TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Kwa nchi za jirani hali huwa inakuwaje, wanarusha live au kurecord
 
Mimi naona ni maamuzi ya busara sana tena sana maana kuna watu hakuna jambo la msingi lakini linaoneshwa live hivyo pesa inatumika bure tuu!
Pia kuonesha bunge live kulikuwa kuna changia vurugu bungeni maana kuna watu wanaligeuza bunge kama sehemu ya kujipatia umaarufu na wengine wanaona ndio sehemu ya kufanyia uhuni!

Sioni sababu ya msingi ya kuonesha bunge live ikiwa kuna kipindi jioni cha bungeni leo!

Mimi napendekeza hata TV binafsi zipigwe marufuku kuonesha bunge live na wafate maelekezo ya TBC na wawe wanachukua kupitia TBC!

Najua hili ni pigo kwa UKAWA kwani wamezoea kufanya vurugu wakijua wanaonekana live.....

Mkuu wangu, nakuuliza tena, kwanini unaaandika usichokiamini, na kwanini umeamua kujidhalilisha hivi?

Kazi ya TBC ni nini basi? Kama taarifa ya habari hai-balance?

Live Coverage hai- balance?

Matangazo hafifu kutokana na wananchi kutoiamini!

Kweli leo unasapoti TV ya taifa irushe harusi LIVE lakini isirushe bunge moja kwa moja?

Kwa hili tuache ushabiki mkuu, Mambo ya UKAWA na CCM yasipewe nafasi hapa, Wizara ya habari imepotoka!!!!!

Nategemea Mkurugenzi mkuu wa TBC na Waziri wajiuzulu usiku huu!
 
Safi kabisa. Hizo pesa zipelekwe kwa watoto wetu wanaokaa chini na wamama wanajifungulia njiani kwa kukosa huduma za dispensary au ambulance za kutosha. Pia zingine ziongezwe kwenye changamoto ya elimu na maji.

Queen Esther

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na
Michezo, Nape Moses Nnauye, amesema
Televisheni ya Taifa imeacha kurusha LIVE
kipindi cha Bunge kuanzia jana ili kubana
matumizi. Na itakuwa ikirekodi baadhi ya
matukio na kuonyesha usiku.

Kama mtanzania, unadhani unatendewa
haki?
 
Hii hoja ya kurusha bunge live au la imeanza kwenye Serikali ya awamu ya nne. Tatizo watu ni wasahaulifu sana.

Queen Esther

Hakuna Bora ndani ya CCM,
Huu upuuzi unaofanywa sasa na Magufuli usikufanye umuone Kikwete ni mzuri.
Kikwete is the Gross of the Gross.
Na bado huu ni Mwanzo tu.
 
Serikali imechukuwa uamuzi sahihi kabisa, ilikuwa inafikia wakati unakwenda ofisini kupata huduma wafanyakazi wamekodoa kwenye luninga wanaangalia Bunge, Nasema SAFI SANA NAPE!
Kama ni hivyo basi hata kula na kujisaidia ipigwe marufuku kwa sababu inafika wakati unaenda ofisini unaambiwa muhusika ameenda kula au kujisaidia. Sisi hatuna haja ya kuangalia, tunataka kusikia. Jee redio itakuwa wazi? Editing ya saa moja wakati bunge linaendelea kwa masaa 10, umeiona wapi hiyo? Watarusha nini na kuwacha nini? Ni mbinu ya kuzuwia wananchi wasione na kusikia michango ya wapinzani tu. Bilioni 4 ni makusanyo ya TRA ya masaa 2 na nusu tu. Kama TBC haiwezi basi muwape right hiyo TV inayoweza kurusha live. Kuna opportunities za matangazo ya biashara yanayoweza kuzidi mara mbili ya gharama kama hiyo nafasi itatumiwa ipasavyo
 
Safi kabisa. Hizo pesa zipelekwe kwa watoto wetu wanaokaa chini na wamama wanajifungulia njiani kwa kukosa huduma za dispensary au ambulance za kutosha. Pia zingine ziongezwe kwenye changamoto ya elimu na maji.

Queen Esther
Zile bilions za NIDA, bandari zifanye nn? shirikisha ubongo wako wewe
 
Yes ni sawa kabisa, hatuoni umuhimu wake zaidi ya mipasho tu na kuuza sura. bora hizo fedha nikanunue madawati au kuimarisha huduma nyingine ya jamii
 
Mmmmmhhhhh hizi mambo za Politics vs Political ideology inakuwaga ni matatizo pale watu tunapotaka Transparency na Efficiency ya Gvt kuwa in PUBLIC.
 
Ilikuwa ya Mwanachama wa CCM. hivi live coverage ya Nape nani analipia???
 
Mimi naona ni maamuzi ya busara sana tena sana maana kuna watu hakuna jambo la msingi lakini linaoneshwa live hivyo pesa inatumika bure tuu!
Pia kuonesha bunge live kulikuwa kuna changia vurugu bungeni maana kuna watu wanaligeuza bunge kama sehemu ya kujipatia umaarufu na wengine wanaona ndio sehemu ya kufanyia uhuni!

Sioni sababu ya msingi ya kuonesha bunge live ikiwa kuna kipindi jioni cha bungeni leo!

Mimi napendekeza hata TV binafsi zipigwe marufuku kuonesha bunge live na wafate maelekezo ya TBC na wawe wanachukua kupitia TBC!

Najua hili ni pigo kwa UKAWA kwani wamezoea kufanya vurugu wakijua wanaonekana live.....
BR. UMECHEMSHA KUONYESHA BUNGE SI KWA AJILI YA UKAWA NI KWA AJILI YA SIE MAKABWELA NA SIO SEHEMU KUONYESHA UMAARUFU KAMA HUJUI KUCHANGIA HOJA UTALAZIMISHA KUONEKANA,
 
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na
Michezo, Nape Moses Nnauye, amesema
Televisheni ya Taifa imeacha kurusha LIVE
kipindi cha Bunge kuanzia jana ili kubana
matumizi. Na itakuwa ikirekodi baadhi ya
matukio na kuonyesha usiku.

Kama mtanzania, unadhani unatendewa
haki?
Tunaomba na mishahara ya hao mawaziri ifutwe ili tuendelee kufanya matumizi vizuri
 
Zile bilions za NIDA, bandari zifanye nn? shirikisha ubongo wako wewe

NIDA bado uchunguzi unaendelea na za Bandari subiri kidogo bajeti ikianza kujadiliwa utajua.

Hivi ile hoja ya wabunge Wa UKAWA kuchangia mfuko Wa jimbo na KUKATAA maposho makubwa makubwa imeishia wapi?

Queen Esther
 
Ninakijua sana kwamba watu wafanye kazi na waache uvivu kwa kuanglia luninga muda ambao walipaswa wafanye uzalishaji na kuongeza kipato chao na cha nchi kwa ujumla!

SAFI SANA W. NAPE!
Ungekua unakijua ulichokiandika ungefahamu tu kua sio kila anaemiliki TV na anataka kuangalia bunge Live Mchana ni muajiriwa!!
 
Back
Top Bottom