TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Magufuli mawaziri alio chagua ndio wanao muangusha.. Nape alikuwa anapita mikoani akiita wenzie mizigo.. Kumbe yeye ndio zigo la kwanza... Ndio maana mh kikwete mawaziri wake aliwapa semina elekezi
 
TBC CCm , baada ya TIdo Mhando kuondoka TBC basi chombo hikincha habari kiliyumba kwa kiasi kikubwa sana na hii ni laana kutoka kwa mwenyezi mungu maana TIdo aliitoa tbc mbali lakini alilipwa kufukuzwa kazi, Tbc wanaonyeshaga tamthiliya za wadada wakiwa uchi hivi nano analipia vile vipindi? wanaonyeshaga miziki ya wadada wakiwa uchi nani ana gharamia vile vipindi? Star tv na Azam wanao onyesha live masaa yote nani anagharamia Vile vipindi. Ujio NEPI NI MKAKATI WA KUDUMAZA UHURU WA KUPATA HABARI.ULIANZA NA MAWIO UMEHAMIA TBC CCM KESHO UTAMALIZIA AZAM, STAR TV, ITV N.K
 
Wananchi wale tu hata wanaofanya kazi na kulipa PAYE tunaweza kutolewa hata shilling Mmoja kulipia matangazo ya Bunge Hivi nape huwaga anamka toka usingizini ati wananchi tumeafiii mlitupa tupige kura ya maoni katika uamuzi huuu kwani Nape unaleta mzaha kwenya mambo ya msingi Rais JPM huyu ndio umeona anafaaaa kwenye wizara ya Habari au ndio mbinu mbadala wa kuuwa vyombo vya habari mbona mnakinzana saaana na hali ahalisi ya ulimwengu wenzenu Media ndio kitu muhimu kuwaelimisha wananchi nyie mnakifungia na kukipa mashariti ya ajabu saaana

kaka hii nchi viongozi wetu hukurupuka sana kama vile yule mkurupukaji wa futuhi, unakumbuka kuna mwaka 1 walileta sheria kuwa ati ukikonyeza mwanamke unaenda kuchezea mvua ya miaka mi5 jela, ikaleta mzozo sana bungeni, sasa sijui alifikiria nini yule mtu kupelekwa kitu kama hicho kikaongelewe bungeni, hapa kwa kweli wamekurupuka, paye tunakatwa na zinaenda wapi hizo pesa, manake hatuoni msaada wake, kama ni madawa, ni misaada kutoka nje, barabara ni misaada kutoka nje, au hizo ni za kuwapeleka wao nje kwa matibabu n.k.
 
sawasawa kabisa Serikali! hivi watanzania wataendelea lini? kama tunaendelea kuentatein gharama za ajabuajabu; hizo gharama za kurusha matangazo siku nzima wakati vijiji watu hawana barabara, hawana maji, hawana vyakula acheni kuwa selfish!
 
duuuh_!!! hii nayo kali... alafu watazania mnajiita kisiwa cha amani?!!! tehtehteh hiki ni kisiwa cha woga amani hakuna.... Uhuru pia hakuna km tumenyimwa Uhuru wa habar kuna Uhuru mwingine.....TV ya taifa ishindwe kuonesha vpindi vya bunge live at kisa kubana matumizi ....hakyamungu hii too much... .hivi kwanin hii nchi tusiiuze tu tugawane chetu tukaishi ata somalia.au kwa nkurunzinza?!
 
Kwendeni huko na ki-tbc chenu! Tv zimejaa kibao wala haitutishi! Tuna ITV, AZAM na Star TV
 
Baadhi ya watu hum ndani kweli vichwa maji. "Eti hakuna shida kwani TBC imebadilisha tu muda; badala ya kuangalia asubuhi na jion km tulivozoea tutaangalia bunge ucku" "Vile vile eti eti serikali inabana matumizi"

Kiukweli anayeshabikia vikao vya bunge visirushwe live ana akili "MATOPE" Niliwaambia kuwa kuna kitu kingine nyuma ya pazia watu wanabisha. Lengo kuu la TBC ni kufanya selection ya vitu gan ndani ya bunge vioneshwe na vipi visioneshwe.

Mfano halis ni leo ijumaa tarehe 29/01/2016, TBC na hcho kipind chao walichokibatiza jina la " "bungeni leo" wameanza saa 22:16 na wamemaliza saa 23:04 that means hta saa haijaisha. Mchango wa baadhi ya wabunge km Zitto haujaoneshwa! Hii inamaana kwamba wameonesha kipisi tu cha kikao cha leo
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimefuatilia sana mjadala unaoendelea bungeni hususani hoja iliyotolewa na serikali juu ya kutorusha Live baadhi ya mijadala bungeni. Hakika iam totally confused. Ukisikia michango ya wabunge na baadhi ya wadau humu mitandaoni hakika unakuja kugundua kuwa ama hii hoja imepokelewa kisiasa ama kuna watu wameamua kujivika ujinga. Nasema haya kutokana na jinsi michango ya watu ilivyo.

