Mr Suggestion
JF-Expert Member
- May 2, 2011
- 605
- 312
Kwani si uchangie tu mjadala wa mwenzako? Kwani ni lazima uanzishe mada?
Lizaboni nipe maoni yako mwana!!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani si uchangie tu mjadala wa mwenzako? Kwani ni lazima uanzishe mada?
dahhh dictatorial ruleWameamua kutuziba Macho na Masikio wakiwa na lengo la kuendelea kutupumbaza.
Wanasahu kuwa "Information Is Power".
Bunge ni muhimu kufanya vikao vyake, siyo kwa kuliangalia, Wabunge wasitafute tu umaarufu kwenye kutazamwa wajikite kwenye hoja.Bunge sio muhim,tena ? bunge ni kwa muda mfupi tu .....tulienda hatua elfu mbele tunarudi nyuma hatua elfumbili.....uhuru wa habari= tu maendeleo ,kama hakuna uhuru wa habari wachache wataendelea neemeka subiri muone madikteta wachache watakavyo itafuna nchi kwa kisingizio cha hapa kazi tu
Karestructuringuli za Mawaziri, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, ametangaza kwamba, Kuanzia tarehe 26 Januari mwaka 2016, TBC1 haitaonesha tena Mikutano ya bunge live kutokana na gharama za kuonesha live kufikia bilioni nne kwa mwaka.
Badala yake TBC1 watarekodi na kuonesha katika kipindi maalum usiku kuanzia saa nne hadi saa tano.
Hii itanyima wanchi fursa ya kuona kinachoendelea Bungeni.
=========
Mheshimiwa spika,
Naomba kutoa kauli ya serikali kuhusu TBC kutangaza moja kwa moja vikao vya majadiliano ya bunge. Mheshimiwa spika, shirika la utangazaji Tanzania, TBC lilianza kurusha moja kwa moja matangazo ya vikao vya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2005. Kabla ya kuanza kurusha moja kwa moja, TBC wakati huo televisheni ya taifa ilikuwa inarekodi matukio yote ya bunge na kurusha usiku katika vipindi maalumu vilivyojulikana kama bungeni leo kwa maana ya yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika.
Baada ya kuanza kwa utaratibu wa kuanza kurusha matangazo moja kwa moja mwaka 2005, gharama za kufanya kazi hio zimekua zikipanda kwa kasi hadi kufikia Tshs. bilioni 4.2 kwa mwaka kwa maana ya mikutano minne ya bunge.
Shirika limekuwa likigharamia kwa sehemu kubwa matangazo hayo kwa kutumia mapato yake yanayotokana na matangazo madogo madogo ya biashara, ifahamike kuwa asilimia 75 ni vipindi vingi vinavyolenga kutoa elimu kwa umma na asilimia 25 ni burudani.
Mheshimiwa spika, kutokana na hali hii, TBC imeona ni busara kubadilisha mfumo wa utangazaji wa shughuli za bunge ili kukabiliana na kupanda kwa gharama za uendeshaji, hivyo basi, TBC imeona ni busara kuanzia mkutano huu wa bunge iwe inarusha baadhi ya matangazo ya bunge moja kwa moja yaani live ikiwa ni njia ya kubana matumizi.
Chini ya utaratibu huu, TBC itahakikisha kuwa, baadhi ya matukio ya matukio ya bunge yatarushwa moja kwa moja na mengine kurekodiwa na kuandaliwa kipindi maalum kitakachoitwa leo katika bunge. Kipindi hiki kitakua na mambo yote muhimu yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika. Kipindi hichi kitakuwa kinarushwa kuanzia saa nne usiku hadi saa tano usiku.
Na mheshimiwa spika kipindi hicho kimeanza jana na tayari baadhi ya wananchi wameonyesha kuridhishwa na utaratibu huu na kuwa na kipindi maalum usiku kikishughulikia shughuli za bunge, mheshimiwa spika, uamuzi huu utapunguza gharama za uendeshaji wa shirika na pia kupitia kipindi cha leo katika bunge, watanzania walio wengi watapata nafasi ya kufahamu yaliyojiri bungeni kwani wakati bunge linaendelea mijadala yake, watanzania walio wengi huwa wanakua na kazi za kiofisi au zingine za ujenzi wa taifa kwa mahali walipo.
Mheshimiwa spika nakushkuru.
ukiona vyaelea ujue vimeundwa ndugu yanguWananchi wale tu hata wanaofanya kazi na kulipa PAYE tunaweza kutolewa hata shilling Mmoja kulipia matangazo ya Bunge Hivi nape huwaga anamka toka usingizini ati wananchi tumeafiii mlitupa tupige kura ya maoni katika uamuzi huuu kwani Nape unaleta mzaha kwenya mambo ya msingi Rais JPM huyu ndio umeona anafaaaa kwenye wizara ya Habari au ndio mbinu mbadala wa kuuwa vyombo vya habari mbona mnakinzana saaana na hali ahalisi ya ulimwengu wenzenu Media ndio kitu muhimu kuwaelimisha wananchi nyie mnakifungia na kukipa mashariti ya ajabu saaana
Duh kwahiyo kwenye kampeni watu wanataka umaarufu ndo maana wanaonyeshwa?? Tanzania tuendako ni kubaya maona udikteta huo...Bunge ni muhimu kufanya vikao vyake, siyo kwa kuliangalia, Wabunge wasitafute tu umaarufu kwenye kutazamwa wajikite kwenye hoja.
mmmh...TV tunayokatwa kodi kuendesha...imelemewa na gharama!tuibinafisishe tujue moja!
Kama bunge siyo muhimu hivyo basii lifutwe tu kusiwe na bunge nchi hiiKipindi cha Kampeni kilikuwa ni muhimu sana, siyo tu kwa mikutano ya CCM bali ya vyama vyote. Sasa hivi hakuna sababu ya kutumia gharama kama hakuna ulazima.
Si kweli, star tv wanatusha kivyao, hawapitii tbc!Star tv nao sidhani kama wangeweza kurusha, maana na wao si walikuwa wanapata feed kutoka TBC.