TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

kwani kutaja shanga ni jambo la ajabu? tunapoteza pesa nyingi zaidi ya bilioni 4 kwa mambo ya hovyo...
Sio jambo la ajabu kwa shanga kutajwa unapokuwa na hawara yako chumbani au unapokuwa kwenye vijiwe vya kahawa lakini unapokuwa kwenye bunge tukufu la JMT halafu unaongelea shanga za kiuno na kuvuana chupi hapo napata wasiwasi wa uwezo wako wa kifikra.
 
mtoa mada huna hoja. cha msingi kama ulivyotangulia kusema ume confuse. kinachopiganiwa na wabunge wetu ni shirika la umma TBC kurusha LIVE vikao vyote vya bunge ili waajiri wa wabunge wajue nini kinafanywa na wabunge wao bungeni. hoja ya kusema kwamba star tv na Azam kurusha live haiondoi hoja ya msingi ya kuitaka TBC iende live. kwani tbc ni chombo kinachoendeshwa kwa kodi zetu. star tv na azam hawalazimiki kurusha mikutano ya bunge bali nimapenzi yao tu kwa taifa letu na watu wake.



Lkn na sisi pia hatutaki chombo chetu kinachoendeshwa na kodi zetu kirushe Bunge wakati ambapo tuko kazini tunataka TBC yetu irekodi na kuonyesha Bunge jioni tukisharudi nyumbani na tuko wengi sana!
 
Lizaboni hujawahi toa hoja zenye mlengo wa kitaifa wewe hoja zako zinamlengo wa kichama ingawa ndo mnufaikaji wa huo uchama but sometimes you have to stand on right side, namkubali mzee tupa-tupa lkn wewe ni shiiiiiidaaa uko tayari hata kuchinja ilimradi maisha yako yaendelee
 
Ukiwa na akili una akili tu. Iko hivi tbc inapatikana kwa urahisi zaidi kwa sababu ukiwa na almost king'amuzi chochote tz unaweza kupata tbc so kama king'amuzi chako star tv haipo au azam tv haipo that means hutapata habari za bunge. So logically hoja ya upinzani ipo hapo. MAJORITY MJOMBA. Please understand.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimefuatilia sana mjadala unaoendelea bungeni hususani hoja iliyotolewa na serikali juu ya kutorusha Live baadhi ya mijadala bungeni. Hakika iam totally confused. Ukisikia michango ya wabunge na baadhi ya wadau humu mitandaoni hakika unakuja kugundua kuwa ama hii hoja imepokelewa kisiasa ama kuna watu wameamua kujivika ujinga. Nasema haya kutokana na jinsi michango ya watu ilivyo.

Ukisikiliza na kuangalia kwa jicho pevu michango hiyo utagundua kuwa kweli tuna safari ndefu. Wapo wanaoamini kuwa Serikali haitaki mikutano ya bunge irushwe live kwa sababu haitaki wananchi waone mijadala inayoendelea bungeni kwa lengo la kuwakandamiza wapinzani. Wengine wanasema kuwa serikali inataka kuedit kwanza michango ya wabunge ndipo iwafikie wananchi. Wengine wanasema serikali ni waoga sana na hivyo wanaogopa michango ya wapinzani.

Hakika hoja zote hizi ni za kijinga. Kwanini nasema hivyo kwasababu serikali haijapiga marufuku kuoneshwa live kwa vikao vya bunge. TBC1, Star TV na Azam TV wamekuwa wakirusha hewani kipindi cha maswali na majibu bungeni. Then Star TV na Azam TV kupitia Channel ya Xtra wamekuwa wakirusha moja kwa moja mijadala yote inayoendelea bungeni.

Hakika nimestaajabu sana kuona wabunge wetu wamekuwa wakitoa mapovu kwa mambo yasiyo na tija as if sisi wananchi hatujui nini kinaendelea. Serikali imekuwa very clear kueleza kwa nini wamechukua maamuzi hayo. Hivyo basi wapinzani kuweni wawazi. Msitudanganye sisi wananchi.
Information is knowledge:: ww ujui kama nape anasema sababu mojawapo ya kuondoa bunge lisirushwe live ni kuwafanya wafanyakazi wafanye kazi na sio kukomaa na bunge mwa mwii
 
Hoja sio bunge kurushwa live. Hoja ni bunge kurushwa live na Televisheni ya Taifa. Tunapoita Televisheni ya Taifa ina maana ya kuwa inaendeshwa na kodi ya wananchi wa Tanzania. Na moja kati ya haki za kikatiba ni ile ya uhuru wa kupata ama kutafuta habari. Sasa unapotaka kusitisha kurusha moja kwa moja ni kuwanyima haki watanzania.

