Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wengi wanao lalamika ni wafuasi wa UKAWA walio waandaa wabunge wao kugeuza bunge sehemu ya kujipatia umaarufu na kuleta uhuni.
Hongera sana Mh Nape..
Si kweli, star tv wanatusha kivyao, hawapitii tbc!
Okey, vipi Azam tv nao?
yelewiiiiiiiiiiiiiiiii sasa tutarajie kuona harusi live kwa wingi
hivi itv star na wengine ambao wanajitegemea wanafanyaje aisee hii wizara ni jipu.. badala kufanya ubunifu wapate jinsi ya kutuonyesha jambo hili muhimu kwa taifa wanaleta longolongo piga chini muhusika
Labda inatakiwa hivyo kuwa watangaze kupitia tbc ila mpaka sasa azam na star tv wanarusha kivyao, jana baada ya tbc kukata matangazo ya live ya bunge dk tatu baadae star tv wakakata! Walianza azam kukata matangazo, hivyo suala la gharama ni uongo.Well, am not sure now... Kama nakumbuka kuna wakati kulikuwa na mjadala kuhusu nani arushe matangazo ya bunge, then ikawa kwamba indepenndent tv zilinyimwa kibali cha kurusha kivyao?
....leo umenichekesha sana aisee!!!
Penye ukakasi ni hapo kwenye "idol" nadhani urekebishe ulikuwa unamaanisha "idle".
But all in all watz kwa sasa wanapelekwapelekwa kama circus wakisubiri matukio mara tezi dume, mara Eritrea...and the list is long. Fanyeni kazi, tafuteni hobby kama anavyoshauri mdau hapo, kama ni kutazama bunge nenda dodoma kabisa! Ila hii tabia ya kuwa cry babies kutaka TV iwashwe mpate cha kuongea itatumaliza!
Waingereza walituharibu sana, tumekuwa wazungumzaji kuliko kuwa watendaji, jambo dogo linakuzwa kuwa kubwaaa...ndio maana EPL ina publicity kuubwa wakati hamna talent kiivyo ni hichi kihulka cha kuwa na uzungumzaji zaidi ya kuwekeza kwenye the actual work.
na alivyoagiza Pesa za sherehe za Bunge zikanunue vitanda hakuingilia mhimili mwingine!?Uko sahihi mkuu lakini pia Kuna mihimili mitatu.kuna Bunge,mahakama,na SERIKALI.Hiyo TV ni mali ya Serikali sio ya bunge.Huwezi lazimisha mali za muhimili mwingine zitumikaje na muhimili mwingine.TBC hawalazimiki kisheria kurusha mijadala ya bunge.
na alivyoagiza Pesa za sherehe za Bunge zikanunue vitanda hakuingilia mhimili mwingine!?
huu ni udikteta unasema ??? bilioni zote hizo si bora wapeleke watoto wetu wasome bure zaidi. mnasahau kwamba hapa ni kazi tu. hakuna siasa sahiz. siasa zitarudi tena mwaka 2020. watchout! !Kweli tunaisoma namba,huu ni udikteta wa hali ya Juu..
Katika kauli za Mawaziri, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, ametangaza kwamba, Kuanzia tarehe 26 Januari mwaka 2016, TBC1 haitaonesha tena Mikutano ya bunge live kutokana na gharama za kuonesha live kufikia bilioni nne kwa mwaka.
Badala yake TBC1 watarekodi na kuonesha katika kipindi maalum usiku kuanzia saa nne hadi saa tano.
Hii itanyima wanchi fursa ya kuona kinachoendelea Bungeni.
=========
Mheshimiwa spika,
Naomba kutoa kauli ya serikali kuhusu TBC kutangaza moja kwa moja vikao vya majadiliano ya bunge. Mheshimiwa spika, shirika la utangazaji Tanzania, TBC lilianza kurusha moja kwa moja matangazo ya vikao vya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2005. Kabla ya kuanza kurusha moja kwa moja, TBC wakati huo televisheni ya taifa ilikuwa inarekodi matukio yote ya bunge na kurusha usiku katika vipindi maalumu vilivyojulikana kama bungeni leo kwa maana ya yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika.
