TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Tatizo siyo gharama amesema hivyo ili wavivu msilalamike lkn sababu hasa ni kwamba huu ni muda wa kazi na siyo wa kuangalia luninga, hivyo fanyeni kazi na Bunge mtaliona jioni baada ya kazi au wkend!
we jamaa mbn huelewi umemsikiliza vizur au ni mahaba hata penye ubovu?unakurupuka kama serikal yako
 
Kuna hoja ya msingi hapa zaidi ya watu kufanya kazi muda kazi na siyo kuangalia Bunge? Kama Serikali ingekataza kuonyeshwa Bunge kabisa hapo sawa lkn litaonyeshwa lote jioni baada ya kazi, tatizo liko wapi hapo?
Wazime mitambo ya television muda wa kazi. Maana sioni mantiki hapo. Kuhusu mtu kufanya kazi hilo ni suala la kiutawala. Kuna wasimamizi kwenye maofisi
 
Anyway, sio kosa lenu. Mmezoea kusifia Kila kitu hata kama ni utumbo. Kwa ushauri tu. Wasirushe hata kipindi cha maswali na majibu maana wanawafanya watu wasifanye kazi waangalie bunge


Kama hilo linawezekana yote heri tu ili muda wa kazi utumike kufanya kazi na jioni mkirudi nyumbani mnaweza kuangalia Bunge lenu tukufu!
 
Bora na jioni tuendelee kufatilia live. Wasitunyanyase kiasi hicho
Hii ya jioni subiri kuangalia bunge ambalo watakuwa wameli edit kutokana na muongozo kutoka kwa waziri wa habari Nape, usidhani utashuhudia cheche za kina LISU, ZITTO, na wabunge wa upinzani wanapo ibana serikali, tuta nangalia ki makapi tu.
 
Tutakosa fursa ya kuona na kusikia mambo mengi, kipindi kinapo kiwa recorded huko kunafanyika editing pale penye ukakasi basi pataondolewa ili kuuficha huo ukakasi, na hakuna tv nyingine yoyote inayolusha matangazo haya moja kwa moja, hi ni kuwakosea watanzania na kupoka haki yao ya kikatiba kupata habari
 
Tutaangalia azam
Wananchi wengi ni wenye kipato cha chini hawana uwezo wa kulipia hiyo Azam, mimi nahisi ni serikali kutaka kuchagua nini waonyeshwe wananchi na nini wasionyeshwe katika yanayotokea bungeni.
 
Wazime mitambo ya television muda wa kazi. Maana sioni mantiki hapo. Kuhusu mtu kufanya kazi hilo ni suala la kiutawala. Kuna wasimamizi kwenye maofisi


Lakini Serikali pia ina jukumu la kuweka mazingira mazuri ya kuongeza ufanisi wa kazi na hii ni pamoja na kuondoa Bunge kuonyeshwa muda wa kazi, huu ni upande wa Serikali na waajiri nao watafanya pale wanapoweza, lkn Serikali imefanya vizuri Sana!
 
Mambo ya bunge live ni kuleta uchochezi tu,ndo maana hata mataifa makubwa yenye democracy kubwa kuliko sisi hakuna mambo ya bunge live,
jk alitudekeza sana,,sasa hivi NI KAZI TU

Uko sahihi mkuu lakini pia Kuna mihimili mitatu.kuna Bunge,mahakama,na SERIKALI.Hiyo TV ni mali ya Serikali sio ya bunge.Huwezi lazimisha mali za muhimili mwingine zitumikaje na muhimili mwingine.TBC hawalazimiki kisheria kurusha mijadala ya bunge.
 
Yaani mm naona hata kumpa haki ya ndoa mkeo unasubiri magu Aseme. Maana sioni tija ya hapa kazi tu na kutoonyesha bunge. Yaani unanithibitishia unyumbu wako


Kama itaongeza uzalishaji na nchi isonge mbele basi na iwe hivyo, HAPA KAZI TU!
 
