote wenye dhamila ya kweli kuleta mabadiliko wasikubali hii kitu..TBC ni mali ya watanzania na bunge linatuwakilisha sisi, hvyo tuna haki zote kujua nini kinaendelea pasipo kificho.
 
Walianza kuzuia Mikutano ya Wapinzani kwa kisingizio cha Hapa Kazi Tu....


Tumekaa kimya..

Sasa wameamua kuzuia na Matangazo ya Bunge.


Jakaya alisaini Open Government Partenership... Huu ndio Uwazi ktk Serikali???
 
Mambo ya bunge live ni kuleta uchochezi tu,ndo maana hata mataifa makubwa yenye democracy kubwa kuliko sisi hakuna mambo ya bunge live,
jk alitudekeza sana,,sasa hivi NI KAZI TU
 
Mbona kwenye banks wahudumu hawazitazami hizo tv wakati wa kipindi cha bunge? Tv zimewekewa wateja sio watoa huduma maofisini na sehemu nyenginezo.



Hata mteja ataangalia Bunge jioni akirudi nyumbani, kuna wateja wengi huwa wanapitiliza wanaitwa namba zao hawazisikii kwa sababu wamekodolea luninga, Bunge na hii yote hupunguza uzalishaji kwani unasogeza muda mbele ambapo wateja wengine wangeshahudumiwa tayari!
 
Back
Top Bottom