TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Hata wakisimama bungeni na kuimba kupinga,haisaidii kitu maana hakuna anaewaona,bora hawa wauza sura wawe wapole na wafanye kazi,zama za kuuza nyago zimepita.

Kwa upande mwingine hii ni neema kwa wamiliki wa magazeti,kwani sasa mauzo lazima yapae juu
 
wanawapumbaza waTZ washajua TBC ipo mikoa yote hadi vijijini kabisaaaaaa,.....
so wanataka kuwaaminisha zaidi watu wa vijijini jpm mpiga kazi kumbe buree,...
na hii nahis watasucced axee,...
dahh inaboa ndgu yangu,...
mui kwangu huwa tbc haishiki na pia siangalii wangefanya kuifuta mojakwa moja haina tija sasa kwa taifa yaan tv ya taifa ishindwe kuonyesha bunge ila ionyeshe

chereko
harusi tena live
na zile tamthilia za kichina hahahahahahah hii nji ni ya ajabu saaaaaaaaaaaana
 
Mh magufuli, Rais wa JMT,watanzania tumekuchagua, hii ni baada ya watu wengi walionyesha kuwa na Imani na wewe, lakini umeingia ikulu na tumeendelea kukuunga mkono.
Mengi yameendelea kujiri ikiwemo utumbuaji wa majipu . na wengi tukaendelea kuwa na wewe,

Salaleh....... Ghafla leo ametokea nape nauye Waziri wa Habari, amepiga marufuku TBC kuonyesha vikao vya bunge live.
Kisingizio eti kubana matumizi.
Ghafla akaibuka chenge, (ambaye kwa wananchi tulio wengi yeye ni JIPU ndani ya chama)
Amekomelea msumari kwenye jeneza kwa kukataa hoja ya zzk Ili kulijadili hili akimlazimisha zitto kumsomea kufungu cha bunge kinachompa Mwenyekiti wa bunge kukubali au kukataa hoja Rasmi ya mbunge kutokana na jambo husika.

My take.
TBC ni chombo cha umma kinachoendeshwa kwa kodi za watanzania wote, bila kujali tofauti zao kiitikadi.

Ni haki ya kila mtanzania kupata Habari muhimu zinazohusu masuala nyeti ya kitaifa, iwe za kimaendeleo, kiuchumi, kisiasa na pia matukio mbalimbali yanayojiri nchini.

Ni wajibu wa chombo cha Habari kumfikishia mlaji wa Habari, ambaye ni mwana nchi. Taarifa za Habari na matukio kwa uhalisia wake bila kupindisha UKWELI.

Isipokuwa kwa vyombo vya Habari vya binafsi, havilazimiki kuyafanya Yale ambayo yanakuwa nje ya uwezo wao kibajeti.
Na ndio maana TBC inasimama kama chombo cha umma kwa maslahi mapana kitaifa, ikiwa pia ni sehemu ya serikali kuwafikia wananchi wake..

Serikali inapaswa kuhakikisha inakipatia chombo hiki fedha za kutosha kujiendesha kama ruzuku yake, kulingana na sheria inavyotamka..

Vikao vya bunge la nchi yoyote ile duniani, vinabaki kuwa muhimu sana kwa sababu nyingi muhimu.

Ni sehemu pekee mpiga kura anapopata wasaa wa kuchambua masuala mbalimbali ya kitaifa iwe, kisiasa uchumi na maendeleo.
Ni sehemu pekee mwananchi anapopata wasaa wa kuijua mipango na mikakati mbalimbali ya kimaendeleo kutoka kwenye serikali yake.

Lakini pia muhimu zaidi ni kwamba wapiga kura tunapata Fursa ya kuwapima wawakilishi wetu bungeni. Na kujua kwa UWAZI kama wanatuwakilisha kama tulivyotarajia wakati tukichukua maamuzi ya kuwapigia kura huko majimboni. Naomba nihitimishe kwa maswali haya.