Hebu labda nikuulize, hakimu anayehukumu wahalifu kifungo cha miaka kadhaa jela, endapo akatenda kosa na kupewa nafasi/uhuru wa kujihukumu mwenyewe je atajihukumu ama atajiweka huru?

Kinachoenda kutokea ni kuwa, serikali kupitia TBC haitakuwa tayari kuona inaaibika mbele ya wananchi wake pale wanapoboronga kwa kurusha matangazo yaliyorekodiwa eti kuonesha waliopoboronga. Lazima wataonesha pale walipopatia na kusifiwa. Pia jiulize baada ya maswali na majibu, kipindi cha bunge kinaendelea kwa saa 5 (saa 5 hadi saa 7 na saa 11 hadi saa 2 usiku) sasa hebu niambie muda wa saa moja utatosha kuonesha yale ya muhimu yaliyojiri?

Kuhusu chaneli binafsi kuonesha moja kwa moja (Star Tv na Azam TV) sio sababu zenye mashiko za kufanya TBC kupata uhalali wa kutoonesha moja kwa moja. Hii ni kwa sababu zifuatazo:

1. Vyote hivyo ni vyombo binafsi kwahiyo wakiamua saa yeyote kuonesha vipindi vingine badala ya bunge hakuna wa kuwauliza. Ila TBC wakikata matangazo wataulizwa.
2. Star Tv tunaifahamu mrengo wake wa kisiasa. Wakati wowote wanaweza kushinikizwa na kutorusha moja kwa moja. (Hili liko wazi hata umiliki wake)
3. Si watu wote wenye uwezo wa kuipata Azam TV. Tunafahamu Azam Tv inapatikana kwenye visimbuzi vya Azam Tv pekee. Mpaka leo kuna baadhi ya watu wanatumia madish ya LNB na wengine visimbuzi vya Star Times, Zuku na vingine. Hivyo kuipata Azam Extra ni vigumu.

Hivyo basi suluhuhisho pekee ni kuiacha TBC ambayo ni mali ya kila Mtanzania ioneshe live.

Magnesium
 
#Lizaboni wewe shukuru tu unakula kwa njia ya chama basi. Haya matatizo mengine waachie wananchi wayapiganie wenyewe, hata wewe kupata hako kamkondo ulipigana. Sasa tulia na ule kwa urefu wa kamba yako, ya Ngoswe muachie Ngoswe zaidi ya hapo unaharibu kiongozi.
 
Usilolijua kweli ni usiku wa giza.... Pole sana ndugu yangu kwani sielewi kama hujui au unajifanya hujui..
Kwa taarifa yako TBC peke yao ndio wanaruhusiwa kurekodi matukio bungeni lakini kurusha yeyote anaruhusiwa .. Sasa kama mtu anayeruhusiwa kurekodi akizuiliwa hao warushaji watarusha nini..???? ....
Kama vituo vingine vya tv vingeruhusiwa kurekodi na kurusha kungekuwa hakuna malumbano bungeni. Kma wewe unakumbukumbu utakumbuka kuwa zamani kila kituo cha tv kilikuwa kina mwakiliahi wake bungeni wa kurekodi , serikali ikatunga sheria kuzuia hilo na haki zote za kurekodi bungeni kurasimiwa kwa TBC
Kamanda lizbon umenisikitisha sana unaposema kuwa serikali IMELETA HOJA bungeni, serikali hijaleta hoja bungeni kimsingi IMELETA TAARIFA au imeleta amri !!!!!
Kama Nape angekuwa na uweledi na akili hili jambo ni dogo sana angefuata utaratibu tu ... Angeleta hoja ijadiliwe bungeni na kwa vile ccm wako wengi bungeni wangepitisha kilaini.. Lakini nape akilini kwake ni 0
 
kamanda nashauri utoe ushauri wa vyanzo vya mapato ambavyo vitaendelea kutufanya tutumie bilioni hizo kwa mwaka ili tu enjoy matangazo ya bunge.
Kwani TBCCM imeanza kuonesha matangazo live Leo? Mbinu mbovu zenu za Kidikteta tulishazistukia mapeema.
 

Serikali imechukuwa uamuzi sahihi kabisa, ilikuwa inafikia wakati unakwenda ofisini kupata huduma wafanyakazi wamekodoa kwenye luninga wanaangalia Bunge, Nasema SAFI SANA NAPE!
Basi na ofisi zote zisiwe na TV maana si kweli kuwa kinanchoangaliwa kweny TV ni Bungetu! Jiongeze acha kutumia akili za mizoga kuwaza.
 
Basi na ofisi zote zisiwe na TV maana si kweli kuwa kinanchoangaliwa kweny TV ni Bungetu! Jiongeze acha kutumia akili za mizoga kuwaza.


