TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Huyo jamaa hakustairi kuingia bungeni anafanya siasa pasipostairi kamavip waifunge kabisa iyo bajet waliokuwa wanawapa iperekwe ITV au AZAM TV
 
Sasa ajira zisizo rasmi za humu jf zipo mashakani. Kama bunge halitakuwa live vijana wengi watapotea humu jukwaani.
 
Bunge sio muhim,tena ? bunge ni kwa muda mfupi tu .....tulienda hatua elfu mbele tunarudi nyuma hatua elfumbili.....uhuru wa habari= tu maendeleo ,kama hakuna uhuru wa habari wachache wataendelea neemeka subiri muone madikteta wachache watakavyo itafuna nchi kwa kisingizio cha hapa kazi tu
Bunge ni muhimu kufanya vikao vyake, siyo kwa kuliangalia, Wabunge wasitafute tu umaarufu kwenye kutazamwa wajikite kwenye hoja.
 
Karestructuringuli za Mawaziri, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, ametangaza kwamba, Kuanzia tarehe 26 Januari mwaka 2016, TBC1 haitaonesha tena Mikutano ya bunge live kutokana na gharama za kuonesha live kufikia bilioni nne kwa mwaka.

Badala yake TBC1 watarekodi na kuonesha katika kipindi maalum usiku kuanzia saa nne hadi saa tano.

Hii itanyima wanchi fursa ya kuona kinachoendelea Bungeni.
=========



Mheshimiwa spika,
Naomba kutoa kauli ya serikali kuhusu TBC kutangaza moja kwa moja vikao vya majadiliano ya bunge. Mheshimiwa spika, shirika la utangazaji Tanzania, TBC lilianza kurusha moja kwa moja matangazo ya vikao vya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2005. Kabla ya kuanza kurusha moja kwa moja, TBC wakati huo televisheni ya taifa ilikuwa inarekodi matukio yote ya bunge na kurusha usiku katika vipindi maalumu vilivyojulikana kama bungeni leo kwa maana ya yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika.

Baada ya kuanza kwa utaratibu wa kuanza kurusha matangazo moja kwa moja mwaka 2005, gharama za kufanya kazi hio zimekua zikipanda kwa kasi hadi kufikia Tshs. bilioni 4.2 kwa mwaka kwa maana ya mikutano minne ya bunge.

Shirika limekuwa likigharamia kwa sehemu kubwa matangazo hayo kwa kutumia mapato yake yanayotokana na matangazo madogo madogo ya biashara, ifahamike kuwa asilimia 75 ni vipindi vingi vinavyolenga kutoa elimu kwa umma na asilimia 25 ni burudani.

Mheshimiwa spika, kutokana na hali hii, TBC imeona ni busara kubadilisha mfumo wa utangazaji wa shughuli za bunge ili kukabiliana na kupanda kwa gharama za uendeshaji, hivyo basi, TBC imeona ni busara kuanzia mkutano huu wa bunge iwe inarusha baadhi ya matangazo ya bunge moja kwa moja yaani live ikiwa ni njia ya kubana matumizi.

Chini ya utaratibu huu, TBC itahakikisha kuwa, baadhi ya matukio ya matukio ya bunge yatarushwa moja kwa moja na mengine kurekodiwa na kuandaliwa kipindi maalum kitakachoitwa leo katika bunge. Kipindi hiki kitakua na mambo yote muhimu yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika. Kipindi hichi kitakuwa kinarushwa kuanzia saa nne usiku hadi saa tano usiku.

Na mheshimiwa spika kipindi hicho kimeanza jana na tayari baadhi ya wananchi wameonyesha kuridhishwa na utaratibu huu na kuwa na kipindi maalum usiku kikishughulikia shughuli za bunge, mheshimiwa spika, uamuzi huu utapunguza gharama za uendeshaji wa shirika na pia kupitia kipindi cha leo katika bunge, watanzania walio wengi watapata nafasi ya kufahamu yaliyojiri bungeni kwani wakati bunge linaendelea mijadala yake, watanzania walio wengi huwa wanakua na kazi za kiofisi au zingine za ujenzi wa taifa kwa mahali walipo.

Mheshimiwa spika nakushkuru.

Frankly speaking hii TBC ni taasisi ambayo inahitaji restructuring. Inachekesha kuona TBC 2 ina airtime kuonyesha miziki almost 24 hrs kila siku. I mean, haiingii akilini mfanyakazi wa TV yuko kazini kwa pesa za taxpayers anakaa kuonyesha muziki all the time around all the week. Na wakati huo huo hata TBC 1 nayo ina airtime ya muziki. Kama hawana ubunifu wa vipindi basi ni afadhali wafunge channel moja ili kupunguza gharama za uendeshaji.
 
mmmh...TV tunayokatwa kodi kuendesha...imelemewa na gharama!tuibinafisishe tujue moja!
 
Wananchi wale tu hata wanaofanya kazi na kulipa PAYE tunaweza kutolewa hata shilling Mmoja kulipia matangazo ya Bunge Hivi nape huwaga anamka toka usingizini ati wananchi tumeafiii mlitupa tupige kura ya maoni katika uamuzi huuu kwani Nape unaleta mzaha kwenya mambo ya msingi Rais JPM huyu ndio umeona anafaaaa kwenye wizara ya Habari au ndio mbinu mbadala wa kuuwa vyombo vya habari mbona mnakinzana saaana na hali ahalisi ya ulimwengu wenzenu Media ndio kitu muhimu kuwaelimisha wananchi nyie mnakifungia na kukipa mashariti ya ajabu saaana
ukiona vyaelea ujue vimeundwa ndugu yangu
 
Bunge ni muhimu kufanya vikao vyake, siyo kwa kuliangalia, Wabunge wasitafute tu umaarufu kwenye kutazamwa wajikite kwenye hoja.
Duh kwahiyo kwenye kampeni watu wanataka umaarufu ndo maana wanaonyeshwa?? Tanzania tuendako ni kubaya maona udikteta huo...
 