Je kwa uamuzi huu wa NAPE leo bungeni, Je ni maamuzi ya pamoja ya baraza la Mawaziri?
(Kama jibu ni Ndio)
Je?
Serikali haikuona umuhimu wa kutafuta fungu lingine Ili kuhakikisha TBC inatimiza wajibu wake kisheria?

Kama serikali inapata fedha za kuvipatia vyama vya siasa ruzuku kila mwezi inakuwaje kwa TBC?

Je zinaelekezwa wapi fedha ambazo serikali ya JPM, imetutangazia wananchi kuokolewa hivi karibuni tangu imeingia madarakani?

Je kwa mfumo huu serikali ya CCM haioni Kwamba inajichimbia shimo kubwa la Ufa Kati yake na wapiga kura na watanzania kwa ujumla?

Je hamuoni kwamba mnaibeba UKAWA bila kujijua?

Kuna nini kinachotakiwa kufichwa wananchi tusishuhudie live kutoka bungeni???

Je Rais JPM, anayajua maamuzi haya pale mnapoyajadili kabla hamjayaleta bungeni?

Tumetahadharisha sana watanzania kuhusu JPM na chama chake CCM.

Au hii ndio mikakati ya kuanza kumchonganisha JPM na wapiga kura wake?

Mko wapi washauri wa Rais kwenye hili?

Naomba wanabodi tuchangie kwa kina hili suala ni la kitaifa zaidi kuliko kiitikadi karibuni...
MUNGU ibariki Tanzania.
1453890622746.jpg
 
haijawahi kutokea binadamu mwenye akili timamu akaogopa kivuli chake mwenyewe isipokuwa kichaa ndiye awawezae kuogopa kivulichake chake mwenyewe

Aswaaaaa hii ndo tabia ya KUBENEA!
 
Aisee hii haijakaa sawa hata kidogo,,,na inaitaji kujichetua akili kutokulipinga hili. TUTAMKUMBUKA KIKWETE HAKYAMUNGU. ,,BALAA HILI HAKYA NANI,,YARAB TUONDOLEE ILI JANGA,,,,NAHISI INAKOENDEA HATA MITANDAO KM JF maybe ikaja kufungiwa,,,, ,,,we remember Jk
Safia sana watu tufanye kaze. Habari ya bunge Usikuuuu!!! Safi sana mambo ya kila mtu kufanya chochote anachotaka yamepitwa na wakati sasa ni kazi tuuuu! Asnte Mh. magufuli! Pole waliokuwa na nafasi ya kuangalia Bun ge mchana!
 
Matangazo ya nini haya ndiyo yamefanya wabunge wengi wamejichetua kama kuku.
 
Kuna maneno mawili ya kiingereza ambayo ni personal na private. Maneno haya kwa kiswahili hutafsiriwa kama binafsi. Vyombo vya habari vya binafsi vimekengeuka kutoka kuwa binafsi kwa maana ya "private" hadi kuwa binafsi kwa maana ya "Personal". Lakini si vyombo vya binafsi tu bali hata vyombo vya umma, navyo vimekengeuka kutoka kuwa public media hadi kuwa personal media.

Suala hili limejidhihirisha bayana katika Bunge la 11 ambapo wananchi wamenyimwa haki yao ya msingi ya kuwaona wabunge wao wakichangia hotuba ya Mh Rais Magufuri. Vyombo hivi vimesahau wajibu walio nao kwenye jamii. Ni vizuri Mh Nape akatabua wajibu wa msingi wa vyombo hivi na vinawajibika kwa nani.

Serikali ya awamu ya tano inachotaka kukifanya ni sawa na mtu mwenye mgahawa alazimishe wateja kula chakula anachotaka na kukipenda yeye. JARIBIO hili ni Hatari na halitafanikiwa
 
Watu kama Mimi tulimchagua Magufuli kwa matumaini makubwa sana. Mpaka sasa sikuwa nimeona kasoro kubwa ya serikali ya Rais Magu. Iwe bomoa bomoa au issue ya Zanzibar. Yote nilipuuzia. Lakini "Kuzima Matangazo ya TBC" kwa kisingizio cha kubana matumizi si tu ni hoja ambayo haiwezi kuingia akilini bali ni kudidimiza demokrasia.

