TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Nina wasiwasi Magufuli anaweza kuwa rais wa kwanza Tanzania kuongoza kwa muhula mmoja tu,kwa kasi hii anayokwenda nayo ya kuirudisha nchi kwenye zama za ujima!hata mimi niliyefikiria kumpa kura yangu mwaka 2020 sasa nimeanza kuingiwa na mashaka naye,he might turn out to be the worst President ever,Kikwete will turn out to be the best one ever,time will tell.
 
Nina wasiwasi Magufuli anaweza kuwa rais wa kwanza Tanzania kuongoza kwa muhula mmoja tu,kwa kasi hii anayokwenda nayo ya kuirudisha nchi kwenye zama za ujima!hata mimi niliyefikiria kumpa kura yangu mwaka 2020 sasa nimeanza kuingiwa na mashaka naye,he might turn out to be the worst President ever,Kikwete will turn out to be the best one ever,time will tell.
Ni bahati nzuri kuwa hata wakati huu aliposhinda hukuchangia lolote ktk ushindi wake iwe kwa kura au lolote..ulikuwa unazungusha mikono upande uleeeeeee!!! Na bora ubakk huko maana bado umuhimu wako huku haujaonekana...
Kama mlitegemea kuuza sura kwa matus na migomo isiyo na tija kwa taifa imekula kwenu...Keep it up Magufuli we're behind you!!!!!
 
Kama aliyechaguliwa alipata Zero kidato cha NNE tusitegmee chochote na pia tumalumu aliyemchagua.Na Tujiulize kwanini kuchagua MTU aliefeli na kuforge vyeti vyake???Hata kama ni zawadi Magufuli hatakaa aaminike.Nilidhani Serikali ni a Magroup fuli kumbe serikali ile ile ya CCM
 
Naona hasira ya kutumbuliwa majipu sasa mmeamua kumuhujumu JPM.Mmefanikiwa.Mmeanza na kufuta matokeo, mkabomoa nyumba za watu sasa mmeamua kulufanya Bunge ni muhuri tu.Anachoamua rais ndicho kinafanyika
 
INAWEZEKANA KWA KUTOKUELEWA AU KWA MAKUSUDI WAZIRI WA HABARI ANASHINDWA KUELEWA NINI MSINGI WA TV YA SERIKALI AU YA TAIFA. ILE TV IPO KWA AJILI YA KUWAPA HABARI ZA MATUKIO MBALIMBALI WANANCHI,IKIWA PAMOJA KUONA YALE YANAYOENDELEA BUNGENI. WANANCHI TAYARI WANALIPIA GHARAMA ZA UENDESHAJI WA CHOMBO HICHO MAANA KINATAKIWA KUENDESHWA KWA KODI ZA WANANCHI MAANA NI CHOMBO CHA UMMA.

NAPE ANAPOTAKA KUDANGANYA WATANZANIA KWAMBA KINATUMIA BILIONI 4.2 KWA MWAKA HAKUNA UKWELI HATA KIDOGO,NA HATA HIVYO TV YA TAIFA KUTUMIA PESA KWA LENGO LA KUWAHUDUMIA WANANCHI NI SAWA,MAANA TUMESHATOA KODI ZETU. MBONA YEYE AMEITUMIA TBC KUFAFANUA MAMBO YAKE LIVE NANI KALIPIA HIZO GHARAMA? KAMA KWELI ANAPENDA KUBANA MATUMIZI KWA NINI HAKUREKODI? HAIWEZEKANI TBC TUNAYOIJUA IKAREKODI HABARI ZA BUNGE HALAFU IKAZIFIKISHA KAMA ZILIVYO.KAMA MAGEZETI TU YALIYOKUWA YANAONAKENA WAZI TBC WALISHINDWA KUYASOMA ITAKUWA KAMA WAZIRI MMOJA KAFANYA MADUDU BUNGENI WATASHINDWA KU EDIT? NAPE ANATAKA KUHADAHA WATANZANIA..KAMA KWELI ANA UCHUNGU NA ANATAKA KUBANA MATUMIZI KWANINI WANALAZIMISHA KURUDIA UCHAGUZI ZANZIBAR AMBAO UMETUMIA PESA NYINGI NA UTATUMIA MAMILIONI WAKIRUDIA
 