Ukisikiliza na kuangalia kwa jicho pevu michango hiyo utagundua kuwa kweli tuna safari ndefu. Wapo wanaoamini kuwa Serikali haitaki mikutano ya bunge irushwe live kwa sababu haitaki wananchi waone mijadala inayoendelea bungeni kwa lengo la kuwakandamiza wapinzani. Wengine wanasema kuwa serikali inataka kuedit kwanza michango ya wabunge ndipo iwafikie wananchi. Wengine wanasema serikali ni waoga sana na hivyo wanaogopa michango ya wapinzani.

Hakika hoja zote hizi ni za kijinga. Kwanini nasema hivyo kwasababu serikali haijapiga marufuku kuoneshwa live kwa vikao vya bunge. TBC1, Star TV na Azam TV wamekuwa wakirusha hewani kipindi cha maswali na majibu bungeni. Then Star TV na Azam TV kupitia Channel ya Xtra wamekuwa wakirusha moja kwa moja mijadala yote inayoendelea bungeni.

Hakika nimestaajabu sana kuona wabunge wetu wamekuwa wakitoa mapovu kwa mambo yasiyo na tija as if sisi wananchi hatujui nini kinaendelea. Serikali imekuwa very clear kueleza kwa nini wamechukua maamuzi hayo. Hivyo basi wapinzani kuweni wawazi. Msitudanganye sisi wananchi.
 
Ukiwafutilia sana hawa waweza jikuta unapata vidonda vya tumbo kwanza nashangaa walisema tbc hua hawangalii hii channel sasa kinachowatoa mapovu ni nini ili khali channel zao pendwa zinaonyesha hiyo mijadala ya bunge pia nilichoweza jifunza kwao ni unafiki tu na gubu.
 
mtoa mada huna hoja. cha msingi kama ulivyotangulia kusema ume confuse. kinachopiganiwa na wabunge wetu ni shirika la umma TBC kurusha LIVE vikao vyote vya bunge ili waajiri wa wabunge wajue nini kinafanywa na wabunge wao bungeni. hoja ya kusema kwamba star tv na Azam kurusha live haiondoi hoja ya msingi ya kuitaka TBC iende live. kwani tbc ni chombo kinachoendeshwa kwa kodi zetu. star tv na azam hawalazimiki kurusha mikutano ya bunge bali nimapenzi yao tu kwa taifa letu na watu wake.
 
Kwanza cha kushangaza ni lini wameanza kuwa na mahaba na TBC? Mimi nahitaji siku wapigane kuondoa sitting allowance!

Nilipomsikiliza Kubenea aliposema wabunge waupinzani walivuliwa chupi na shanga hapo ndio nilijiuliza ndiyo haya wanataka yawe live?
Kimsingi kipindi cha maswali na majibu ndicho kilicho takiwa kionekane live!
 
Serikali inabana matumizi kama kuna chombo kinaweza kuonesha kioneshe...hatuwezi kupoteza billion 4 kuonesha live watu wanaosema rafiki zao wamechukuliwa chupi na shanga....
 
Kwanza cha kushangaza ni lini wameanza kuwa na mahaba na TBC? Mimi nahitaji siku wapigane kuondoa sitting allowance!

Nilipomsikiliza Kubenea aliposema wabunge waupinzani walivuliwa chupi na shanga hapo ndio nilijiuliza ndiyo haya wanataka yawe live?
Kimsingi kipindi cha maswali na majibu ndicho kilicho takiwa kionekane live!
hoja hii haiondoi umuhimu na ulazima wa tbc kurusha bunge live kamwe.watanzania tunataka uwazi. tbc ilikuwa inapata watazamaji wengi kipindi cha vikao vya bunge tu...
 
mtoa mada huna hoja. cha msingi kama ulivyotangulia kusema ume confuse. kinachopiganiwa na wabunge wetu ni shirika la umma TBC kurusha LIVE vikao vyote vya bunge ili waajiri wa wabunge wajue nini kinafanywa na wabunge wao bungeni. hoja ya kusema kwamba star tv na Azam kurusha live haiondoi hoja ya msingi ya kuitaka TBC iende live. kwani tbc ni chombo kinachoendeshwa kwa kodi zetu. star tv na azam hawalazimiki kurusha mikutano ya bunge bali nimapenzi yao tu kwa taifa letu na watu wake.
Hiyo bilioni nne ingeenda kuboresha upatikanaji wa matangazo ya TBC katika mikoa ya pembezoni badala ya kurusha porojo za shanga zinazotolewa na kina kubenea
 
Sasa mbona unasema mtoa mada hana hoja na wakati umemjibu swali lake
 
Hiyo bilioni nne ingeenda kuboresha upatikanaji wa matangazo ya TBC katika mikoa ya pembezoni badala ya kurusha porojo za shanga zinazotolewa na kina kubenea
kwani kutaja shanga ni jambo la ajabu? tunapoteza pesa nyingi zaidi ya bilioni 4 kwa mambo ya hovyo...
 
uzi umekosa wachangiajii

Naomba wote mnao jielewa tumpuuze huyu nyumbu kwa kuto reply chochotee.

Weka like kwangu kuunga mkono kauli hii.
Umekosa wachangiaji wakati wewe umechangia?
 
Back
Top Bottom