Ukiniulza mimi, ndiyo zilipaswa TV ziondolewe, ingawaje ni kweli kwamba kinachoangaliwa siyo Bunge tu lkn wakati wa Bunge huwa ni shida hata kupata huduma mara nyingi sana nimeshacheleweshewa huduma Benki kwa kuwa walikuwa wamekodolea Bunge wakati wanapashana!

Hivyo Naunga HOJA kwa 100%!
 
Ukiniulza mimi, ndiyo zilipaswa TV ziondolewe, ingawaje ni kweli kwamba kinachoangaliwa siyo Bunge tu lkn wakati wa Bunge huwa ni shida hata kupata huduma mara nyingi sana nimeshacheleweshewa huduma Benki kwa kuwa walikuwa wamekodolea Bunge wakati wanapashana!

Hivyo Naunga HOJA kwa 100%!
Ndiyo uelewa wako siwezi kukulaumu! Nadhani jana mmejitathimini mlivyo watupu baada ya TL na Zitto kuwaambua na umbumbumbu wenu. Kumuelimisa Mpumbavu ni gharama kweli.
 
Ndiyo uelewa wako siwezi kukulaumu! Nadhani jana mmejitathimini mlivyo watupu baada ya TL na Zitto kuwaambua na umbumbumbu wenu. Kumuelimisa Mpumbavu ni gharama kweli.


Pole sana, kwa maana una kazi kubwa sana ya kutuelewesha kwa maana ndiyo tulio wengi wengi na ndiyo wenye nchi sasa, hapo sasa sijui utafanyaje, lkn habari ndiyo hiyo TBC hakuna Bunge live Serikali yetu imeamua na tunatii, Mahakama ya Mafisadi inakuja na mafisadi wote lazima mtaozea lupango tu, nusu nzima ya chadema ni Mafisadi kuanzia viongozi mpaka wanachama wote fisadis!
 
Mtaisoma Naaambaaa guilt are always afraid ,,,wanaogopa nini kama wao hawana pesa wawaruhusu wenye pesa warecord na kurusha
 
Mjadala wa TBC umepamba moto. Mimi kama mdau wa habari naomba kutoa mchango wangu kama ifuatavyo

Kuna kitu kuhusu TBC ambacho serikali inakijua lakini inajitia pamba masikioni na TBC Management wanakijua lakini badala ya kukitekeleza, wanabaki na kazi ya kujikomba komba kwa serikali as if kitendo cha kugharimiwa na serikali it's just a favour na sio right ndio maana kila siku inaomba kiasi fulani cha budget ili itekeleze majukumu yake kikamilifu lakini inapewa kuduchu.

Kitu hicho dhana kuwa TBC ni Television ya Serikali hivyo serikali inaitumia jinsi vile inaona inafaa kwa manufaa ya serikali.

Kiukweli TBC sio TV ya serikali. TBC ni TV ya Umma wa Watanzania, wenye TV hiyo ni Watanzania. Serikali inayo haki ya kuitumia TBC kama mteja mwingine yoyote tena bila any preferential treatment yoyote! .

Lakini kinachofanyika ni kinyume. Serikali ndio inajiona ni mmiliki wa TBC, na TBC kazi yake ni kujikombakomba na kulamba miguu ya serikali.

TBC kama Public Television Station haiwajibiki kwa serikali, inawajibika kwa umma kupitia an independent board free of government biases! .

TBC inatakiwa kuwa funded by the government as an obligation and not as a favour. TBC ipewe fedha za kutosha bila kupigwa panga lolote! . Fedha za TBC ziwe statutory kama zilivyo fedha za SDL (Skills Development Levy) ambazo zinakatwa moja kwa moja toka kwenye sources kama kodi inavyokatwa.

Ikiwa hivi TBC yenyewe kupitia bodi yake ndio itakuwa huru kutangaza nini live na nini kutotangaza live na kama kuna tukio lolote la yoyote linataka kutangazwa live kitu cha Kwanza kuangaliwa ni maslahi ya Taifa kisha hiyo live ilipiwe. Kama ni Bunge live, bunge lilipe.

Kulipia huku hakutaondoa jukumu la TBC kutangaza bure tukio lolote lenye maslahi mapana ya Taifa.

Mjadala huu sasa unatoa fursa ya kuijadili TBC na kuiondoa katika umiliki wa serikali uliyoiteka na kuiweka chini ya umiliki wa umma ambao ndio wa haki.
Pasco.
Mwandishi wa makala hii aliwahi kuwa Mtumishi wa TBC. Mwaka 2002 alitimuliwa kazi kwa summary dismissal kwa kosa la insubordination.
 
Maparachichi yanaongeza uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo, nafikri umeleta hii hoja makusudi ili Lizaboni anunue mwambie direct "kula parachichi uengeze uwezo wa kufikiri" unamwogopa,,
 
Safi sana... ni waTZ wachache wanaojielewa kwa kiwango hiki
 
Back
Top Bottom