kitendo cha tbc kutooneshwa live kimenifurahisha sana.
lilikuwa ni jambo lililokuwa linanikera sana kutoa maneno ya hovyo na wajinga watazamaji wanalishangilia pasipokujua mbunge wao anawasaidia nini kwenye jimbo lao
DARASA LAKO LINAJULIKANA WALA HUJAKOSEA
 
kumbuka TBC wanapata ruzuku na inaendeshwa na kodi ya Watanzania.swali hizo galama zinatumika na zinaenda wapi? hapo kuna jipu na Nape usiwarudishe watanzania kwenye zama za kale.

swissme
hizi gharama TBC wameanza lini kuzilipia wenyewe.nakumbuka Anne Makinda aliwahi kuwa kemea TBC wakati Fulani kwamba wamelipwa pesa na serikali hivyo nikosa kutokurusha live kutoka bungeni .alikuwa akijibu hoja ya Mbowe bungeni.tena ni wakati ule upinzani wakidai wapinzani wakiongea TBC inakata matangazo.lakini sishangaii kwani Nape yuko hapo kuziba sehemu zote zilizo kuwa zinaiumeza ccm kupitia media .bila kusahau katibu muenezi Wa ccm ndio huyo huyo (waziri)katibu muenezi wataifa
 
kumbuka TBC wanapata ruzuku na inaendeshwa na kodi ya Watanzania.swali hizo galama zinatumika na zinaenda wapi? hapo kuna jipu na Nape usiwarudishe watanzania kwenye zama za kale.

swissme
Bajeti inatengwa lakini hakuna pesa inatolewa. Jenga tabia ya kusikiliza hoja kuliko kukimbilia kupost hapa
 
Nape + tbc ni jipu lililoivaaa sanaaa
Sio jipu tuu.wanaiua kabisa TBC .Kwa maslahi ya ccm .kwangu Mimi ilikuwa na angali TBC wakati wa bunge tuu.kwa maana hiyo sasa sintaangalia tena.kama gazeti la uhuru
 
mbona wanazidi kuipoteza tbc kwenye ramani ya vyombo vya habari. maana walikuwa wanapata watazamaji kwenye bunge tu
 
Kama lengo lao ni kukwepa gharama za uendeshaji, kwanini hawataki vyombo vingine binafsi vionyeshe bunge moja kwa moja?
 
Swali kwa TBC na Bunge:

1. Bajeti ya Wizara hii fedha hizi zilipitishwa?
2. Kama fedha zilipitishwa na waziri amelalamika kwamba challenge ni kwamba gharama za kurusha matangazo haya zimekuwa zikipanda kila mwaka, je wameshajaribu TV stations nyingine waone gharama zao?
3. Kwa utaratibu ambao waziri ameelezea ina maana bado waandishi na equipments za TBC zitabaki Dodoma kwa ajili ya kurekodi vipindi vyote vya bunge halafu wachague nini cha kurusha kwenye kipindi hicho cha saa nne usiku- Wanasave shilingi ngapi ukilinganisha na utaratibu wa awali?
 
kumbuka TBC wanapata ruzuku na inaendeshwa na kodi ya Watanzania.swali hizo galama zinatumika na zinaenda wapi? hapo kuna jipu na Nape usiwarudishe watanzania kwenye zama za kale.

swissme
Ni bora kufanya utafiti kidogo maana siku hizi ruzuku ni kama hazipo kabisa. Kwa sasa mashirika mengi ya umma yanatakiwa kujiendesha bila kutegemea ruzuku toka serikalini. Kwa hali kama hiyo TBC itabidi ibane matumizi hakuna jinsi. Maoni yangu ni kuwa Wabunge wapunguziwe marupurupu ili fedha hizo zigharamie suala hili
 
kama hali sio nzuri tbc kifedha mpaka kushindwa kurusha matangazo live, hawakuwa na bajeti ya mwaka huu ambao haujaisha? hawawezi kuomba vituo vyenye pesa virushe live? au hatutakiwi tuone live mpaka tuvalishwe miwani!! najiuliza tu.....
 
Back
Top Bottom