Baada ya kuanza kwa utaratibu wa kuanza kurusha matangazo moja kwa moja mwaka 2005, gharama za kufanya kazi hio zimekua zikipanda kwa kasi hadi kufikia Tshs. bilioni 4.2 kwa mwaka kwa maana ya mikutano minne ya bunge.
Shirika limekuwa likigharamia kwa sehemu kubwa matangazo hayo kwa kutumia mapato yake yanayotokana na matangazo madogo madogo ya biashara, ifahamike kuwa asilimia 75 ni vipindi vingi vinavyolenga kutoa elimu kwa umma na asilimia 25 ni burudani.
Mheshimiwa spika, kutokana na hali hii, TBC imeona ni busara kubadilisha mfumo wa utangazaji wa shughuli za bunge ili kukabiliana na kupanda kwa gharama za uendeshaji, hivyo basi, TBC imeona ni busara kuanzia mkutano huu wa bunge iwe inarusha baadhi ya matangazo ya bunge moja kwa moja yaani live ikiwa ni njia ya kubana matumizi.
Chini ya utaratibu huu, TBC itahakikisha kuwa, baadhi ya matukio ya matukio ya bunge yatarushwa moja kwa moja na mengine kurekodiwa na kuandaliwa kipindi maalum kitakachoitwa leo katika bunge. Kipindi hiki kitakua na mambo yote muhimu yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika. Kipindi hichi kitakuwa kinarushwa kuanzia saa nne usiku hadi saa tano usiku.
Na mheshimiwa spika kipindi hicho kimeanza jana na tayari baadhi ya wananchi wameonyesha kuridhishwa na utaratibu huu na kuwa na kipindi maalum usiku kikishughulikia shughuli za bunge, mheshimiwa spika, uamuzi huu utapunguza gharama za uendeshaji wa shirika na pia kupitia kipindi cha leo katika bunge, watanzania walio wengi watapata nafasi ya kufahamu yaliyojiri bungeni kwani wakati bunge linaendelea mijadala yake, watanzania walio wengi huwa wanakua na kazi za kiofisi au zingine za ujenzi wa taifa kwa mahali walipo.
Mheshimiwa spika nakushukuru.
Kumbuka deo ,unaye mjua leo ni kwasababu kipindi chake cha.yale aliyokuwa anafanya bungeni yalirushwa liveNAYASEMA HAYA BAADA YA KUGUNDUA WATANCHI TUNAKOSEA KUWACHAGUA WAWAKILISHI WETU BUNGE ,TUNACHAGUA MAVUVUZELA BUNGENI NA WANAOTAFUTA KUONEKANA BUNGENI ILI KUPATA UMAARUFU MAJIMBONI BADALA YA KUWATUMIKIA WANANCHI,
USHAIDI UPO
MFANO HAKUNA MBUNGE AMBAYE AMEJITOKEZA WAZI KUPELEKA HOJA BINAFSI YENYE MASLAI JIMBONI KWAKE ADI SASA, WENGI BADALA YA KUWATUMIKIA WANACHI MAJIMBONI WAMAJIKITA KUPATA SIFA BUNGENI TU,
NAWAKUMBUSHA,ILI BAADA YA KUONA LEO WABUNGE WENGI AKILI ZAO ZIMEJIKITA KWENYE MATANGAZO YA BUNGE AUBUHI KWA KINGEZO CHA WANANCHI KUWAPA HAKI YAO KURIKO WAO KUTOKUTIMIZA HAKI HIYO YA KUWATUMIKIA IPASAVYO WANANCHI,
MAREHEMU
DEO FILIPO LUNJOMBE ALIYEKUWA MBUNGE WA LUDEWA ALIKUWA MBUNGE MWENYE KUJILIKANA SANA NA HESHIMA KUBWA ALIYOIPATA KWA KUFANYA KAZI NA KUWATUMIKIA WANANCHI WAKE JIMBONI KURIKO KUTENGEMEA UMAARUFU WA KWENYE TV ,USIO NA FAIDA KWA WANANCHI MASIKINI,
WABUNGE WOTE ACHANA NA SIFA ZA KWENYE TV JIFUNZE KWA DEO,