Msijali sana mwanadamu ana hulka moja mnapo mbana kwa njia moja yeye hufikiria njia nyingine ni swala la muda tu ngoja tuone hizi sarakasi zinaishia wapi ,ndio maana kwenye zile picha za January kuna nyani wazee wamekaa wanamwangalia nyani mtoto anavyocheza na nyaya za umeme ...........
 
Kuna hoja ya msingi hapa zaidi ya watu kufanya kazi muda kazi na siyo kuangalia Bunge? Kama Serikali ingekataza kuonyeshwa Bunge kabisa hapo sawa lkn litaonyeshwa lote jioni baada ya kazi, tatizo liko wapi hapo?
Huoni tatizo? Kuna kitu kinaitwa KUCHUJWA KWA HABARI.
 
Kwamba gharama ta kurusha live ni kubwa, hivyo watarekodi na kurushwa kuanzia saa nne usiku. Live itakuwa asubuhi tu kipindi cha maswali na majibu. Na Star TV nao...
Hzo bilioni nne ni posho au nini? Yan techonlogia ilivyokubwa hv vikao vya bunge kwa mwaka mipesa yote hyo. Hapo pana jipu Hapo sio bure
 
Ule mpango wa kupiga kelele na kujionesha kwa wananchi eti unawatetea kumbe unatetea tumbo lako umefikia ukingoni....

Sasa kipimo cha ubunge sio kubwabwaja kwa sauti kubwa bali kuwasilisha hoja za maana.

Daktari haitaji live coverage ili afanye kazi zake....

Mwalimu haitaji live coverage ili afundishe...

Wale wapenda sifa na comedians imekula kwao!
 
Bunge lenyewe linaoneshwa muda wa kazi,,ivi nani anapata muda wakuangalia bunge? Humu ndani inaonekana watu wengi ni mahouse girl ndo mnaolalamika manake mnakuwa nyumbani muda mwingi basi Nape amewasikia atawafikiria..!!
 
TBC sio Shirika la Biashara.

Linaendeshwa kwa kodi zetu....
Sasa hizo Gharama anazosema Nappe 4bil za wapi? Ndio hizo zitalipwa kwa kodi zetu yeye(Nappe) asiwe na wasiwasi maaana serikali ina hela nyingi sana ndio maana tumepigwa bil 129 na NIDA.
 
Kama hilo linawezekana yote heri tu ili muda wa kazi utumike kufanya kazi na jioni mkirusdi nyumbani mnaweza kuangalia Bunge lenu tukufu!
Waziri wako kasema kubana matumizi, we unasema watu wafanye kazi, watanzania wamsikilize nani?.
 
Ni kuwanyima wananchi kuona wawakilishi wao wanafanya nini
 
Katika kauli za Mawaziri, Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, ametangaza kwamba, Kuanzia tarehe 26 Januari mwaka 2016, TBC1 haitaonesha tena Mikutano ya bunge live kutokana na gharama za kuonesha live kufikia bilioni nne kwa mwaka.

Badala yake TBC1 watarekodi na kuonesha katika kipindi maalum usiku kuanzia saa nne hadi saa tano.

Hii itanyima wanchi fursa ya kuona kinachoendelea Bungeni.
Tuache kulala na wake zetu usiku tuangalie bunge sa tano. Bora wasirushe kabisa tu.
 
Nape:

Anatangaza kuwa TBC
itakuwa inatangaza baadhi
ya matukio ya Bunge
Lengo ni kubana
matumizi..


Anasema gharama za kuendesha Bunge zimefikia 4Bln kwa Mwaka.


Anasema kutakuwa na
kipindi maalum kitakachokuwa kinarushwa usiku kuanzia saa 4 hadi 5 Usiku.



.
Wataangalia popo na bundi...mimi nitakua nimelala muda huo.
 
Back
Top Bottom