Mh magufuli, Rais wa JMT,watanzania tumekuchagua, hii ni baada ya watu wengi walionyesha kuwa na Imani na wewe, lakini umeingia ikulu na tumeendelea kukuunga mkono.
Mengi yameendelea kujiri ikiwemo utumbuaji wa majipu . na wengi tukaendelea kuwa na wewe,
Salaleh....... Ghafla leo ametokea nape nauye Waziri wa Habari, amepiga marufuku TBC kuonyesha vikao vya bunge live.
Kisingizio eti kubana matumizi.
Ghafla akaibuka chenge, (ambaye kwa wananchi tulio wengi yeye ni JIPU ndani ya chama)
Amekomelea msumari kwenye jeneza kwa kukataa hoja ya zzk Ili kulijadili hili akimlazimisha zitto kumsomea kufungu cha bunge kinachompa Mwenyekiti wa bunge kukubali au kukataa hoja Rasmi ya mbunge kutokana na jambo husika.
My take.
TBC ni chombo cha umma kinachoendeshwa kwa kodi za watanzania wote, bila kujali tofauti zao kiitikadi.
Ni haki ya kila mtanzania kupata Habari muhimu zinazohusu masuala nyeti ya kitaifa, iwe za kimaendeleo, kiuchumi, kisiasa na pia matukio mbalimbali yanayojiri nchini.
Ni wajibu wa chombo cha Habari kumfikishia mlaji wa Habari, ambaye ni mwana nchi. Taarifa za Habari na matukio kwa uhalisia wake bila kupindisha UKWELI.
Isipokuwa kwa vyombo vya Habari vya binafsi, havilazimiki kuyafanya Yale ambayo yanakuwa nje ya uwezo wao kibajeti.
Na ndio maana TBC inasimama kama chombo cha umma kwa maslahi mapana kitaifa, ikiwa pia ni sehemu ya serikali kuwafikia wananchi wake..
Serikali inapaswa kuhakikisha inakipatia chombo hiki fedha za kutosha kujiendesha kama ruzuku yake, kulingana na sheria inavyotamka..
Vikao vya bunge la nchi yoyote ile duniani, vinabaki kuwa muhimu sana kwa sababu nyingi muhimu.
Ni sehemu pekee mpiga kura anapopata wasaa wa kuchambua masuala mbalimbali ya kitaifa iwe, kisiasa uchumi na maendeleo.
Ni sehemu pekee mwananchi anapopata wasaa wa kuijua mipango na mikakati mbalimbali ya kimaendeleo kutoka kwenye serikali yake.
Lakini pia muhimu zaidi ni kwamba wapiga kura tunapata Fursa ya kuwapima wawakilishi wetu bungeni. Na kujua kwa UWAZI kama wanatuwakilisha kama tulivyotarajia wakati tukichukua maamuzi ya kuwapigia kura huko majimboni. Naomba nihitimishe kwa maswali haya.
Je kwa uamuzi huu wa NAPE leo bungeni, Je ni maamuzi ya pamoja ya baraza la Mawaziri?
(Kama jibu ni Ndio)
Je?
Serikali haikuona umuhimu wa kutafuta fungu lingine Ili kuhakikisha TBC inatimiza wajibu wake kisheria?
Kama serikali inapata fedha za kuvipatia vyama vya siasa ruzuku kila mwezi inakuwaje kwa TBC?
Je zinaelekezwa wapi fedha ambazo serikali ya JPM, imetutangazia wananchi kuokolewa hivi karibuni tangu imeingia madarakani?
Je kwa mfumo huu serikali ya CCM haioni Kwamba inajichimbia shimo kubwa la Ufa Kati yake na wapiga kura na watanzania kwa ujumla?
Je hamuoni kwamba mnaibeba UKAWA bila kujijua?
Kuna nini kinachotakiwa kufichwa wananchi tusishuhudie live kutoka bungeni???
Je Rais JPM, anayajua maamuzi haya pale mnapoyajadili kabla hamjayaleta bungeni?
Tumetahadharisha sana watanzania kuhusu JPM na chama chake CCM.
Au hii ndio mikakati ya kuanza kumchonganisha JPM na wapiga kura wake?
Mko wapi washauri wa Rais kwenye hili?
Naomba wanabodi tuchangie kwa kina hili suala ni la kitaifa zaidi kuliko kiitikadi karibuni...
MUNGU ibariki Tanzania.