Asilimia kubwa ya Watanzania wako vijijini na hawana TV wanaendelea na shughuli za kujitafutia maendeleo. Nyie asilimia ndogo mnaona mna haki ya kuitaka serikali ilipe ghrama kubwa ya kurusha Bunge live kwa ajili yenu tu!? Mnataka Magufuli ajaze dawa mahospitalini, ajenge barabara nareli, asomeshe bure nk nk. Akisema msiangalie Bunge kuokoa pesa ili zielekezwe kwenye hayo muhimu mnang'aka! Una hamu ya kuangalia Bunge live chukua likizo nenda bungeni kama kweli ni muhimu sana kuangalia live. Mmeambiwa litaonyeshwa saa 4 usiku! Mnashindwa nn kusuburi kuangalia ucku? Saa hizo ni nzuri za kupumzika na kuangalia TV. Watanzania bwana Magufuli kazi unayo ya kupigana na wasiopenda kazi.
 
Haiwezekani kila maamuzi Rais aombwe ushauri, inakua haina maana ya waziri kuwepo.
Acha watu wafanye wanavyoona inafaa mwisho wa siku kila mmoja ahukumiwe kwa utendaji wake, hatutaki kusikia mambo ya 'oda' kutoka juu.
 
mmmh...TV tunayokatwa kodi kuendesha...imelemewa na gharama!tuibinafisishe tujue moja!



Naangalia TBC hapa nimeona Tangazo kuwa TBC watakuwa wanaonyesha Vipindi Maalumu vya Shughuli za Raisi JPM.


Je! hivi vipindi havitumii fedha?????????!!!"
 
Kipindi cha Kampeni kilikuwa ni muhimu sana, siyo tu kwa mikutano ya CCM bali ya vyama vyote. Sasa hivi hakuna sababu ya kutumia gharama kama hakuna ulazima.
Kama bunge siyo muhimu hivyo basii lifutwe tu kusiwe na bunge nchi hii
 
Huu ni uhuni mkubwa sana. Wanaficha madudu yao wakiogopa wataonekana. Kams sababu ni gharama waruhusu tv nyingine idadi yeyote warushe live. Tv inaendeshwa kwa kodi za wananchi anasema gharama kubwa. Hizo binafsi kama azam na star tv wasemeje. Tbc si inafanya biashara kurusha harusi, hii sio haki kabisa. Ameshindwa kutoa sababu za msingi. Magufuli je atakubaliana na hili? Wananchi hatuna haki ya kuwaona tuliowachagua wakituwakilisha bungeni kama wanatutendea haki. Hata hiyo saa nne wasirushe
 
Nape anadhani cheo chake Ndani ya CCM ni bora kuliko Cheo cha Kuwa Waziri wa Jamhuri ya Muungano
Badala ya kufanya kazi kwa maslahi mapana ya nchi, anafanya kazi kwa maslahi ya CCM
Naunga mkono hoja, kwa hatua hii, nadhani Magufuli kuna haja akaingilia kati kuona kama je HII HATUA YA SERIKALI YA KUZUIA UWAZI, NA KUMINYA INFORMATION ILI WANANCHI WASIJUE YANAYOJIRI KATIKA BARAZA LAO, JE NI KWA MASLAHI MAPANA YA UMMA AU MASLAHI YA KISIASA YA WATU WACHACHE?

Pia Natoa Rai kwa Raisi kujiridhisha je Anataka kuongoza Watu mbumbumbu wasio na taarifa, au anapenda kuongoza watu wenye ufahamu wa nini serikali yao inafanya?

Katika suala la Demokrasia na Uwazi nchi hii imepiga hatua kubwa katika tawala zilizopita, Hatutegemei Serikali ya Magufuli itupeleke hatua nyuma!, WE WANT DEMOCRATIC AND TRANSPARENCY PROGRESS, NOT RECESS!
 
Alianza na MAWIO tukanyamaza
Amekuja na TBC tukinyamaza,
Atakuja JamiiForums
Hapo ndipo tutalia na kusaga meno
SAY NO CENSORSHIP
 
Halafu jpm kama mnafiki vile kumuhusisha Mungu na matendo yake tofauti kabisa mimi ndo maana huyu Mungu wa TB joshua wala simuamini.watu wamechota bil 300 tena wachache leo bil 4 kwa mwaka watanzania waone bunge ni kero. Pesa ngapi walilipana bunge la katiba na haikupatika hebu ifike Mahali waache kutucheze leo ccm ndo ya kuonea uchungu pesa ya watanzania .lake oil tu akilipa ni miaka 2 tunapata bunge.achana na twiga walioiba na sasa yupo albino olé wenu apotee tena
 
Zitto Kabwe


Hoja ya gharama ni hoja
dhaifu sana katika kuzuia
mikutano ya Bunge kurushwa
'live'. Demokrasia ni gharama
 
Back
Top Bottom