Je Rais anaweza kusema hajui hili la maamuzi ya Nape? Please Please mpendwa Rais hujachelewa. Turudishie matangazo yetu "Live". Kama ni billioni nne ni kodi yetu. Na kama eti tunakuwa kazini hata huko tunafuatilia na wengine tumejiajiri. Kuchuja Matangazo ni kurudi Miaka kumi nyuma alipotutoa Mh. Kikwete!!!

Tunakupenda sana lakini huwezi kuwa Malaika. Waache wananchi wajue udhaifu na mafanikio ya serikali yako. Itakusaidia na wewe kujipima na kujirekebisha na kusonga mbele.
 
Hili ni pigo na matusi kwa watanzania na walipa kodi wa nchi hii...hii inaonyesha ni jinsi gani watanzania tulivyo na utawala dhaifu usiojali haki za raia wake.......
Hii inaenda kinyume na katiba ya nchi......

Au ndio kusema hicho watakachokuwa wanakijadili huko bungeni sisi hakituhusu...na kama hakituhusu tuliwachagua wanini na hicho wanachokijadili huko bungeni ni kwa manufaa ya nani...,,?

Huu aina ya udikteta unaofanywa ndani ya nchi inayojinadi kuwa ni ya kidemokrasia....

Shame on you.....

Lakini hakuna marefu yasiyo na ncha....
 
Hili ni pigo na matusi kwa watanzania na walipa kodi wa nchi hii...hii inaonyesha ni jinsi gani watanzania tulivyo na utawala dhaifu usiojali haki za raia wake.......
Hii inaenda kinyume na katiba ya nchi......

Au ndio kusema hicho watakachokuwa wanakijadili huko bungeni sisi hakituhusu...na kama hakituhusu tuliwachagua wanini na hicho wanachokijadili huko bungeni ni kwa manufaa ya nani...,,?

Huu aina ya udikteta unaofanywa ndani ya nchi inayojinadi kuwa ni ya kidemokrasia....

Shame on you.....

Lakini hakuna marefu yasiyo na ncha....


Watatuonyesha Usiku baada ya kupitia na kujiridhisha.


CCM Hoyeeeeeeerrr!!
 
mui kwangu huwa tbc haishiki na pia siangalii wangefanya kuifuta mojakwa moja haina tija sasa kwa taifa yaan tv ya taifa ishindwe kuonyesha bunge ila ionyeshe

chereko
harusi tena live
na zile tamthilia za kichina hahahahahahah hii nji ni ya ajabu saaaaaaaaaaaana
tatizo linakuja wapi unajua flora msoffe
TV zingine zote zipo connected na tbc soni shida,...
Lissu wangu mie ntaona wapi tena hojaaa zakee mieeeeeeeeeeeee dahhh
 
Nilitegemea vyombo vya habari kususia kuandika habari za serikali.Na watanzania kususia kununua Magazeti ya serikali na vijarida vya CCM,ambavyo vinaandika yale tu wanayopenda yaandikwe.Hawataki kuandika kibaya ,wanataka kusifia hawajui kwamba JPM hahitaji SIFA bali kusaidiwa ili kuendelea kutumbua MAJIPU.Na ili kutumbua MAJIPU magazeti lazima waandike wasiyoyapenda Watawala,ambayo ndiyo yatasaidia kuenelewa na kumuwezesha JPM kufanya kazi nzuri zaidi.
 
Only in Tanzania

Harusi inapewe full coverage

Bunge no no tunapunguza matumizi
 
Wasio kuwa na lakufanya kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana ajira yao kuangalia runinga tu kwa kisingizio eti bunge imekula kwao
Na kutafuta umaarufu kipitia kuuza sura bungeni nao imekula kwao tutashuhudia wabunge hata kuchangia hoja wataacha kisa hawaonekani kwenye luninga
Watu wafanye kazi
 
Inabidi tumwombee JPM...............Ili Mwenyezi Mungu amuepusha na WABUNGE wanafiki
 
Back
Top Bottom